Mwakyembe azungumzia Kauli ya Kabudi kuwa Azory Gwanda amefariki

Huyu Mwakyembe naona majukumu yamemuelemea hadi majukumu yanamshinda. Mfano alishindwa kama waziri mwenye dhamana kwenda kuipa nguvu Stars Afcon na kuiacha jukumu hilo kufanywa na Mkuu wa mkoa. Leo Kabudi kumsemea kuwa Azory alitoweka na kufa anajifanya hajasikia. Utawala huu naona rais kama wasaidizi wake vipimo vya viatu vyao haviendani na kasi
Haswaaa, huyu jamaa anafeli wapi? Issue ya RICHMOND nayo alifeli?
 
Aliliwasilisha lini mambo ya ndani? Na hiyo ripoti kuhusu kupotea kwa Mtanzania mwenzetu Azory Gwanda aliambiwa itakuwa tayari baada ya muda gani?

Vipi kuhusu kupotea kwa Ben Saanane na kutekwa na kuteswa kwa Watanzania wenzetu wengine Lugola na uhamiaji mbona wako kimya!? Serikali yote mbona iko kimya pamoja na muda mrefu kupita!?

!
!
Kabudi Anafahamu Kilichomtokea Azory. Na Ameshakisema.
Sasa Haya Mengine Ni Kumfurahisha Mkuu Tu Kila Mmoja Anakuja Na Maelezo Yake. Ni Huyu Huyu Mwakyembe Alinukuliwa Akisema Kama Mtu Kaondoka Mwenyewe Wamfanyaje
 
July 11, 2019
Bonn, Germany

Waziri Harrison Mwakyembe mwenye dhamana ya kusimamia habari Tanzania katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani DW, ametofautiana na kauli ya waziri wa mambo ya nje ya Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi.

Harrison Mwakyembe amesema hawezi kusema kwa uhakika kilichomtokea mwandishi wa habari aliyetoweka ktk mazingira ya utatanishi na kuongeza aliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ili walichukulie kwa uzito suala hilo.

Mh. Harrison Mwakyembe akaongeza kuwa suala hilo kwa vile aliwasiliana na kuliwakilisha kwa vyombo vya usalama, anasubiri ripoti kamili toka vyombo hivyo.

Wakati huohuo wanaharakati wameanza kuichagiza serikali ya Tanzania kutoa ripoti kamili kuhusu yaliyomkuta mwanahabari huyo aliyetoweka baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi, kuthibitisha kifo cha mwandishi wa habari huyo Bw. Azory Gwanda.

Tunaimani na kabudi ccm iache chenga,watajulikana tu wasiojulikana hakuna namna
 
Miaka miwili bado tu anasubiri ripoti
 
Wangemuhoji kwa Kingereza naye angeteleza tu kama mwenzake ....... Hata Kabudi kwenye interview ya Kiswahili kwa jambo lile lile alihandle vizuri sana.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom