Mwakyembe azungumzia Kauli ya Kabudi kuwa Azory Gwanda amefariki

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,031
23,822
July 11, 2019
Bonn, Germany

Waziri Harrison Mwakyembe mwenye dhamana ya kusimamia habari Tanzania katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani DW, ametofautiana na kauli ya waziri wa mambo ya nje ya Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi.

Harrison Mwakyembe amesema hawezi kusema kwa uhakika kilichomtokea mwandishi wa habari aliyetoweka ktk mazingira ya utatanishi na kuongeza aliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ili walichukulie kwa uzito suala hilo.

Mh. Harrison Mwakyembe akaongeza kuwa suala hilo kwa vile aliwasiliana na kuliwakilisha kwa vyombo vya usalama, anasubiri ripoti kamili toka vyombo hivyo.

Wakati huohuo wanaharakati wameanza kuichagiza serikali ya Tanzania kutoa ripoti kamili kuhusu yaliyomkuta mwanahabari huyo aliyetoweka baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi, kuthibitisha kifo cha mwandishi wa habari huyo Bw. Azory Gwanda.
 
LK. :6:45
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Inawezekana Prof ndani ya Moyo wake aidha kwa kufahamu au kwa kusikia anajua kilichomkuta Azory na alichokisema ni sahihi kabisa maana kinywa hunena kile kilichomo moyoni mwake
 
Kabudi kazungumza kwa uhalisia wa Jambo air Malaysia iliipotea na watu zaidi ya 270.

Ripoti ya mwisho ya serikali ya Malaysia inaamini watu wote waliokuamo katika ndege iyo wamepoteza maisha.

the same to Mr azory, Paramaganba Kama waziri Ana uhakika na serikali inajua Azori hayupo ndani wala nje ya mipaka ya Tanzanania kwa lugha laisi lazima utasema kafariki.
 
Aliliwasilisha lini mambo ya ndani? Na hiyo ripoti kuhusu kupotea kwa Mtanzania mwenzetu Azory Gwanda aliambiwa itakuwa tayari baada ya muda gani?

Vipi kuhusu kupotea kwa Ben Saanane na kutekwa na kuteswa kwa Watanzania wenzetu wengine Lugola na uhamiaji mbona wako kimya!? Serikali yote mbona iko kimya pamoja na muda mrefu kupita!?
 
Huyu Mwakyembe naona majukumu yamemuelemea hadi majukumu yanamshinda. Mfano alishindwa kama waziri mwenye dhamana kwenda kuipa nguvu Stars Afcon na kuiacha jukumu hilo kufanywa na Mkuu wa mkoa. Leo Kabudi kumsemea kuwa Azory alitoweka na kufa anajifanya hajasikia. Utawala huu naona rais kama wasaidizi wake vipimo vya viatu vyao haviendani na kasi
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom