July 11, 2019
Bonn, Germany
Waziri Harrison Mwakyembe mwenye dhamana ya kusimamia habari Tanzania katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani DW, ametofautiana na kauli ya waziri wa mambo ya nje ya Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi.
Harrison Mwakyembe amesema hawezi kusema kwa uhakika kilichomtokea mwandishi wa habari aliyetoweka ktk mazingira ya utatanishi na kuongeza aliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ili walichukulie kwa uzito suala hilo.
Mh. Harrison Mwakyembe akaongeza kuwa suala hilo kwa vile aliwasiliana na kuliwakilisha kwa vyombo vya usalama, anasubiri ripoti kamili toka vyombo hivyo.
Wakati huohuo wanaharakati wameanza kuichagiza serikali ya Tanzania kutoa ripoti kamili kuhusu yaliyomkuta mwanahabari huyo aliyetoweka baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi, kuthibitisha kifo cha mwandishi wa habari huyo Bw. Azory Gwanda.