Mwakyembe azuia watumishi wizara yake kupanda daraja la kwanza kwenye ndege

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,868
30,337
mwakyembe.jpg
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe

KWA UFUPI

“Kulingana na hali halisi ya maisha ya baadhi ya ya Watanzania, wizara yangu haitakuwa tayari kuona fedha zikitafunwa na watu wachache kwa njia za kifisadi. Matumizi yafanyike kulingana na hali halisi ya Watanzania,” alisema Mwakyembe na kuongeza;


WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewapiga marufuku wafanyakazi wote walio chini ya wizara yake kusafiri kwa ndege katika daraja la kwanza, akieleza kuwa huo ni ubadhirifu wa fedha za umma.Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga jana, Mwakyembe alisema atakayekaidi agizo hilo, atakatwa fedha katika mshahara wake.


Mwakyembe ambaye tangu ateuliwe kuwa Waziri wa Uchukuzi amekuwa akifanya uamuzi magumu, alisema hawezi kuvumilia
mtu yeyote ambaye atatumia hovyo fedha za walipa kodi, huku akiwataka wafanyakazi wa wizara yake kufanya kazi kwa maadili na kuwatumikia wananchi.

“Kulingana na hali halisi ya maisha ya baadhi ya ya Watanzania, wizara yangu haitakuwa tayari kuona fedha zikitafunwa na watu wachache kwa njia za kifisadi. Matumizi yafanyike kulingana na hali halisi ya Watanzania,” alisema Mwakyembe na kuongeza;

“Kuanzia leo nawapiga marufuku watendaji wote wa wizara yangu kusafiri na ndege kwa kutumia daraja la kwanza.”

Akizungumzia hali za Mamlaka za Bandari Tanzania (TPA), Dk Mwakyembe alisema, Wizara yake imeunda bodi ya watu wanane ambao wataanza kazi Januari mwakani. Alisema kikosi kazi hicho, kitaleta mapinduzi ya utendaji wa kazi katika mamlaka hiyo.

Alisema bodi hiyo itatambulishwa mara baada ya kukamilika kwa baadhi ya mambo muhimu na hivyo kuwataka wananchi kuwa wavumilivu.

Alisema kwa sasa bodi hiyo imeanza mikakati ya kuhakikisha Tanzania inaingia kwa nguvu zote katika soko la ushindani la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Alisema Wizara yake inakusudia kuleta mageuzi katika sekta ya usafirishaji katika bandari zake (PTA) ili kuweza kuleta ushindani wa kibiashara na nchi jirani na kuweza kuwavutia wafanyabiashara watakaoweza kushusha shehena zao katika bandari zake.

‘Baada ya kuunda bodi mpya ya watu wanane ya (PTA), tumedhamiria kwa dhati kuondoa madudu ambayo yalikuwa yanatusumbua katika bandari zetu na kuonekana kama tumeshindwa,” alisema Dk Mwakyembe.
Akizungumzia kuhusu Bandari Mpya ya Mwambani ambayo ujenzi wake bado haujaanza, Waziri Mwakyembe, alisema wale ambao wana ubeza mradi huo mwisho wake wataumbuka kwani ndani ya miezi sita ijayo utaanza.

Alisema mradi huo wa kujenga bandari mpya utaanza ndani ya miezi sita ijayo, hivyo wale ambao wamekuwa wakiubeza na kuleta upinzani watambue kuwa mradi huo upo na utaendelea kuwepo na Serikali itahakiksha inatekeleza azma yake.

“ Hao wapinzani wanaoubeza mradi huu wajue kuwa mwisho wake wataumbuka kwani mradi upo na ndani ya miezi sita tutaanza kwani kila kitu kiko tayari na bado utekelezaji wake tu” alisema Dk Mwakyembe.

Kuhusu bandari ya nchi kavu Mwakyembe alisema itajengwa Wilayani Korogwe sambamba na mradi wa reli ambao utakuwa mkombozi kwa watu Korogwe na maeneo ya jirani husasuani kwa wafanyabiashara.

Alisema bandari hiyo ambayo itajengwa sambamba na mradi wa reli utaweza kuwanufaisha wananchi wa Tanga na mikoa jirani kwani mbali ya ajira pia wataweza kujitafutia masoko katika nchi jirani.
Mwakyembe azuia watumishi wizara yake kupanda daraja la kwanza kwenye ndege - Biashara - mwananchi.co.tz 

nlambaa

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
361
55
Aitoshi kwa Mwakyembe peke yake, agizo hili lilitakiwa litolewe na waziri mkuu au na katibu mkuu kiongozi kwa watumishi wote wa serikali. Kampuni nyingi binafsi zina utaratibu huu wa kutumia madaraja ya kawaida kwa watumishi wake wanaposafiri kwa ndege.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom