Mwakyembe azuia watumishi wizara yake kupanda daraja la kwanza kwenye ndege

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281
mwakyembe.jpg

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewapiga marufuku wafanyakazi wote walio chini ya wizara yake kusafiri kwa ndege katika daraja la kwanza, akieleza kuwa huo ni ubadhirifu wa fedha za umma.Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga jana, Mwakyembe alisema atakayekaidi agizo hilo, atakatwa fedha katika mshahara wake.

Mwakyembe ambaye tangu ateuliwe kuwa Waziri wa Uchukuzi amekuwa akifanya uamuzi magumu, alisema hawezi kuvumilia
mtu yeyote ambaye atatumia hovyo fedha za walipa kodi, huku akiwataka wafanyakazi wa wizara yake kufanya kazi kwa maadili na kuwatumikia wananchi.

“Kulingana na hali halisi ya maisha ya baadhi ya ya Watanzania, wizara yangu haitakuwa tayari kuona fedha zikitafunwa na watu wachache kwa njia za kifisadi. Matumizi yafanyike kulingana na hali halisi ya Watanzania,” alisema Mwakyembe na kuongeza;

“Kuanzia leo nawapiga marufuku watendaji wote wa wizara yangu kusafiri na ndege kwa kutumia daraja la kwanza.”

Akizungumzia hali za Mamlaka za Bandari Tanzania (TPA), Dk Mwakyembe alisema, Wizara yake imeunda bodi ya watu wanane ambao wataanza kazi Januari mwakani. Alisema kikosi kazi hicho, kitaleta mapinduzi ya utendaji wa kazi katika mamlaka hiyo.

Alisema bodi hiyo itatambulishwa mara baada ya kukamilika kwa baadhi ya mambo muhimu na hivyo kuwataka wananchi kuwa wavumilivu.

Alisema kwa sasa bodi hiyo imeanza mikakati ya kuhakikisha Tanzania inaingia kwa nguvu zote katika soko la ushindani la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Alisema Wizara yake inakusudia kuleta mageuzi katika sekta ya usafirishaji katika bandari zake (PTA) ili kuweza kuleta ushindani wa kibiashara na nchi jirani na kuweza kuwavutia wafanyabiashara watakaoweza kushusha shehena zao katika bandari zake.

‘Baada ya kuunda bodi mpya ya watu wanane ya (PTA), tumedhamiria kwa dhati kuondoa madudu ambayo yalikuwa yanatusumbua katika bandari zetu na kuonekana kama tumeshindwa,” alisema Dk Mwakyembe.
Akizungumzia kuhusu Bandari Mpya ya Mwambani ambayo ujenzi wake bado haujaanza, Waziri Mwakyembe, alisema wale ambao wana ubeza mradi huo mwisho wake wataumbuka kwani ndani ya miezi sita ijayo utaanza.

Alisema mradi huo wa kujenga bandari mpya utaanza ndani ya miezi sita ijayo, hivyo wale ambao wamekuwa wakiubeza na kuleta upinzani watambue kuwa mradi huo upo na utaendelea kuwepo na Serikali itahakiksha inatekeleza azma yake.

“ Hao wapinzani wanaoubeza mradi huu wajue kuwa mwisho wake wataumbuka kwani mradi upo na ndani ya miezi sita tutaanza kwani kila kitu kiko tayari na bado utekelezaji wake tu” alisema Dk Mwakyembe.

Kuhusu bandari ya nchi kavu Mwakyembe alisema itajengwa Wilayani Korogwe sambamba na mradi wa reli ambao utakuwa mkombozi kwa watu Korogwe na maeneo ya jirani husasuani kwa wafanyabiashara.

Alisema bandari hiyo ambayo itajengwa sambamba na mradi wa reli utaweza kuwanufaisha wananchi wa Tanga na mikoa jirani kwani mbali ya ajira pia wataweza kujitafutia masoko katika nchi jirani.
 
Haya haya na mawaziri watumie usafiri wa mabasi ya public wanapokwenda mikoani gari za kuwapeleka vijijini watazikuta mikoani.
 
hayo ndiyo maneno shukrani sana mh. Waziri tungepata watendaji kumi ka wewe na magufuli tungefika mbali sana
 
Hata uteuzi wake wa ile bodi ambapo ame-balance kati ya wajumbe wa bodi kutokana na imani zao za kidini unaonyesha kuwa ni mtu mwenye nia ya dhati ya kuondoa matatizo mengi yanayowakabili Watanzania sasa hivi.
 
awapige na marufuku pia kutembelea VX kuanzia naibu wake,katibu mkuu na watendaji wa idara zingine ili kukokoa fedha za umma
apige pia marufuku uagizaji wa magari ya kifahari katika wizara yake na awe wa kwanza kutembelea gari la kawaida
lenye CC 2000 ili kupunguza matumizi yasio ya lazima
kama kenya waliweza kwanini na yeye asiweze?
suala la ndege peke yake halitoshi ni kiasi kidgo sana kitaokolewa aanzie na magari
 
Mwakyembe azuia watumishi wizara yake kupanda daraja la kwanza kwenye ndege
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
Na Salim Mohammed, Tanga - Mwananchi
Posted Alhamisi,Novemba22 2012 saa 24:49 AM

KWA UFUPI
"Kulingana na hali halisi ya maisha ya baadhi ya ya Watanzania, wizara yangu haitakuwa tayari kuona fedha zikitafunwa na watu wachache kwa njia za kifisadi. Matumizi yafanyike kulingana na hali halisi ya Watanzania," alisema Mwakyembe na kuongeza;
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewapiga marufuku wafanyakazi wote walio chini ya wizara yake kusafiri kwa ndege katika daraja la kwanza, akieleza kuwa huo ni ubadhirifu wa fedha za umma.Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga jana, Mwakyembe alisema atakayekaidi agizo hilo, atakatwa fedha katika mshahara wake.
Mwakyembe ambaye tangu ateuliwe kuwa Waziri wa Uchukuzi amekuwa akifanya uamuzi magumu, alisema hawezi kuvumilia
mtu yeyote ambaye atatumia hovyo fedha za walipa kodi, huku akiwataka wafanyakazi wa wizara yake kufanya kazi kwa maadili na kuwatumikia wananchi.

"Kulingana na hali halisi ya maisha ya baadhi ya ya Watanzania, wizara yangu haitakuwa tayari kuona fedha zikitafunwa na watu wachache kwa njia za kifisadi. Matumizi yafanyike kulingana na hali halisi ya Watanzania," alisema Mwakyembe na kuongeza;

"Kuanzia leo nawapiga marufuku watendaji wote wa wizara yangu kusafiri na ndege kwa kutumia daraja la kwanza."

Akizungumzia hali za Mamlaka za Bandari Tanzania (TPA), Dk Mwakyembe alisema, Wizara yake imeunda bodi ya watu wanane ambao wataanza kazi Januari mwakani. Alisema kikosi kazi hicho, kitaleta mapinduzi ya utendaji wa kazi katika mamlaka hiyo.

Alisema bodi hiyo itatambulishwa mara baada ya kukamilika kwa baadhi ya mambo muhimu na hivyo kuwataka wananchi kuwa wavumilivu.

Alisema kwa sasa bodi hiyo imeanza mikakati ya kuhakikisha Tanzania inaingia kwa nguvu zote katika soko la ushindani la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Alisema Wizara yake inakusudia kuleta mageuzi katika sekta ya usafirishaji katika bandari zake (PTA) ili kuweza kuleta ushindani wa kibiashara na nchi jirani na kuweza kuwavutia wafanyabiashara watakaoweza kushusha shehena zao katika bandari zake.

‘Baada ya kuunda bodi mpya ya watu wanane ya (PTA), tumedhamiria kwa dhati kuondoa madudu ambayo yalikuwa yanatusumbua katika bandari zetu na kuonekana kama tumeshindwa," alisema Dk Mwakyembe.
Akizungumzia kuhusu Bandari Mpya ya Mwambani ambayo ujenzi wake bado haujaanza, Waziri Mwakyembe, alisema wale ambao wana ubeza mradi huo mwisho wake wataumbuka kwani ndani ya miezi sita ijayo utaanza.

Alisema mradi huo wa kujenga bandari mpya utaanza ndani ya miezi sita ijayo, hivyo wale ambao wamekuwa wakiubeza na kuleta upinzani watambue kuwa mradi huo upo na utaendelea kuwepo na Serikali itahakiksha inatekeleza azma yake.

" Hao wapinzani wanaoubeza mradi huu wajue kuwa mwisho wake wataumbuka kwani mradi upo na ndani ya miezi sita tutaanza kwani kila kitu kiko tayari na bado utekelezaji wake tu" alisema Dk Mwakyembe.

Kuhusu bandari ya nchi kavu Mwakyembe alisema itajengwa Wilayani Korogwe sambamba na mradi wa reli ambao utakuwa mkombozi kwa watu Korogwe na maeneo ya jirani husasuani kwa wafanyabiashara.

Alisema bandari hiyo ambayo itajengwa sambamba na mradi wa reli utaweza kuwanufaisha wananchi wa Tanga na mikoa jirani kwani mbali ya ajira pia wataweza kujitafutia masoko katika nchi jirani.
 
[h=2]Mwakyembe bans first class travel[/h][h=3]TheMinister for Transport, Dr Harrison Mwakyembe, has prohibited officials of his ministry from flying in first (business) class when travelling abroad in a bid to minimize costs.[/h]
Dr-Harrison-Mwakyembe.jpg

The Minister for Transport, Dr Harrison Mwakyembe

He warned that any official who would take a first class flight during official travel he or she will face the music including deduction of her/his salary to recover the extra money. Dr Mwakyembe made the warning at a press conference at Tanga Port, after handing over a report prepared by the Port Authority to the Board of Directors.
The minister said he wanted to have patriotic government officials who were not considering travel as a chance for free spending. “If your job description states that you will use first class when travelling abroad, you have to know that I’ve abolished such privilege and if any official wants to travel in first class may do so at his own expenses.
“It is now high time for government officials to feel the pinch of tax payers (Tanzanians) money. Most taxpayers live in abject poverty and need the same money for development projects,” he insisted. Dr Mwakyembe directed the board members to be objective and execute their functions according to the requirements of the laws and regulations that govern their board.
He further directed it to improve services at Tanzanian’s ports in order to attract more customers and boost national economy. Dr Mwakyembe was, however, optimistic that the Board would excel, as it comprised experienced, well trained members who want to see their country move forward economically.
 
Back
Top Bottom