Mwakyembe azuia watumishi wizara yake kupanda daraja la kwanza kwenye ndege

Keep it up Mh. Makyembe!! Kwani wakipanda economy class hawafiki waendako? Tena ungesema luxury bus kabisa kama lipo na ndege tu pale ambapo luxury bus haifiki!
 
Ajitoe akili, ampige marufuku na huyu ombaomba anayeruka kila siku kwa watu.
 
ukisikia maagizo ya zimamoto ndo hayo,ilipaswa kwanza tuambiwe, walikuwa wanatumia kiasi gani, hivyo kwa maamuzi hayo zitaokolewa shilingi ngapi, na zitatumika kufanyia nini na je maamuzi hayo ni ya kisera au yeye mwakyembe akiondoka anaondoka na maamuzi yake, binafsi nakerwa na maamuzi hayo yenye mrengo wa kupigiwa makofi huku hakuna nafuu yeyote kwa mwananchi au mfanyakazi wa kawaida wa eneo husika
 
uyu jamaa na magufuli nawakubali sana yani ndio viongoz wa tanzania ninao wakubali hao tu wawili

Ila mimi 6shangaa nikija kusikia wamehamishwa wizara tena ambazo hazina hata kash kash, mfano ya mazingira,
Tanzania ni zaidi ya unavoijua bana! spidi yao si kila mtu anaifurahia hasa wasiopenda kasi hii ya ajabu! Big up guys Mwakyembe n Magufuli, naona hata Kagasheki yuko vizuri kuliko the past.
 
Mwakwembe heshima kwako mkuu,wewe ni mtendaji sio mwanasiasa.!
 
Tafsiri ya hatua hii ni kuwa raisi wa nchi hii amalala usingizi wa pona.

Agizo la raisi si lingekuwa la nchi nzima.

Kudhibiti wizara moja kuna tija gani wakati nchi hii ina wizara lukuki?
 
Madaraja ya usafiri yako kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma. Wapo watumishi kwa mujibu wa nyadhifa zao wanastahili kusafiri kwa daraja la I,II na III. Kuwazuia watumishi wa wizara yake pekee huku watumishi wa taasisi nyingine za serikali wakiendelea kuponda raha,kwa maoni yangu nadhani wahusika hawajatendewa haki. Pengine ingekuwa vema kama mh. Mwakyembe angewasilisha mapendekezo ya marekebisho ya kanuni kwenye mamlaka husika ili kuzuia watendaji wote wa umma wakiwemo mawaziri kusafiri kwa daraja la kwanza. Kwa kufanya hivyo naamini tungeokoa fedha nyingi zaidi. Naunga mkono hoja yake lakini isiishie wizarani kwake tu.
 
Labda angesema hao watumishi wa wizara yake huwa wanasafiri kwenda wapi na kwa nini!! Kinyume na hapo ni porojo tu!!
 
Haya maamuzi magumu kwa nini serikali nzima isisitishe wakuu kutumia First Class? What for? Huu ni upuuzi sana!
 
Na wabunge wa kila mkoa watumie Toyota Hiace moja kwenda Bungeni badala ya kila mbunge kutumia VX.
 
Dar-kia tu safari ya dk 50 watu wa serikalini wanapanda 1st class chezea pesa za msaada ww
 
Anacho kifanya Mwakyembe ni upuuzi. Hilo swala liko kwenye Standing order. Kila mtumishi katika level fulani anaruhusiwa kisheria kusafiri kwa daraja fulani. Yeye mbona hasafiri kwa basi?
 
Kilicho mkuta kyela huyo siri yake mwenyewe mwache apatwe na hasila za namna hiyo kwao hakubaliki hata kidogo wamebwagwa balaa na CDM halimashauri ya mji mdogo kyela imechukuliwa na wapinzani sasa mwache ajisafishe kwa hilo hongera mwakyembe
 
Madaraja ya usafiri yako kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma. Wapo watumishi kwa mujibu wa nyadhifa zao wanastahili kusafiri kwa daraja la I,II na III. Kuwazuia watumishi wa wizara yake pekee huku watumishi wa taasisi nyingine za serikali wakiendelea kuponda raha,kwa maoni yangu nadhani wahusika hawajatendewa haki. Pengine ingekuwa vema kama mh. Mwakyembe angewasilisha mapendekezo ya marekebisho ya kanuni kwenye mamlaka husika ili kuzuia watendaji wote wa umma wakiwemo mawaziri kusafiri kwa daraja la kwanza. Kwa kufanya hivyo naamini tungeokoa fedha nyingi zaidi. Naunga mkono hoja yake lakini isiishie wizarani kwake tu.

Is true, but ukitaka kumove agenda anza kutekeleza mwenyewe kwanza. Labda ndicho anafanya coz hana mamlaka na wizara nyingine.
Tafuta upenyo umshauri ashikilie hapohapo ktk wizara yake then apeleke hoja ktk baraza la mawaziri huku akiendelea kutekeleza kwenye wizara yake, hoja itakuwa na nguvu pia akionesha significant saving + maeneo mengine...
 
Na yeye Mwakiembe aache kununua viwanja vya bilioni moja
ili aache kukomba pesa za ufisadi bandarini.
 
Swala la masilahi ya watumishi wa umma liko chini ya wazara y utumishi. Hivyo Mwakyembe hata kama anataka walioko chini ya wizara yake wasisafiri kwa daraja la kwanza, hana nguvu ya kisheria hadi waraka utoke utumishi. Kwa hiyo huko ni kukurupuka na kuonyesha namna gani elimu yake ya sheria haijamsaidia. Na hii tabia ndio inaifanya tanzania kuwa ya ovyo ovyo. Maana kila waziri anaedesha wizara kwa anavyofikiria yeye sio kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
 
Back
Top Bottom