Mwakyembe azitaka ofisi za Umma kutoa taarifa kwa wanahabari

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1590076095809.png

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imezitaka ofisi za Umma kutoa taarifa kwa wanahabari kwa kuwa siyo hisani na siyo hiyari, bali ni takwa la kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18 (d). Kauli hiyo imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya tasnia ya Habari Dkt. Harrison Mwakyembe alipokutana na ujumbe wa viongzi wa Chama cha Waandishi wa Habari kutoka mkoani Arusha pamoja na Asasi ya Vyombo vya Habari Mbadala (Alternative Media) leo jijini Dodoma.

“Serikali haina ugomvi na vyombo vya habari, bila vyombo vya habari hatutaweza kuwahabarisha wananachi masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu” amesema
Dkt. Mwakyembe. Aidha, amewakumbusha wanahabari kuwa kazi wanayofanya ni muhimu sana ambapo nchi zilizoendelea bado wanatumia vyombo vyao vya habari ikiwemo Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ambalo lina miaka zaidi ya 90 na linatangaza habari zake kwa lugha zaidi ya 40 ili kuwafikia wananchi wake na dunia kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari kutoka mkoa wa Arusha Bw. Claud Gwandu amemshukuru Waziri Dkt. Mwakyembe kwa mapokezi, majadiliano yenye tija kwa uwazi na ukweli na kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya katika sekta anazozisimamia.

“Tunamshukuru Waziri kwa kutupa nafasi ili tuweze kushirikiana katika kuimarisha tasnia ya habari iwe bora kwa mustakabali wanchi yetu” amesema Gwandu.
 
Back
Top Bottom