Mwakyembe: ATCL Kununua Ndege Mbili Mpya!

K-Boko

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
697
218
Dk. Harrison Mwakyembe ameliambia Bunge punde tu kuwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) litanunua ndege mbili mpya katika mwaka ujao wa fedha.

Katika maelezo yake hajaweka wazi hadi sasa ATCL ina ndege ngapi zinazomilikiwa kwa asilimia 100 na shirika hilo mbali na kuzungumzia ndege kadhaa za kukodi.

Najua JF ina wajuvi wengi, mwenye taarifa hizi atiririke hapa tujue!
 
Amesema pia TPA itanunua Meli za abiria na mizigo, ni story tu anasimulia, sina hakika kama sheria iliyoanzisha Mamlaka hii imeshabadilishwa.
 
Hiviii kwa utawala UPI? Kama ni huu wa huyu Mzee wa chalinze basi tegemea IPTL ya pili
 
Dk. Harrison Mwakyembe ameliambia Bunge punde tu kuwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) litanunua ndege mbili mpya katika mwaka ujao wa fedha. Katika maelezo yake hajaweka wazi hadi sasa ATCL ina ndege ngapi zinazomilikiwa kwa asilimia 100 na shirika hilo mbali na kuzungumzia ndege kadhaa za kukodi. Najua JF ina wajuvi wengi, mwenye taarifa hizi atiririke hapa tujue!
Blah blah hizi tumezizoea
 
Sijui kama wabunge wamepitisha pesa kiasi cha kutosha kununulia ndege hizo mbili - au ndio kawaida ya kuahidiahidi tu!
 
Vipi hajazungumzia wizi unaoendelea bandarini?

Alitudanganya kuwa amekomesha wizi wa mizigo,na kukwapua vitu kwenye magari ya wateja.

Lakini hivi karibuni jamaa zangu watatu wote waliopitisha magari yao bandari ya Dar es Salaam ,wamekuta sreen imenyofolewa,mmoja wamekomba jeki,mwingine wameina spare tyre na kumuwekea ambayo imesha kwisha.

Tanzania tumeoza kila kona,acha kagame atudharau.
 
Halafu wizara yake itaishia kupewa 25% ya budgeted amount for 2014/2015 fiscal year ataishia kuuchuna kimyaaa, akiulizwa mwakani ndege mbili ulizoahidi ziko wapi? Ndio ataanza blah blah zao ooh!!! Wizara ilipewa 25% ya pesa ilizoomba hivyo tukashindwa kununua ndege kama tulivyoahidi kwenye kikao cha bajeti kilichopita.
 
Back
Top Bottom