Mwakyembe atajiuzulu hivi karibuni?

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
1,697
Wanyakyusa ni watu wanaojiamini sana na ni miongoni mwa watu wajasiri. Leo katika press conference yake ukimsikiliza kwa makini maelezo yake utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kuna kauri ambayo aliiongea kwamba " yeye ndiye waziri mwenye dhamana na wasanii na kama kuna jambo lolote linahusu wasanii ni vema akapewa kwanza yeye taarifa, anashangaa yeye kupata habari za wadau wake kwenye mitandao ya kijamii, " kwa kuwa suala lipo kwenye upelelezi tuache tusije kuharibu uchunguzi"

Ukifuatilia kwa makini utaona mh. Mwakyembe kutokuwa na taarifa juu ya kilichowapata wadau wake. lakini pili kutokuwa na uhakika kama ni kweli waliofanya tukio hilo ni askali au la, kama ni wao kwa nini asipewe taarifa juu ya wasanii wake.

Wanyakyusa ni wajasiri sana nakumbuka mwaka ule ambapo mwandosa akiwa naibu waziri wa maji na mifugo na JK akiwa waziri waliingia mgogoro lakini mwandosya bila kuogopa alimjibu waziri wake JK kwamba yeye anaweza kuwa waziri muda na saa yoyote, lakini yeye JK hawezi kuwa profesa milele. Hiyo ni kauli ya kijasiri inayoweza kutoka kwa jasiri tu , si mtu mwoga mwoga.

Baada ya upelelezi kukamilika nini kitafuatia, stay tuned
 
Vipi hajaunda tume?? Na lowasa na kundi lake washitakiwe kwa kumtegeshea mwakyembe sumu kwa kumtumia yule Dada ambaye baada ya muda alikutwa amekufa..alikuwa PS wa mwaky
 
Sidhani kama hatajiuzulu huyu wazir wetu wa visingeli chezea madaraka wewe! Nani asiyependa kuitwa Mh Waziri
 
Kama angekuwa shujaaa angejiudhuru,alipopata demotion, kutoka waziri mwenye dhamana na sheria na kuletwa kwenye usanii sanii kama ulikuwa hujui kwa msomi kama Mwakyembe ni demotion hiyo,ila njaa na unafiki vinasababisha wasomi wetu waendeshwe na bado ataendeshwa sana
 
Kujiudhuru! Sio Mwakyembe huyu ninayemfahamu. Hata Magufuli alikuwa anangoja Mwakyembe asitokee kwenye uapisha. Na alisema angeshangaa sana kama Mwakyembe asingetokea (kwa vile anamjua ni mtu mpenda madaraka na haswa kuonekana onekana kwenye media.)
 
Wanyakyusa ni watu wanaojiamini sana na ni miongoni mwa watu wajasiri. Leo katika press conference yake ukimsikiliza kwa makini maelezo yake utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kuna kauri ambayo aliiongea kwamba " yeye ndiye waziri mwenye dhamana na wasanii na kama kuna jambo lolote linahusu wasanii ni vema akapewa kwanza yeye taarifa, anashangaa yeye kupata habari za wadau wake kwenye mitandao ya kijamii, " kwa kuwa suala lipo kwenye upelelezi tuache tusije kuharibu uchunguzi"

Ukifuatilia kwa makini utaona mh. Mwakyembe kutokuwa na taarifa juu ya kilichowapata wadau wake. lakini pili kutokuwa na uhakika kama ni kweli waliofanya tukio hilo ni askali au la, kama ni wao kwa nini asipewe taarifa juu ya wasanii wake.
wanyakyusa ni wajasiri sana nakumbuka mwaka ule ambapo mwandosa akiwa naibu waziri wa maji na mifugo na JK akiwa waziri waliingia mgogoro lakini mwandosya bila kuogopa alimjibu waziri wake JK kwamba yeye anaweza kuwa waziri muda na saa yoyote, lakini yeye JK hawezi kuwa profesa milele. Hiyo ni kauli ya kijasiri inayoweza kutoka kwa jasiri tu , si mtu mwoga mwoga.

Baada ya upelelezi kukamilika nini kitafuatia, stay tuned

Na wewe umeamini?

aisee wewe utakuwa ni bomu la karne
 
Ajiuzulu. Hahahaaa. We umesahau walimuwekea sumu akanyonyoka nyele na kuwa zeruzeru na bado ameng'ang'ana. Kifo tu ndio kitakachomtenganisha na siasa. Kwa ulafi wa madaraka alokuwa nao hamna namna ya kujitoa mwenyewe
 
Kama kakutuma uandike hayo mwambie aanze upya. Njaa ilimlevya na sasa ni laana za raia wasio na hatia ndio zimeamza kumtafuna kwa unafiki wake. Kuna wanyakyusa wa kutolea mfano lakini sio yeye yeye kwa sasa amebaki kuwa "mnyambolea".
Kama ulivyoweza kutolea mfano wa Prof. Mwandosya. Muulize kwanini na yeye alipotoka India hakuweza kutuambia watanzania ni nini kilimsibu mpaka akalazwa India badala ya Tanzania au aliumwa nini?
 
Mwakyembe ni muhanga wa mateso waliyopata kina Roma kutoka kikosi cha siri walimpa sumu akanyonyoka kama kanga..ashukuru maombi ya Gwajima yalirudisha muonekano wake alikuwa anavaa pama na soksi za mikono kama kaka jambazi
 
Back
Top Bottom