Mwakyembe apelekwa nje kwa matibabu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,641
155,003
Mwakyembe amepelekwa India leo mchana kwa ndege ya Qatar Airways kwa ajili ya matibabu ya kina akisindikizwa na Nelson Mwambalaswa mbunge wa Lupa, Chunya ambaye pia ni msemaji wa familia.
ITV hawajaonyesha picha zake kwa kuwa KAVIMBA VIBAYA.
Source ITV habari.
 
Afadhali maana sasa tutajua kwa uhakika chanzi cha madhila yake lakini pia wale wenye nia mbaya sasa wameumbuka!
 
Kwanini usingesubiri saa2 ikifika utoe habari kamili?
Ok! Tunakusubiria kwa hamu sana ndg.
 
Amesafiri leo hii. Uwanjani alikuja na nape nauye. Ndugu zake kadhaa walikuwepo kumuaga, mengi pia alikuja kumuaga.
Awali waandishi wa habari walielezwa kua mgonjwa ameomba asiongee nao wala asipigwe picha. Polisi walijaribu kuwasihi waandishi waondoke maeneo ya vip lakini hawakutoka. Sijui kama walipiga picha au la.
Mimi nilikuwepo eapoti mida hiyo.
 
kila la kheli nahisi atutakuwa na wewe muda si mrefu kwa ulianza kutofutiana na wenzako.
mungu akubariki amina..
 
Good of him, ndugu yangu bujibuji angeugua si ndo angejifia zake Mwananyamala!!!

acha utani bana......
Mabango ya waganga wa jadi yamejaa tele mitaani, wala hawataki rushwa kama manesi na madaktari wa Mwananyamala.
Ningeenda kwa mganga na kama kufa ningefia huko, ila ningemwambia atengeneze zigo la kuwamaliza wale wote walionifanyia ubaya
 
Mungu awe pamoja naye huyu ndg yetu, apone haraka aje ahudumie taifa. Bado tunamuhitaji ....japo wagamba wanajitahidi kumuingiza kwenye system ya kifisadi.
 
...Awali waandishi wa habari walielezwa kua mgonjwa ameomba asiongee nao wala asipigwe picha. Polisi walijaribu kuwasihi waandishi waondoke maeneo ya vip lakini hawakutoka. Sijui kama walipiga picha au la.
Kama wamekataa basi waandishi wa habari wameanza kuelewa somo, na wapongezwe. Tuliwa lambast wakati lilipokuja jitu moja hapa linaji identify kama owner la Dowans likadai eti lisipigwe picha na waandishi wetu maskini waka comply.

Waziri anaenda kutibiwa nje kwa pesa yangu na yako, nataka taarifa na evidence za miendo yake yote anayoifanya kwa pesa yangu. Hutaki picha nenda jigharimie privately au jitoe kwenye uongozi.
 
Ina maana Tanzania hatuna madaktari wa kuutambua ugonjwa wake?
 
Ile delegation ni kubwa sana, Mawaziri wa2, familia pamoja na viongozi wengine. Sikuona sababu ya kina Magifuli kwenda. Ingekuwa nimepanga list ya wasindikizaji basi ningepeleka wafuatao

1. Mke wakr
2. Personal Assistant
3. Ndugu 1 wa kiume
4. Ndugu 1 wa kike

PERIOD
 
Mwakyembe-Mwamba.jpg

Dr. Mwakiembe akiwa na mbunge Victor Mwambalaswa Bungeni Dodoma siku za karibuni

3.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Naibu Waziri wa Ujenzi Dkt.Harrison Mwakyembe
wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam jana(Jumamosi) mchana

Too much illusion. Kwa umbile la Dr. Mwakiembe na anavyoonekana pichani ni tofauiti kabisa na maneno yaliyokuwa yakisemwa hapa janvini. Siyo kiasi cha kivimba mwili kama walivyosema wengine, tuongee kitu baada ya kujiridhisha kupata uhakika kutoka source za kuaminika badala ya habari za kusimuliwa au kufikirika.

Picha mbili za juu zinaonyesha Dr. Mwakiembe alivyokuwa anaonekana siku za karibuni alipokuwa bungeni na picha ya pili alipotembelewa na Rais Kikwete Juzi nyumbani kwake. Je, mbona sioni tofauti ya pekee kama ilivyoongelwa hapa katika picha hizo mbili? Mimi sina hulka ya kuongelea mambo ya kufikirika ila niko makini kuongelea kitu chenye source ya uhakika.
 
Hivi Presidaa hayuko busy kabisa!!!! Si mbaya kwenda kumjulia hali Waziri wake ila excuse ya yeye kutokwenda kwa wingi wa shughuli za Uraisi tungemuelewa tu!!!!
 
Back
Top Bottom