Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, kwa sasa Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe anajibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wabunge wakati wa mjadala wa wizara hiyo. Miongoni mwa hoja ni zile zilizotolewa na taarifa ya Kambi ya Upinzani iliyowasilishwa na Waziri Kivuli wa Wizara hiyo, Moses Machali. Miongoni mwa hoja za Machali ni juu ya UDA, DART, Ubungo Bus Terminal na Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba maeneo ambayo Mwakyembe amesema kuwa yana Wizara zake ( Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Elimu). Amemshangaa sana Machali kwa kuibua hoja ambazo hazipo kwenye wizara yake. Amesema kuwa Machali ameonesha umbumbumbu mkubwa sana. Hata hivyo amesema kuwa huenda hali hiyo imetokana na ugeni wake kwenye kazi ya Uwaziri Kivuli. Amemshauri Machali kujifunza kutoka kwake na wakati wote yupo tayari kumfundisha utendaji wa Wizara hiyo
Hawa ni aina ya Mawaziri Kivuli ambao Freeman Mbowe aliwatangaza kwa Mbwembwe
Hawa ni aina ya Mawaziri Kivuli ambao Freeman Mbowe aliwatangaza kwa Mbwembwe