Mwakyembe amteua Albert Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya hakimiliki

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,409
20,753


Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amemchagua Mwanasheria na mdau wa masuala ya Sanaa Albert Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.

Katika tarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara Bi Leah Kihimbi kuhusu uteuzi huo wa Msando imesema kwamba uteuzi huo umetokana na vikao vilivyofanywa na wadau wa sanaa pamoja Mh. Waziri Mwakyembe.

Kwa upande wa Albert Msando ambaye amepatiwa nafasi hiyo na serikali ameahidi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria za nchi zinalinda haki za wasanii na kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao.

Msando ameandika "Ulaya na Marekani wasanii wengi sio masikini. Hapa kwetu wasanii wengi ni majina tu. Wengi wanaishi maisha ya 'naomba nitoe niko vibaya'. ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria zetu zinalinda haki za wasanii".

Ameongeza "Harrison Mwakyembe tutafanya kazi uliyotutuma"

Msando mara nyingi amekuwa mbele katika kuwasaidia wasanii kwenye masuala yanayohitaji msaada wa kisheria.


2.jpg




Muungwana
 
Hongera kwake
Haya Chadema vipeeee hakuna w kubutwa kutoka huko?
Mnimesahau mlisomea chuo chenu na ulafi, kupenda pesa za kuhongwa na hata wazungu, uongo, udaku n.k

Ha ha haaaaa
Kama nawaona mnazidi kusaga meno leo
Eeeeeeh
 
Duh! Jamaa anazidi kuula tu. Nimeamini ukimtanguliza Mungu na kuwa na bidii mambo yanakunyookea mpaka we ukaanza kujishangaa tu.
 
Hyo kamati si itakua inaukomo.. Ama ni ya milele kusimamia umiliki...
 
Duh! Jamaa anazidi kuula tu. Nimeamini ukimtanguliza Mungu na kuwa na bidii mambo yanakunyookea mpaka we ukaanza kujishangaa tu.
Jidanganye na mungu wako!! Ccm hawajui huyo mungu,kama unataka cheo pale basi mtumikie Dinosaur kwa nguvu zote na kwa akili zote! Majambazi kibao yameula huku kwetu kwa kuutumia ujambazi wao kuitumikia ccm!! Uki--- mpinzani cheo kinakufuata chenyewe
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom