Mwakyembe amtaja waziwazi Rostam Aziz!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Suala la Dowans lilijitokeza juzi jumatatu wakati kamati ya wabunge wa CCM iliyoketi Dar es Salaam, nimefurahishwa na hii nukuu jinsi alivyozungumza Mwakyembe: "Mnahangaika nini? Aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja tu: anaitwa Rostam Aziz. Serikali ifanye kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizi hazilipwi"

Source: Mwana Halisi Janaury 26-Feb 1, 2011 Ukurasa wa pili paragrafu ya 22
 
In other news...TANESCO washatukatia umeme

hivi lile dili la MWAKYEMBE na WAKOREA kutuletea umeme wa upepo limeishia wapi?
 
Hawa ndo baadhi ya watu tunaowaitaji kwenye mwenge wa Mara,,big up Mwakyembe..
 
hana lolote Mwakyembe...mi sijamuona kama kuna la maana analoongea kama anakerwa na haya why sasa anaendelea kuwa miongoni mwao huko CCM...
 
CCM wakubali mfumo huo wa umeme halafu wakale wapi hawa wazee wa midili bila kuzima zima umeme na kusingizia ukame???
 
hana lolote Mwakyembe...mi sijamuona kama kuna la maana analoongea kama anakerwa na haya why sasa anaendelea kuwa miongoni mwao huko CCM...

Hapo Kalamu umesema kweli kabisa.
Mwakyembe alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa Richmond, angetuletea hilo alilosema sasa moja kwa moja badala ya kuzunguka mbuyu tusingekuwa tumefika hapa. Wao wenyewe walisema kuna vitu wameficha ili kuisaidia serikali sasa Rostam ni serikali?
 
:A S kiss::A S-fire1:Safi sana mwakyembe kwa ujasiri wako! Hapo unawasaidia Wadanganyika walio wengi! Bravo ka' Mwakyembe!!!!!!!!!!!!:shock::A S kiss:
 
CCM wanamwogopa sana Rostam na wananchi hatumwogopi raia yeyote yule...Tunauhakika Rostam atkwenda jela tu na JK hawezi kumficha kila leo.
 
:A S kiss::A S-fire1:Safi sana mwakyembe kwa ujasiri wako! Hapo unawasaidia Wadanganyika walio wengi! Bravo ka' Mwakyembe!!!!!!!!!!!!:shock::A S kiss:

Ujasiri ni kuongelea kwenye Kamati Kuu ya CCM? Hiyo taarifa anayo toka alipoketi kama Mwenyekiti wa Kamati ile! Alikuwa anaijua kabla ya hukumu kutolewa! Akapewa na uwaziri kama zawadi! Akaukubali na anaendelea nao! Sasa hivi Rostam akijiuzulu uchaguzi katika jimbo lake utarudiwa fedha ya kodi itatumika bado ametusaidia? Mbona hakusema kabla ya uchaguzi wananchi wajue? Au anasaidia chama kwanza then watanganyika?

Na Mwakyembe anajua, Raisi hajui? Siku zote hajamwambia? Kama amemwambia na Raisi amekaa kimya ametusaidiaje? Kama hajamwambia kwa nini?

Lazima tujiulize sana katika hili jambo na kupata majibu sahihi! Tukikurupuka tutabaki washabiki kama ilivyokuwa kipindi cha kujiuzulu kwa EL!
 
Suala la Dowans lilijitokeza juzi jumatatu wakati kamati ya wabunge wa CCM iliyoketi Dar es Salaam, nimefurahishwa na hii nukuu jinsi alivyozungumza Mwakyembe: "Mnahangaika nini? Aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja tu: anaitwa Rostam Aziz. Serikali ifanye kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizi hazilipwi"

Source: Mwana Halisi Janaury 26-Feb1 2011 Ukurasa wa pili paragrafu ya 22

lolz......nimemcheki live muda kidogo Dr akinunua gazeti hilo street za imalaseko....
 
Tusikomee kuongea peke yake tuchukue hatua. Inabidi yaandaliwe maandamano ya kumtaka Rais awawajibishe wale wote waliohusika kwenye sakata la Dowans/Richmond akishindwa aachie ngazi
 
Kuna mzungu aliiweka serikali ya Mwalimu J K Nyerere mfukoni habari zake mlizisikia. Je RA amechukua nafasi yake baada ya mtetezi kuondoka? Kwanini hakuna wa kumkemea. Turudi Tunisia basi kama kuna ushirikiano na walioko juu
 
Back
Top Bottom