MWAKYEMBE AMPONZA SITTA - Ahojiwa Polisi kuhusu tuhuma za sumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MWAKYEMBE AMPONZA SITTA - Ahojiwa Polisi kuhusu tuhuma za sumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 22, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Habari kuu, Mtanzania

  *Ahojiwa Polisi kuhusu tuhuma za sumu

  Na Mwandishi Wetu

  JESHI la Polisi nchini limemhoji Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kuhusiana na tuhuma alizotoa akidai mafisadi wamempa sumu Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye yupo nchini India kwa matibabu.

  Chanzo cha habari cha kuaminika ndani ya jeshi hilo kimesema, baada ya Sitta kuhojiwa na kutakiwa kuwasilisha ushahidi wa tuhumu alizotoa, alipeleka ushahidi ambao uliwashangaza wengi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

  "Mzee baada ya kutoa zile tuhuma, tuliona si jambo dogo, linaweza hata kuhatarisha amani ya nchi hivyo tukaona ni busara tumhoji, atupatie ushahidi wake, ili sisi kama wanausalama tuufanyie kazi.
  "Lakini kilichotuchekesha na kutushangaza, akatuletea ushahidi kutoka kwenye mitandao ya jamii, akijua kabisa ule si ushahidi mbele sheria pamoja na kuwa yeye ni mwanasheria."Katika mambo yanayoandikwa kwenye mitandao ya jamii, kuna mengi ya kweli na uongo, ndio sababu hata wachangiaji wengi hawaweki majina wala anwani zao hali, sasa ni vipi mtu anazungumza mambo mazito kwa ushahidi wa aina hiyo?" kilihoji chanzo chetu.Katika ushahidi huo wa Sitta (nakala tunayo) pia yeye binafsi anatajwa kuwa mmoja wa walengwa katika mkakati wa kuua watu kadhaa.

  Wengine waliotajwa ni Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanahalisi, Saed Kubenea.
  Sitta, ambaye ni rafiki mkubwa na mshirika wa karibu wa Dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini, alisema wasiwasi huo unatokana na mabadiliko ya ngozi na nywele aliyoondoka nayo nchini kwenda India, ambayo ni mara ya kwanza kuishuhudia katika kipindi chote cha maisha yake.Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha ITV katika kipindi chake cha Dakika 45, kilichorushwa hivi karibuni."Ijumaa iliyopita nilikwenda kumuona nyumbani kwake, Kunduchi Mtongani.

  Nilishtuka sana. Kwa sababu umri wangu sasa wa zaidi ya miaka 65, sijaona mtu anajishika halafu inatoka vumbi, inadondoka chini kutoka kwenye ngozi," alisema Sitta.
  Aliongeza: "Kuna kitu kama mba kwenye nywele na kwenye ngozi ya Dk. Mwakyembe. Akishika hivi, baadhi ya nywele zinadondoka. Mkono umevimba, sehemu mbalimbali. Mke wake alichukua video. Alikuwa anatuonyesha kwenye laptop (kompyuta ndogo). Kwa kweli inatisha."Alisema inatisha zaidi hasa baada ya madaktari bingwa nchini kushindwa kugundua kitu kilichomsababishia Dk. Mwakyembe kupatwa na hali hiyo, hadi anaondoka kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.

  Hata hivyo, alisema anamshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuamua Dk. Mwakyembe apelekwe India kwa madaktari bingwa, ambako itajulikana nini kilichomsababishia hali hiyo.
  "Lakini kilichokuwa kinaonekana dhahiri pale ni uwezekano wa kitu cha hovyo kuwa kimefanywa cha aina labda ya sumu," alisema Sitta.Hata hivyo, alisema anamuachia Mungu kwani kila mtu ana siku yake ya kuondoka duniani.

  Akijibu swali namna anavyoliona suala la kuugua huko kwa Dk. Mwakyembe, Waziri Sitta alisema ni kama limechukua sura ya kuwekeana sumu na vitisho.

  Hata hivyo, alisema suala hilo linabaki kuwa ni sehemu ya mapambano na kukumbusha kila mwanadamu amezaliwa siku moja, hivyo kufa ni lazima.
  "Kwa hiyo, sijui mambo haya yamefanywaje. Mimi napata vitisho kwenye simu. Utaona namba zangu za simu nabadili mara kwa mara kwa sababu natishiwa sana.

  Na vita bayana ipo kwenye magazeti yao," alisema Waziri Sitta.
  Kabla ya Dk. Mwakyembe kwenda India kutibiwa, kulikuwa na habari kwenye magazeti kuwa alikuwa amelishwa sumu, ingawa yeye binafsi hajakanusha waka kuthibitisha habari hizo.
   
 2. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Lisemwalo lipo! Na kama halipo basi linakuja! Get well soon Dr. Mwakembe we all pray for you.:pray2:
   
 3. eddo

  eddo JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 16, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  duh hii ni hatari
   
 4. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Hatari sana !
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kiukweli kwa kauli za sitta, inaonekana amechoka na yanayoendelea. Wabaya wake wanamwinda usiku na mchana na hawana sababu ya kumkosa.

  Tatizo la kutokuamini habari za mtandaoni litatumaliza. Kama hawaamini, mbona wamekubali tishio la kikosi 2858? Ni wehu hawa watu. Lisemwalo lipo. Sitta mwenyewe shahidi wa hayo.

  Wakati akiwa spika aliwahi kukataa taarifa ya kifisadi ya richmond kisa iko mtandaoni. Mwisho wa siku alikubali. Ccm waache umafya wa wazi. Na hao wanaoficha id zao ni kwa usalama wao. Mbona UWT wanaficha id zao?
   
 6. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  police mbona haijatoa tamko au wanasubiri afe alafu waseme alikuwa na ngoma kama walivyosema kwa Dr. Balali wa BoT
   
 7. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  jamaa aliwapelekea live ripoti ya jason ilyowekwa humu jf nadhani walishangaa kuona na mkuu yumo, unadhani wangesema ni habari ya kweli?
   
 8. Meshe

  Meshe Senior Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Tusubiri yatafunguka
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Source;Mtanzania ! Linamilikiwa na nani ? Rostam Azizz.
   
 10. D

  Deo JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kawapa chenga ya mwili TISS

  Ukweli na imamani ya 6 kawekewa sumu au kalogwa na TISS
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na wewe tuondolee nukuu zako za magazeti uchwara ambayo kila kukicha kazi ni kufanya distortion ya habari. Huna kazi ya kufanya zaidi ya hii reproduction yako?
   
 12. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hata ile ya barua ya Dr Mwakyembe kwa polisi kuhusu njama za kumuua, ilianza kutoka Mtanzania, kunani!!!!
   
 13. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Duh, hii nchi kaaz kwel!
   
 14. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ukweli ndio huo!!!
   
 15. S

  Shembago JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Days are numbered who ever is behind this scandal,The destiny will prevail!
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Ya EPA na mengine mengi tu mbona yalikuwa ya kweli?

  Kwamba ni mitandaoni si lazima yawe uongo,hata wao wamekiri hivyo,kuwa yanaweza kuwa ya ukweli ama pia yanaweza kuwa ya uongo.

  Na kwahiyo wao walichotakiwa ni kuzifanyia kazi tuhuma hizo ili kuweza kujuwa kama ni za kweli ama za uongo na si kuja na kudai eti yanaweza kuwa ya kweli ama ya uongo kwasababu ya mtandao...What a hopeless statement kutoka kwa vichwa nazi!

  Uchunguzi ndio utabainisha,polisi nao siku hizi siasa kwa sana!

  Hawajui kazi yao kubwa ni kulinda raia na mali zao na wanalipwa kwa hilo!?
   
 17. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  nchi hiii kwa kupindisha mambo?? wao polisi kama wanachunguza wanchunguze na waombe riport ya daktari ili awambie kama ni sumu au si sumu....mbona kila kitu kiko wazi juu ya mwakyembe..kapigwa sumu full stop...waache ubabaishaji wa kazi...
   
 18. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  alichoongea sitta ni ukweli mtupu wasijidai kumuhoji kiunafiki ili kupotosha ukweli
   
 19. M

  Malova JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  polisi wanachokiongea hawakielewi sawasawa. mtandao siku hivi unahabari nyingi za kuaaminika. mbona magazeti wanayaamini kwani wanakaa wangapi kuandika habari moja.
   
 20. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  movie inaanza sasa
   
Loading...