Mwakyembe alivyoshindwa vita ya dawa za kulevya

sajosojo

JF-Expert Member
Apr 14, 2010
1,018
630
Amesema alipata taarifa za kichunguzi kuhusu jinsi dawa za kulevya zinavyopitishwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na akaamua kutangaza vita akisaidiana na mtu ambaye hajamuweka wazi, lakini mwisho mtu huyo aliyekuwa akiongoza vita hiyo, aliishia kufungwa gerezani mpaka leo.
Mwakyembe amesema hata baada ya yeye kutumia nguvu zake kumtoa gerezani ameshindwa, jambo ambalo linaonesha kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya ni ngumu kuliko kawaida, huku akionesha matumaini kuwa katika awamu hii, serikali itashinda.
Dk. Mwakyembe amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam, alipokutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.
source
Mwakyembe alivyoshindwa vita ya dawa za kulevya | East Africa Television
 
Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe, amepongeza jitihada za Rais Magufuli za kupambana na dawa za kulevya huku akisimulia alivyoshindwa vitahiyo wakati alipokuwa Wazri wa Uchukuzi, hususan katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.

Waziri Dkt. Harison Mwakyembe (Wakati huo akiwa ni Waziri wa Uchukuzi) akionesha picha ya msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari, picha zilizotokana nacamera za usalama za uwanja wa ndege, zikionesha jinsi alivyopita na kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ni dawa za kulevya, Agost 2013, na kuchukua hatua yakuwafukuza watumishi wa uwanja huo wa ndege waliodaiwa kumsaidia.

Amesema alipata taarifa za kichunguzi kuhusu jinsi dawa za kulevya zinavyopitishwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na akaamua kutangaza vita akisaidiana na mtu ambaye hajamuweka wazi, lakini mwisho mtu huyo aliyekuwa akiongoza vita hiyo, aliishia kufungwa gerezani mpaka leo.

Mwakyembe amesema hata baada ya yeyekutumia nguvu zake kumtoa gerezani ameshindwa, jambo ambalo linaonesha kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya ni ngumu kuliko kawaida, huku akionesha matumaini kuwa katika awamu hii, serikali itashinda.

Dk. Mwakyembe amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam, alipokutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaadawa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.

Chanzo : EATV
 
Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe, amepongeza jitihada za Rais Magufuli za kupambana na dawa za kulevya huku akisimulia alivyoshindwa vita hiyo wakati alipokuwa Wazri wa Uchukuzi, hususan katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.

c746b225efc7664656e0a69ec37201fb.jpg

Waziri Dkt. Harison Mwakyembe (Wakati huo akiwa ni Waziri wa Uchukuzi) akionesha picha ya msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari, picha zilizotokana na camera za usalama za uwanja wa ndege, zikionesha jinsi alivyopita na kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ni dawa za kulevya, Agost 2013, na kuchukua hatua ya kuwafukuza watumishi wa uwanja huo wa ndege waliodaiwa kumsaidia.

Amesema alipata taarifa za kichunguzi kuhusu jinsi dawa za kulevya zinavyopitishwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na akaamua kutangaza vita akisaidiana na mtu ambaye hajamuweka wazi, lakini mwisho mtu huyo aliyekuwa akiongoza vita hiyo, aliishia kufungwa gerezani mpaka leo.

Mwakyembe amesema hata baada ya yeye kutumia nguvu zake kumtoa gerezani ameshindwa, jambo ambalo linaonesha kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya ni ngumu kuliko kawaida, huku akionesha matumaini kuwa katika awamu hii, serikali itashinda.

Dk. Mwakyembe amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam, alipokutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.
 
Hebu jaribu kusikiliza na kisicho ongelewa kama utamuelewa huyu muheshimiwa.

Na washawasha!
 
Ni nani huyu aliefungwa mpaka leo?
na hata alipojitahidi kumtoa kashindwa?
Na pia alipotumia nguvu zake kashindwa?
Na je, ni lini atatoka?
Au ni yule jamaa aliefungwa kwa kesi ya ajabu.?
 
Cha kusikitisha huyu masogange hayupo katika orodha ya makonda aliyoitaja kwenye vyombo vya habari majuzi
 
Kwanini hakujiuzulu? hajui cheo ni dhamana ukishindwa unaachia wanasiasa wa Tanzania wanaona kama ni Sehemu ya ajira
 
Boss wa masogange ni noma kama alimshikisha adabu mwakyembe pamoja na kuwa waziri wa sheria ameshindwa kumtoa mtu waliyokuwa naye kwenye mapambano shikamoo wauza ngada
 
Mwakyembe amesema hata baada ya yeye kutumia nguvu zake (Kama Waziri wa Sheria na Katiba, na Mwalimu NGULI wa Sheria Nchini) AMESHINDWA kumtoa gerezani..
Sasa ANAFANYA NINI Hapo Wizarani? Ndo maana Raisi anaLAUMU Serikali KUSHINDWA kesi nyingi Mahakamani!
 
Hua nashangaa sana pale shetani anapo tamka hadharani eti hatendi dhambi....
 
Back
Top Bottom