Mathayo Fungo
JF-Expert Member
- Nov 13, 2018
- 319
- 510
Mbunge wa Kyela na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) ameshiriki leo tarehe 22 Novemba, 2019 ameshiriki kwenye ufunguzi wa kampeni ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Kata ya Serengeti uliofanyika katika kitongoji cha Keifo.
Akifungua mkutano Mwenyekiti wa CCM Kata ya Serengeti, Willy Mwangomile amewashukuru wana-Serengeti kwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo. Aidha, Bw. Mwangomile amewahakikishia wananchi kwamba CCM imejipanga vizuri na uchaguzi wa Serikali za Mitaa licha ya vyama vingine kujitoa.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Serengeti Martin Mwainyekule amemshukuru Mbunge kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata ya Serengeti ikiwemo barabara, maji na afya. Diwani Martin ameelezea pia ya Kata katika barabara na usambazaji wa maji zaidi katika vitongoji na kumuomba Mbunge kusaidia katika utekelezaji wa masuala hayo.
Kwa upande wake Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kyela na Mjumbe wa Secretariat Wilaya Peter Tungulu amewapongeza wana-Serengeti kwa kujitokeza kwa wingi na kwa mapokezi mazuri waliyoyafanya. Bw. Peter ametumia wasaa huo kuishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi katika Kata ya Serengeti na kuwahakikishia wananchi kwamba CCM itasimamia utekelezaji wa miradi iliyobaki.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya Bi. Lydia Sanga amewashukuru wana-Serengeti kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano. Aidha Bi. Lydia amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi tarehe 24 Novemba, 2019 na kuwachagua viongozi wa CCM.
Akihutubia katika mkutano huo, Dkt. Mwakyembe amewataka wana-Serengeti kujitokeza kwa wingi tarehe 24 Novemba, 2019 na kuwachagua viongozi wa CCM. Dkt. Mwakyembe pia amewaambia wana-Serengeti Serikali itakamilisha kusambaza umeme katika maeneo machache yaliyobaki, kukamilisha ukarabati na ujenzi wa barabara kwa maeneo yenye changamoto, kuongeza mtandao wa usambazaji wa maji na kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake.
Akihitimisha hotuba yake Dkt. Mwakyembe amewaombea kura wagombea wote wa CCM wa Kata ya Serengeti.
Awali akitoa utangulizi, Katibu wa CCM Kata ya Serengeti ndugu Adam Katembo aliwahakikishia wana-Serengeti ushindi katika uchaguzi kwa kuwa wagombea wote waliochaguliwa wana uwezo wa kutosha.
Imetolewa na:
Amani Mwakipesile,
Katibu wa Mbunge,
Ofisi ya Mbunge Kyela.
22 Novemba, 2019