Mwakyembe acha siasa bandarini, unaua uchumi wetu

Tuache siasa, bandarini tunaua uchumi

Mwandishi wetu

WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe sasa ametangaza kupokea ripoti ya tume aliyoiunda kuchunguza tuhuma ambazo zimekuwa zikidaiwa kuwa chanzo cha kuzorota kwa huduma za bandari zetu na hasa Bandari ya Dar es Salaam.

Tuhuma za Dk. Mwakyembe wakati akiunda tume yake na hata sasa, zinaelekezwa tu kwa uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzani (TPA) na zaidi viongozi maalumu anaowalenga yeye tu na mfumo mzima katika sekta husika.

Kwa kuwa waziri hana taaluma katika maswala ya usafiri kwa njia ya majini bandari nikiwa kama mmoja wa wadau kwenye sekta hiyo naamini sasa atakuwa amepata ufahamu wa kuifahamu vema sekta nzima ikiwa ni pamoja na mfumo mzima wa kupokea, kuhifadhi na kusafirisha mizigo ipitayo kwenye bandari zetu zikiwamo zile za maziwa.

Kwa wadau waliobobea kwenye eneo hili na ambao biashara zao za kila siku hutegemea ufanisi endelevu wa kila mdau kwenye eneo hili wanategemea kuona ripoti yenye weledi na muonekano wa kitaaluma kuliko ya kutafuta makosa ndani ya mdau mmoja.

Kwa maelezo ya Dk. Mwakyembe na wanaoungana naye, kwa sasa inaonekana tuhuma zinaelekezwa TPA ili kuhalalisha mbele ya umma kwamba Bandari ya Dar es Salaam kuna uozo, wizi, rushwa na kila aina ya uovu unaofahamika duniani.

Baadhi ya wadau wanaona matamshi kama haya na ambayo hayajahusisha wadau wote kwa kina yanatoa taswira ambayo inaweza kuwapoteza wateja kabisa hata wateja wachache tulionao Tanzania.

Waziri anadiriki kusema eti amehakikishiwa na mawaziri wenzake wa uchukuzi wa nchi jirani kwamba nchi hizo zitaendelea kuzitumia bandari zetu hasa ya Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau na wafanyabiashara wanasema kwamba mawaziri siyo wanaofanya biashara ila kazi yao ni kuweka na kusimamia sera ya biashara husika.

Tunafahau na waziri lazima afahamu kwamba bandari haiwezi kufanya kazi zake bila kuhusisha kwa umakini sekta nyinginezo na mfanyabiashara mmoja anayemiliki meli kubwa duniani ameliambia gazeti hili wazi kwa kusema, "Bandari haiwezi kufanya kazi kivyakevyake kama kitu kilichojitenga bila vifaa, watu au taasisi na mitandao inayopaswa kufanya nayo kazi!"

Hali kadhalika bandari haiwezi kufanya kazi ikawa na ufanisi bila kuwa na viunganishi thabiti kwa maana ya barabara, reli na mabomba ya mafuta.

Pia bandari haiwezi kuwa na ufanisi wa kupokea mizigo mingi kwa wakati mmoja kama haina miondombinu ya kutosha na ya kisasa kama gati za kutosha na zenye kina kinachoweza kuegesha meli kubwakubwa ambazo zinaweza kutia nanga hapa kama zilivyo kwenye bandari zinazoshindana na Bandari ya Dar es Salaam.

Ikumbukwe baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 wa Kenya kugubikwa na vurugu, wafanyabiashara wa Uganda walipata shida kutokana na mizigo yao kukwama kwenye Bandari ya Mombasa kwa zaidi ya miezi mitatu mpaka hali ilipotengemaa.

Ni wakati huo ujumbe mzito ulikuja kutoka Uganda ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, kuja kuona uwezekano wa kutumia Bandari ya Dar es Salaam na kuahidi kwamba Uganda ingetumia kupitisha asilimia 30 ya mizigo yake hapa kama mbadala wa Bandari ya Mombasa.

TPA ilibidi iweke wakala kule Uganda kama njia ya kuwavutia Waganda lakini wafanyabiashara wamekuwa wanasita kutokana na ukweli kwamba miundombinu yetu bado ni hafifu.

Kukosekana kwa reli kumefanya Waganda waghairi kutokana na gharama kubwa kwa njia ya barabara wakilinganisha na umbali wa kutoka Mombasa mpaka Kampala.

Hoja hapa ni kwamba pamoja na kuhakikishiwa na Waziri wa Uchukuzi wa Uganda wa kutoa ahadi ya asilimia 30 ya mizigo ya Uganda kupitia hapa imekuwa ni kitendawili kutokana na changamoto za mapungufu katika mtandao wetu wa njia za usafirishaji mpaka mzigo ufike Uganda au utoke Uganda mpaka bandarini Dar es Salaam.

Kama wadau, tunaona changamoto za uendeshaji bandari ziangaliwe kitaaluma zaidi kuliko kuchukua mrengo wa kisiasa.

Inashangaza kuona inachukua zaidi ya miaka mitano kuamua namna ya kuongeza gati mbili kwa nia ya kuongeza ufanisi kwenye sekta nzima kwa njia ya bahari ambayo faida yake yake ni kuongeza pato la taifa kwa kuwa kila mdau kwenye biashara inayohusiana na Bandari ya Dar es Salaam atakuwa anachangia kwa kiasi kikubwa kwenye GDP!

Mombasa wanaongeza gati nne kwenye katika bandari yao na mkandarasi yuko kazini mwaka wa pili sasa.

Pia wanajenga bandari mpya ya Lamu ambayo pia mkandarasi yuko kazini; hapa tunalumbana wakati wenzetu wanashangilia kwa ujinga wetu.

Waziri anahusisha vipi TPA peke yake na wizi wa makontena?! Mizigo hutolewa bandarini kwa njia ya nyaraka ambazo zina mlolongo mrefu.

Je, kama nyaraka za mzigo husika zimeghushiwa wakati mzigo unapotolewa bandarini au toka kwenye eneo linalomilikiwa TICTS, bandari au mkaguzi mkuu wa bandari atajuaje?

Tumeona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna makontena yameshikwa huko Hongkong yakiwa na pembe za ndovu zikitokea Dar na Mombasa.

Je, hapa TPA inahusika vipi wakati anayetakiwa kufungua na kukagua makontena kabla hayajapelekwa kwenye meli kupakiwa ni ofisa forodha?

Ni vema wanasiasa wakajifunza kwanza jinsi bandari inavyofanya kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine ndani ya mfumo kabla ya kufanya maamuzi ambayo kwa kiasi kikubwa yatakuwa hayajengi zaidi ni kuuvuruga mfumo wote wa usafirishaji kwa njia ya majini na kuua uchumi wetu kwa maslahi ya kisiasa.

Source: www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=41830

Hili Gazeti huwa kwa kila siku linanichukulia Hela Yangu ila kwa hii story, Naona kuna Msukumo Wa kisirisiri wa kifisadi!! Mwandishi wamekununua kwa TZS Ngapi?
 
Tuache siasa, bandarini tunaua uchumi

Mwandishi wetu

WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe sasa ametangaza kupokea ripoti ya tume aliyoiunda kuchunguza tuhuma ambazo zimekuwa zikidaiwa kuwa chanzo cha kuzorota kwa huduma za bandari zetu na hasa Bandari ya Dar es Salaam.

Tuhuma za Dk. Mwakyembe wakati akiunda tume yake na hata sasa, zinaelekezwa tu kwa uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzani (TPA) na zaidi viongozi maalumu anaowalenga yeye tu na mfumo mzima katika sekta husika.

Kwa kuwa waziri hana taaluma katika maswala ya usafiri kwa njia ya majini bandari nikiwa kama mmoja wa wadau kwenye sekta hiyo naamini sasa atakuwa amepata ufahamu wa kuifahamu vema sekta nzima ikiwa ni pamoja na mfumo mzima wa kupokea, kuhifadhi na kusafirisha mizigo ipitayo kwenye bandari zetu zikiwamo zile za maziwa.

Kwa wadau waliobobea kwenye eneo hili na ambao biashara zao za kila siku hutegemea ufanisi endelevu wa kila mdau kwenye eneo hili wanategemea kuona ripoti yenye weledi na muonekano wa kitaaluma kuliko ya kutafuta makosa ndani ya mdau mmoja.

Kwa maelezo ya Dk. Mwakyembe na wanaoungana naye, kwa sasa inaonekana tuhuma zinaelekezwa TPA ili kuhalalisha mbele ya umma kwamba Bandari ya Dar es Salaam kuna uozo, wizi, rushwa na kila aina ya uovu unaofahamika duniani.

Baadhi ya wadau wanaona matamshi kama haya na ambayo hayajahusisha wadau wote kwa kina yanatoa taswira ambayo inaweza kuwapoteza wateja kabisa hata wateja wachache tulionao Tanzania.

Waziri anadiriki kusema eti amehakikishiwa na mawaziri wenzake wa uchukuzi wa nchi jirani kwamba nchi hizo zitaendelea kuzitumia bandari zetu hasa ya Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau na wafanyabiashara wanasema kwamba mawaziri siyo wanaofanya biashara ila kazi yao ni kuweka na kusimamia sera ya biashara husika.

Tunafahau na waziri lazima afahamu kwamba bandari haiwezi kufanya kazi zake bila kuhusisha kwa umakini sekta nyinginezo na mfanyabiashara mmoja anayemiliki meli kubwa duniani ameliambia gazeti hili wazi kwa kusema, “Bandari haiwezi kufanya kazi kivyakevyake kama kitu kilichojitenga bila vifaa, watu au taasisi na mitandao inayopaswa kufanya nayo kazi!”

Hali kadhalika bandari haiwezi kufanya kazi ikawa na ufanisi bila kuwa na viunganishi thabiti kwa maana ya barabara, reli na mabomba ya mafuta.

Pia bandari haiwezi kuwa na ufanisi wa kupokea mizigo mingi kwa wakati mmoja kama haina miondombinu ya kutosha na ya kisasa kama gati za kutosha na zenye kina kinachoweza kuegesha meli kubwakubwa ambazo zinaweza kutia nanga hapa kama zilivyo kwenye bandari zinazoshindana na Bandari ya Dar es Salaam.

Ikumbukwe baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 wa Kenya kugubikwa na vurugu, wafanyabiashara wa Uganda walipata shida kutokana na mizigo yao kukwama kwenye Bandari ya Mombasa kwa zaidi ya miezi mitatu mpaka hali ilipotengemaa.

Ni wakati huo ujumbe mzito ulikuja kutoka Uganda ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, kuja kuona uwezekano wa kutumia Bandari ya Dar es Salaam na kuahidi kwamba Uganda ingetumia kupitisha asilimia 30 ya mizigo yake hapa kama mbadala wa Bandari ya Mombasa.

TPA ilibidi iweke wakala kule Uganda kama njia ya kuwavutia Waganda lakini wafanyabiashara wamekuwa wanasita kutokana na ukweli kwamba miundombinu yetu bado ni hafifu.

Kukosekana kwa reli kumefanya Waganda waghairi kutokana na gharama kubwa kwa njia ya barabara wakilinganisha na umbali wa kutoka Mombasa mpaka Kampala.

Hoja hapa ni kwamba pamoja na kuhakikishiwa na Waziri wa Uchukuzi wa Uganda wa kutoa ahadi ya asilimia 30 ya mizigo ya Uganda kupitia hapa imekuwa ni kitendawili kutokana na changamoto za mapungufu katika mtandao wetu wa njia za usafirishaji mpaka mzigo ufike Uganda au utoke Uganda mpaka bandarini Dar es Salaam.

Kama wadau, tunaona changamoto za uendeshaji bandari ziangaliwe kitaaluma zaidi kuliko kuchukua mrengo wa kisiasa.

Inashangaza kuona inachukua zaidi ya miaka mitano kuamua namna ya kuongeza gati mbili kwa nia ya kuongeza ufanisi kwenye sekta nzima kwa njia ya bahari ambayo faida yake yake ni kuongeza pato la taifa kwa kuwa kila mdau kwenye biashara inayohusiana na Bandari ya Dar es Salaam atakuwa anachangia kwa kiasi kikubwa kwenye GDP!

Mombasa wanaongeza gati nne kwenye katika bandari yao na mkandarasi yuko kazini mwaka wa pili sasa.

Pia wanajenga bandari mpya ya Lamu ambayo pia mkandarasi yuko kazini; hapa tunalumbana wakati wenzetu wanashangilia kwa ujinga wetu.

Waziri anahusisha vipi TPA peke yake na wizi wa makontena?! Mizigo hutolewa bandarini kwa njia ya nyaraka ambazo zina mlolongo mrefu.

Je, kama nyaraka za mzigo husika zimeghushiwa wakati mzigo unapotolewa bandarini au toka kwenye eneo linalomilikiwa TICTS, bandari au mkaguzi mkuu wa bandari atajuaje?

Tumeona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna makontena yameshikwa huko Hongkong yakiwa na pembe za ndovu zikitokea Dar na Mombasa.

Je, hapa TPA inahusika vipi wakati anayetakiwa kufungua na kukagua makontena kabla hayajapelekwa kwenye meli kupakiwa ni ofisa forodha?

Ni vema wanasiasa wakajifunza kwanza jinsi bandari inavyofanya kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine ndani ya mfumo kabla ya kufanya maamuzi ambayo kwa kiasi kikubwa yatakuwa hayajengi zaidi ni kuuvuruga mfumo wote wa usafirishaji kwa njia ya majini na kuua uchumi wetu kwa maslahi ya kisiasa.

Source: www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=41830

Kwa hiyo unataka nini?wezi waachwe au?acha propaganda wakati mnaiba kila siku halafu wachapakazi wakija mnataka kuwapunguza nguvu, vita inaua hata ambao sio wanajeshi,
 
Acheni mwakyembe afanye kazi, mmeshaona anafichua uozo wenu mnahisi mtatimuliwa.Msilete blablaaa hapa.Chapeni kazi kuokoa uchumi wetu
 
Yaani hii nchi wezi ndio wanaotetewa na wazarendo ndio wanaopingwa,hivi konteina zaidi ya 15 kupotea pale bandarini,je hizo zimekuwa ni embe? Harafu mnamlaumu waziri,ili muweze kuendelea kuiba.
Waziri,komaa nao hadi kieleweke,hakuna kucheza nao
 
Inawezekana kabisa Mwakyembe anaua uchmui wao. Yaani uchumi wa wale watu ambao kazi yao ilikuwa ni kutuibia pale bandarini. Lazima uchumi wao utaanguka.
 
Mnataka hata wanao iba makontena ya vitenge tuwachekee tu wake zetu mnataka watembee uchi sio?
 
Huyu mzee anapenda sana cheap popularity ndo maana walimpiga ***** wa milele
 
kwa upande wangu watu wa bandarini siwachekei,maana tunajibana sana kuagiza vitu,wao hawahangaishi akili zao wanasubiri tulete mizigo yetu na kuibeba kiurahisi,hatuwezi kuwachekea ktk hili,mtu kakopa pesa kaleta kontena,na zinapotea kiurahisi kabisa,bado mnataka tuwachekee?
 
Huyu mzee anapenda sana cheap popularity ndo maana walimpiga ***** wa milele

Inawezekana kweli, lakini tusiongelee mambo jumla jumla.

Katika hili cheap popularity ipo wapi?

Kuona kwamba bandarini kuna tatizo, kuondoa viongozi walioshindwa kazi wapishe uchunguzi na kuanzisha mchakato wa uchunguzi ulioongozwa na watu wenye uzoefu na bandari, sheria na sekta ya uchukuzi kwa ujumla?

Cheap popularity iko wapi hapo? Labda unajua tusichojua.
 
Kama haina changamoto ni vyema kuikosoa mapungufu yake, ndio msingi wa mjadala. Mfano kusema kwamba Mwandishi amekosea kuingiza suala la ujio wa Waziri wa Uganda, miaka ya nyuma na baadae wafanyabiashara wa huko kushindwa kufuata maelekezo ya Waziri wao.
Mkuu Halisi,
Mh.Mwakyembe aliunda tume kuchunguza madhaifu aliyiyakuta na aliona haiwezi kuwa sehemu nyingine inasababisha mapungufu hayo kama wizi pasipo top leaders wa bandari kujua,sasa jana kakabidhiwa ripoti ta tume aliyoiunda na hatuja elezwa chochote kilichomo ktk ripoti hiyo,Mwandishi kuja na kuanza kusemea watu maana yake nini?Kuna jambo wao waliohusika wanalijua hivyo wameamua kulisema kwa namna ya kumtumia mwandishi wa habari kuwajengea hoja dhaifu.
What we need ni kusikia Mh.Mwakyembe amegundua nini toka kwenye uchunguzi ambao tume imeufanya na nani kafanya nini akiwa ofisini na nani hakuwajibika kama alivyostahili kufanya.mikakati mingine ya kuboresha bandari kimiundombinu na kiutendaji inakuja baada ya kujiridhisha kama team uliyonayo ni ya kukupeleka kwennye matamanio ya wengi au la.Lets the man afanye kazi yake.
 
Huyu mzee anapenda sana cheap popularity ndo maana walimpiga ***** wa milele

huo ndo ukweli.pamoja na lengo zuri alilonalo mwakyembe aache siasa na afanye kaz na tuione maana hapa badala ya kuhangaika kubadili system ya utendaji kaz pale bandalini anahangaika na watu.kwa hali ya sasa labda umlete malaika ndo ataweza kufanya kaz nzuri vinginevo hta aje nani naye atajoin atakaowakuta then life goes on.

pale bandarin kuna mamlaka zaidi ya moja na kila mamlaka inaurasmu wake wa kazi wakiwemo tra wakwamishaji wakuu wa uchumi wetu wenye urasmu wa hali ya juu ambao wakati mwingine haun tija.Mh anatakiwa aone umhimu wa kuunda mfumo mpya wa uendeshaji ambao utaweza kumtoa nje mtu yoyote mzembe mvivu na yoyote yule asiyefaa.

Mfano mdogo ni wa TICTs.mh anajua kabisa namna Ticts ilivo na mkataba wake na anajua kabisa container zinaibiwa Ticts lakn kwa sababu anayoijua yy anasem mAcontainer yameibiwa TPA.Hii sio sawa hata kidogo.tuko nyuma yako mh pambana na mkataba wa ticts kule ndo kuna hela na sio tpa.simanish tpa hawana kitu lkn ticts ndo hasa wanaleta matatizo haya.

Natambua mahusiano yako na wadau wakubwa wa ticts sio mazuri sana maana ww ndo mpambanaji wetu toka wakati wa richmond na wadau wakuu ndo wale wale wa ticts.sasa hapo siunaona kabisa namna kaz ilibokuwa kubwa kwako kwa mara ya pili tena.ulituahid utaeleza kila kitu wakat wa richmond mpaka sasa hujAELEZA na sasa umekutana nao tena kwa namna nyingine na uzur kwa sasa unamamlaka sio km wakat ule kwa hiyo mh fanya maamzi kila mtanzania mpenda maendeleo atakuunga mkono na siasa uziache vyeo tutakupa mbele ya safari huko baada ya safar ndefu ya mapambano hata urais tutakupa kama ukiishinda vita hii.

ukweli ni kwamba ww ni mchapakaz lkn huyu dg uliyempa akaimu udg tpa knows litle kuhusu bandar operation na ww ni shahidi wa hilo kwani yy ni mtaalam sana wa mambo ya mizani barabarani lkn ht hivyo anahitaji mgt skills imsaidie ili atimize malengo ya nchi.nimesikia kwamba siku moja alienda nje ya nchi kwenye forum ya kimataifa juu ya port operation hakuiwakilisha vizur kwan hakuwa na uelewa wa kutosha juu shughuli za bandari.anyway ataimprove as he continues bt plz supervise him otherwise atachemka.

nawasilisha
 
Inasikitisha sana Tanzania tunapopata waziri ambaye kidogo anaonyesha ahueni watu wanaanza majungu, sasa mlete maada anajitetea ama ndo ile tufe wote, mimi nadhani hizo sehemu zingine zinaweza fata baadae but waziri inaonekana amaeona TPA ndo hasa kwenye tatizo kubwa... sasa suala la aaah mara waziri hana utaalamu huo c ujinga aliyekwambia duniani mawziri wanatakiwa wawe na utaalamu nani? c hata mimi ningeenda kusomea uwaziri, haya basi ww ndo mwenye utaalamu tuambie amefanya kosa gani kuchunguza TPA? hapo lazima mng'oke wezi wakubwa nyie
 
My opinion! Mwakyembe yuko okay, hata homa unapoitibu dawa inakunyong?onyesha kwanza! He is in a wright truck!
 
Tina, what i can learn! You want to play politics on issues! Bandari ya dar inanuka! Mwakyembe go! Hebu rekebisha!
 
huo ndo ukweli.pamoja na lengo zuri alilonalo mwakyembe aache siasa na afanye kaz na tuione maana hapa badala ya kuhangaika kubadili system ya utendaji kaz pale bandalini anahangaika na watu.kwa hali ya sasa labda umlete malaika ndo ataweza kufanya kaz nzuri vinginevo hta aje nani naye atajoin atakaowakuta then life goes on.

pale bandarin kuna mamlaka zaidi ya moja na kila mamlaka inaurasmu wake wa kazi wakiwemo tra wakwamishaji wakuu wa uchumi wetu wenye urasmu wa hali ya juu ambao wakati mwingine haun tija.Mh anatakiwa aone umhimu wa kuunda mfumo mpya wa uendeshaji ambao utaweza kumtoa nje mtu yoyote mzembe mvivu na yoyote yule asiyefaa.

Mfano mdogo ni wa TICTs.mh anajua kabisa namna Ticts ilivo na mkataba wake na anajua kabisa container zinaibiwa Ticts lakn kwa sababu anayoijua yy anasem mAcontainer yameibiwa TPA.Hii sio sawa hata kidogo.tuko nyuma yako mh pambana na mkataba wa ticts kule ndo kuna hela na sio tpa.simanish tpa hawana kitu lkn ticts ndo hasa wanaleta matatizo haya.

Natambua mahusiano yako na wadau wakubwa wa ticts sio mazuri sana maana ww ndo mpambanaji wetu toka wakati wa richmond na wadau wakuu ndo wale wale wa ticts.sasa hapo siunaona kabisa namna kaz ilibokuwa kubwa kwako kwa mara ya pili tena.ulituahid utaeleza kila kitu wakat wa richmond mpaka sasa hujAELEZA na sasa umekutana nao tena kwa namna nyingine na uzur kwa sasa unamamlaka sio km wakat ule kwa hiyo mh fanya maamzi kila mtanzania mpenda maendeleo atakuunga mkono na siasa uziache vyeo tutakupa mbele ya safari huko baada ya safar ndefu ya mapambano hata urais tutakupa kama ukiishinda vita hii.

ukweli ni kwamba ww ni mchapakaz lkn huyu dg uliyempa akaimu udg tpa knows litle kuhusu bandar operation na ww ni shahidi wa hilo kwani yy ni mtaalam sana wa mambo ya mizani barabarani lkn ht hivyo anahitaji mgt skills imsaidie ili atimize malengo ya nchi.nimesikia kwamba siku moja alienda nje ya nchi kwenye forum ya kimataifa juu ya port operation hakuiwakilisha vizur kwan hakuwa na uelewa wa kutosha juu shughuli za bandari.anyway ataimprove as he continues bt plz supervise him otherwise atachemka.

nawasilisha

Mwakyembe angetaka "kuhangaika na watu" kama unavyosema, angeishia kumuondoa Mgawe na wenzake.

Hakuishia hapo, kaunda timu ya uchunguzi ambayo inatakiwa kuangalia hayo yote unayoyasema mambo ya institutional investigation.

Sasa utasemaje Mwakyembe anaangalia watu badala ya kuangalia system?
 
Ni watu wachache waliokuwa wanakula kutoka hapo bandarini ndio wanaopiga kelele!! Move ya Mwakyembe ni sahihi na ili kuijenga Bandari yetu, hatua aliyochukua ni nzuri na haina budi kuungwa mkono. Hatuwezi kuendelea kwa kufumbia macho watu wachache wanaoturudisha nyuma. Tumpe Mwakyembe nafasi ya kuifanyia kazi ripoti aliyopewa.
 
Mbona viongozi wa idara ya ulinzi bandarini hawakuguswa kama kuna wizi bandarini? Huyu mwakembe anatafuta watu. Hana lolote. Mnafiki mkubwa huyu. Ticts wana walinzi wao wala siyo wa tpa awashapulie hao ticts kama ana ubavu
 
Wewe umejuaje kama analenga watu fulani? Umejuaje kuwa pesa za walipa kodi zimetumika kulipia kamati ya kutoa /kushauri kuwatowa watu? Nadhani wewe ni mmoja wa wezi au yupo jamaa au ndugu yako au anyekuhusu hapo bandarini, Umejuaje kuwa kuna ushauri wa kutoa watu? Alama za mnafiki ni tatu Moja akisema a,nasema uongo, mbili akiamniwa haaminiki,akiahidi hatimizi sasa kama si mnfaki dhibitisha unayoyasema naamini huwezi kuthibitisha maana ripoti haijasomwa hadharani hivyo basi mimi:-
Nadhani wewe ni wale wezi waliyozoea kuiba bandarini naamini kama wewe si miongoni mwa waliowahi kukumbwa na matukio ya bandari yetu maana usingesema hayo; ila kwa vile ni wewe au mzazi wako au ndugu yako ananufaika na wizi unaotokea bandarini anaona si vyema kufanya hayo yanayoshauriwa na lakini kama yangemkuta ya bandari yetu asingeshauri kuondolewa watu baadhi bali wote wangeondoka maana kama ni matukio ya bandarini ni mengi na yanakera kwa mtu ambaye kweli unafahamu nini maana ya haki na wajibu wa kuhudumiwa kama mteja na kuishia kupoteza gari, vifaa vya ndani ya gari mfano radio n.k,au kupoteza document ulizoambiwa upeleke au ukawaonyeshe
Mi nadhani wewe umetumwa kuona hasira za waliokutwa na visanga vya bandari yetu maana; wateja wengi wameshakimbia je Mwakiembe aliwakimbiza?Au ndugu au wanaokusuhusu ndo wamefanya madudu kwa wateja wa bandari yetu? Je Mwakyembe aliua reli? je Mwakiembe alipitisha magogo, pembe za ndovu zinazokamatwa ughaibuni?Je mali zetu zinazopotea bandarini aliiba Mwakiembe?Kama unataka usafi Mshauri awatoe wote maana hata hao wanaofanya kazi hapo hawakuzaliwa hapo bali walijufunza?Na kumbuka ukweli haujifichi ipo siku utakuwa wazi je utasema ni siasa?
Naomba kama unaakili timamu na si kichaa au mwizi au mlamba miguu ya mabwana zako sema yaliyo ya kweli kwani haki ya mtu asipoipata hapa ataipata kwa mola wake kwa ailiyemdhulumu na mdhulumaji atapata adhabu ili ajute kwa aliyoyatenda.
Naomba tambua kuwa Mola wako anajua yaliyo moyoni mwako na kumbuka kuwa kila siku uchao unakimbilia kaburi lako ambapo ndo mwanzo wa kujua uliokuwa unayafanya ni haki au la?
Kumbuka hakuna atakayekufa kwa ajili ya mwenzake; siku yako ikifika utaondoka naomba aandaa safari yako kwenda kwa mola wako kwa kutenda yaliyomema na kama mliiba au mlifanya ubadhirifu tubuni kwani bado mko hai msisubiri mfe kwa presha na huku hamjafanya toba kwa mola wetu.
Nakusihi washauri waliokutuma kuwa walionyuma ya Mwakyembe ni wengi hata akiwatoa wote ndo bora zaidi maana akiwacha mtamfitini ili mabadiliko yasilete tija na kumbuka hakuna atakayelalamika ila wanaofaidika na wizi wa hapo na kumbuka vijana wengi wanamaliza vyuo hawana kazi na wanauwezo wa kufanya kazi na tunaomba Mwakyembe fanya kazi kama ya Magufuli toa uozo maana hata huko yaonesha kuna watoto wa vigogo kama ilivyotanroad.
 
Back
Top Bottom