Mwakyembe acha siasa bandarini, unaua uchumi wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe acha siasa bandarini, unaua uchumi wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tina, Oct 23, 2012.

 1. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Tuache siasa, bandarini tunaua uchumi

  Mwandishi wetu

  WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe sasa ametangaza kupokea ripoti ya tume aliyoiunda kuchunguza tuhuma ambazo zimekuwa zikidaiwa kuwa chanzo cha kuzorota kwa huduma za bandari zetu na hasa Bandari ya Dar es Salaam.

  Tuhuma za Dk. Mwakyembe wakati akiunda tume yake na hata sasa, zinaelekezwa tu kwa uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzani (TPA) na zaidi viongozi maalumu anaowalenga yeye tu na mfumo mzima katika sekta husika.

  Kwa kuwa waziri hana taaluma katika maswala ya usafiri kwa njia ya majini bandari nikiwa kama mmoja wa wadau kwenye sekta hiyo naamini sasa atakuwa amepata ufahamu wa kuifahamu vema sekta nzima ikiwa ni pamoja na mfumo mzima wa kupokea, kuhifadhi na kusafirisha mizigo ipitayo kwenye bandari zetu zikiwamo zile za maziwa.

  Kwa wadau waliobobea kwenye eneo hili na ambao biashara zao za kila siku hutegemea ufanisi endelevu wa kila mdau kwenye eneo hili wanategemea kuona ripoti yenye weledi na muonekano wa kitaaluma kuliko ya kutafuta makosa ndani ya mdau mmoja.

  Kwa maelezo ya Dk. Mwakyembe na wanaoungana naye, kwa sasa inaonekana tuhuma zinaelekezwa TPA ili kuhalalisha mbele ya umma kwamba Bandari ya Dar es Salaam kuna uozo, wizi, rushwa na kila aina ya uovu unaofahamika duniani.

  Baadhi ya wadau wanaona matamshi kama haya na ambayo hayajahusisha wadau wote kwa kina yanatoa taswira ambayo inaweza kuwapoteza wateja kabisa hata wateja wachache tulionao Tanzania.

  Waziri anadiriki kusema eti amehakikishiwa na mawaziri wenzake wa uchukuzi wa nchi jirani kwamba nchi hizo zitaendelea kuzitumia bandari zetu hasa ya Dar es Salaam.

  Baadhi ya wadau na wafanyabiashara wanasema kwamba mawaziri siyo wanaofanya biashara ila kazi yao ni kuweka na kusimamia sera ya biashara husika.

  Tunafahau na waziri lazima afahamu kwamba bandari haiwezi kufanya kazi zake bila kuhusisha kwa umakini sekta nyinginezo na mfanyabiashara mmoja anayemiliki meli kubwa duniani ameliambia gazeti hili wazi kwa kusema, "Bandari haiwezi kufanya kazi kivyakevyake kama kitu kilichojitenga bila vifaa, watu au taasisi na mitandao inayopaswa kufanya nayo kazi!"

  Hali kadhalika bandari haiwezi kufanya kazi ikawa na ufanisi bila kuwa na viunganishi thabiti kwa maana ya barabara, reli na mabomba ya mafuta.

  Pia bandari haiwezi kuwa na ufanisi wa kupokea mizigo mingi kwa wakati mmoja kama haina miondombinu ya kutosha na ya kisasa kama gati za kutosha na zenye kina kinachoweza kuegesha meli kubwakubwa ambazo zinaweza kutia nanga hapa kama zilivyo kwenye bandari zinazoshindana na Bandari ya Dar es Salaam.

  Ikumbukwe baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 wa Kenya kugubikwa na vurugu, wafanyabiashara wa Uganda walipata shida kutokana na mizigo yao kukwama kwenye Bandari ya Mombasa kwa zaidi ya miezi mitatu mpaka hali ilipotengemaa.

  Ni wakati huo ujumbe mzito ulikuja kutoka Uganda ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, kuja kuona uwezekano wa kutumia Bandari ya Dar es Salaam na kuahidi kwamba Uganda ingetumia kupitisha asilimia 30 ya mizigo yake hapa kama mbadala wa Bandari ya Mombasa.

  TPA ilibidi iweke wakala kule Uganda kama njia ya kuwavutia Waganda lakini wafanyabiashara wamekuwa wanasita kutokana na ukweli kwamba miundombinu yetu bado ni hafifu.

  Kukosekana kwa reli kumefanya Waganda waghairi kutokana na gharama kubwa kwa njia ya barabara wakilinganisha na umbali wa kutoka Mombasa mpaka Kampala.

  Hoja hapa ni kwamba pamoja na kuhakikishiwa na Waziri wa Uchukuzi wa Uganda wa kutoa ahadi ya asilimia 30 ya mizigo ya Uganda kupitia hapa imekuwa ni kitendawili kutokana na changamoto za mapungufu katika mtandao wetu wa njia za usafirishaji mpaka mzigo ufike Uganda au utoke Uganda mpaka bandarini Dar es Salaam.

  Kama wadau, tunaona changamoto za uendeshaji bandari ziangaliwe kitaaluma zaidi kuliko kuchukua mrengo wa kisiasa.

  Inashangaza kuona inachukua zaidi ya miaka mitano kuamua namna ya kuongeza gati mbili kwa nia ya kuongeza ufanisi kwenye sekta nzima kwa njia ya bahari ambayo faida yake yake ni kuongeza pato la taifa kwa kuwa kila mdau kwenye biashara inayohusiana na Bandari ya Dar es Salaam atakuwa anachangia kwa kiasi kikubwa kwenye GDP!

  Mombasa wanaongeza gati nne kwenye katika bandari yao na mkandarasi yuko kazini mwaka wa pili sasa.

  Pia wanajenga bandari mpya ya Lamu ambayo pia mkandarasi yuko kazini; hapa tunalumbana wakati wenzetu wanashangilia kwa ujinga wetu.

  Waziri anahusisha vipi TPA peke yake na wizi wa makontena?! Mizigo hutolewa bandarini kwa njia ya nyaraka ambazo zina mlolongo mrefu.

  Je, kama nyaraka za mzigo husika zimeghushiwa wakati mzigo unapotolewa bandarini au toka kwenye eneo linalomilikiwa TICTS, bandari au mkaguzi mkuu wa bandari atajuaje?

  Tumeona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna makontena yameshikwa huko Hongkong yakiwa na pembe za ndovu zikitokea Dar na Mombasa.

  Je, hapa TPA inahusika vipi wakati anayetakiwa kufungua na kukagua makontena kabla hayajapelekwa kwenye meli kupakiwa ni ofisa forodha?

  Ni vema wanasiasa wakajifunza kwanza jinsi bandari inavyofanya kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine ndani ya mfumo kabla ya kufanya maamuzi ambayo kwa kiasi kikubwa yatakuwa hayajengi zaidi ni kuuvuruga mfumo wote wa usafirishaji kwa njia ya majini na kuua uchumi wetu kwa maslahi ya kisiasa.


  Source: www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=41830
   
 2. J

  John W. Mlacha Verified User

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wezi(majizi) yamekasirika.. Mnampinga kwa vitu vinavyoonekana? Iweje kontena liyeyuke bandari kama kiberiti kinavyoyeyuka juu ya meza
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  yeye ni mwanasiasa lazima afanye siasa. Tatizo watendaji ni lazima wafanye kazi sio siasa
   
 4. Pdraze

  Pdraze JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  duh kachemka eti sio mtaalamu wa mambo ya usafirishaji kwani hiyo ripot kaifanya yeye peke yake??? mi nadhani kuna watu wengi ambao ni wazoefu nao walishirikishwa
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kwani Mwakyembe hiyo kazi ya uchunguzi bandarini anaifanya yeye mwenyewe?

  Mbona tumeona kamteua Bernard Mbakileki, mtu ambaye ni mwanasheria wa siku nyingi, kashakuwa mkurugenzi bandarini kwa miaka mingi na baada ya hapo kaenda kuongoza "Tanzania Central Freight Bureau" kwa hiyo ana uzoefu si tu wa kisheria kuchunguza bandarini, bali ana uzoefu wa kufanya kazi katika sekta ya uchukuzi ndani na nje ya bandari.

  Sasa mtu atasemaje Mwakyembe anaendesha uchunguzi kisiasa kwa msingi wa Mwakyembe kutokuwa na uzoefu bandarini?

  Kwani Mwakyembe anafanya yeye uchunguzi?

  Sema jingine, si hili.
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Majibu mepesi kwa hoja nzito, ndio chanzo cha matatizo yetu na hata majizi wa kweli wanasalimika kwa kuwa hatuko serious na tumatoa majibu ya mkato na ya kisiasa hata inapotokea jambo likawa zito. Tusije kukuta tunawasalimisha majizi na kuwafumba midomo wapiga kelele (wapiga filimbi). Pamoja na kazi nzuri anayoifanya Mwakyembe, naaminu anahitaji changamoto kama hizi katika hii makala ili afanye kazi vizuri na si kumsifia kwa kila kitu na kumuacha aogelee bila kuwa na koti la kumsaidia aishiwapo pumzi. Tuwe makini, tujadili mada, neno kwa neno, ili tumsaidie Kamanda wa mapambano ya ufisadi.
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  bandarini kule kuna uonevu sana hasa kama wewe ni nobody hujui mtu mi namuunga mkono tifuatifua kila kitu kuna uozo mkubwa huko bandarini mwakyembe aweke watu wapya ufanisi wa kazi tuuone vitu viwe vinapitishwa haraka na kiuhalali bila uonevu wowote
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Changamoto iko wapi katika "makala"?
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Uko sahhi mkuu, wapo waliofanya uchunguzi, tena watu wenye uzoefu, kama wale wa Tume ya Mwangosi. Tume iliundwa Agosti 24, 2012 ikapewa wiki mbili, imekabidhi juzi Oktoba 21, na bado tunaambiwa utekelezaji utachukua hadi Desemba na kwamba baadhi ya watu waliohumumu watahojiwa kwa nguvu. Huu ni ujasiri wa hali ya juu wa Waziri na kitakachomsaidia ni sisi tunaomuamini kujadili badala ya kuzuia mijadala ili afanye uamuzi akiwa na weledi wa kutosha.
   
 10. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Wezi wameguswa penyewe sasa wanahaha kutishia mwakyembe,halafu kuna wakati ni hawa hawa watu wa bandari walidai wao ndo kila kitu pale hata aje nani ataondoka yeye wao wataendelea kuwepo.waomeona anakama mmoja mmoja wanaanza kuhanyahanya.go dr.mwakyembe go!
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Nani kazuia mjadala?
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kama haina changamoto ni vyema kuikosoa mapungufu yake, ndio msingi wa mjadala. Mfano kusema kwamba Mwandishi amekosea kuingiza suala la ujio wa Waziri wa Uganda, miaka ya nyuma na baadae wafanyabiashara wa huko kushindwa kufuata maelekezo ya Waziri wao.
   
 13. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wameguswa sasa wanaanza kushambulia kote kote ,kila kitu kina mwisho wake bana kwani nyie nani mpaka mdumu milele ? toka wameniibia vitu kwenye gari yangu sina hamu nao majizi wakubwa na mtandao wao wote.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
 15. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tuendelee
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo ambayo Mwakyembe anaweza kubanwa, hasa kama hataifanyia ripoti kazi na kuonyesha assertive leadership.

  Lakini sasa hivi ndo kwanza kapewa ripoti anakuja some dimwit anaandika "makala" ambayo haina hata quote moja kutoka kwa wahusika, anaanza kulalamika Mwakyembe analeta siasa bandarini.

  Tukisema katumwa na waliotolewa tutakuwa tunakosea?
   
 17. J

  John W. Mlacha Verified User

  #17
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  huyu aliyeandika hii makala ni wazi katumwa .. Kuna maslahi ambayo wanataka Mwakyembe asiyaguse . Sijaona changamoto ambayo mnataka kumpa hapo zaidi ya kulalamika na kuogopa ufanyakazi wa mwakyembe
   
 18. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,042
  Likes Received: 7,488
  Trophy Points: 280
  Kabla ya hicho unachokicholea conclution kuwa ni siasa, hali ya bandari au Uchumi ilikuwaje? Inamaana ujio wa Mwakyembe ndiyo umeanza kuua uchumi wetu wa mabaloon au?
  Naomba msaada, maana nchi hii naweza kijifanya naijua kumbe hakuna nijualo na mwisho wa siku watu wana weza hata ku-edit uraia wangu.
   
 19. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kuwa huwa sipendi kabisa kusema kuna mtu anayetumwa, inawezekana kabisa ukawa sahihi. Na kwa kuwa haina jina, inawezekana pia aliyeandika ni mhusika ama wahusika ambao ukisoma utaona wanazungumzia mambo wanayohusija nayo ama walikuwapo wakati yakitokea. Kimsingi katika mfumo wa Kidemokrasia kika mtu anayo nafasi ya kujieleza na wanaoona anapotoka wanapata nafasi ya kumjadili. Aidha katumwa ama kajituma kutetea maslahi yake ama yao, bado tunapata nafasi ya kujua kuna watu wanaoguswa na Mwakyembe na hiyo ndio tija ya kazi yOyote. Tuliona na sote tunajua matokeo ya Richmond na hadi sasa Lowassa na wenzake wanapambana kufa na kupona kujisafisha, lakni bado
  Inawang'ang'ania hiyoRichmond. Kimsingi kama ripoti itatoka hadharani hatutakua na sababu kujadili malumbano ama utetezi wa yeyote yule bali facts zilizokusanywa na wataalamu waliobobea katika sekta husima.
   
 20. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,839
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hii story ni ya Kutungwa full!! Wezi waliojilimbikizia siku Zote Huwa wana Mbinu Kibao za Kujitetea!! Bandari sio Shamba lao!! Wapo watu wengi creative wanaoweza kuweka mambo sawa!! Kwa hiyo naona anachofanya Mwakiembe ni Sahihi Kabisa!! Fikiria wale wezi waliotaka kuiba shaba kwa kutumia Treni!! Sijajua kama wamepelekwa wapi!! Kwani Kesi Yao sijaisikia tena!!
   
Loading...