Mwakyembe: Aagiza BMT kuangalia namna ya kupunguza wachezaji wa kigeni Ligi Kuu

redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,688
2,000
Hicho anachokitaka Mwakyembe kinafaa kufanywa katika amateur league na siyo professional league.

Mtu anawekeza pesa zake halafu unamlazimisha atumie watu ambao hawatamfikisha popote ?

Haiwezekani

Sent using Jamii Forums mobile app
Lini Tanzania imekua Ligi ya kulipwa? Ligi ya Tanzania ni amature, Yanga ilifika robo ya champion league 1998, kombe la washindi Afrika 1995, Tena Yanga iliyofika robo kombe la washindi ni vijana wapya wengi ni Yanga Yoso.
Simba ilifika fainali ya Caf 1993 ikiwa naasilia 99% wazawa.
Simba juzi imeingia robo fainali Afrika na wageni wa kutosha imepigwa tano,tano, za kutosha. Inabidi vilabu virudi na mpango wa kuandaa chipkiz wake baadae iwatumie. Ayo Mambo wanayofanya wachezaji wageni Leo kwenye soka letu yalikua yanafanywa na wachezaji wetu wakibongo.
Nina hakika Yanga ya 1993 au Simba ya 1993 si Morrison au Chama wanao weza kuanza kikosi Cha kwanza.
Ili wacheze inabidi Lunyamila awekwe bench na Morrison au Marsha awekwe Bench na Chama. Shabiki yupi wa Simba au Yanga ange kuelewa!! Kocha angechezea bakora tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,507
2,000
MWAKYEMBE KILA ANAPOWEKWA ANAVURUGA HIVI AJIULIZI PAMOJA NA KUWA MWALIMU WA SHERIA KWANINI ALIONDOLEWA KUWA WAZIRI WA SHERIA, NI KUTOKANA NA MATAMKO YAKE YASIOELEWEKA
 

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,882
2,000
Wachezaji wa Tz wanaubora mdogo, hawataweza kupambania timu katika mashindano ya kimataifa...
Wacheza wote waki'Tz wanafanana viwango kuanzia FDL mpaka ligi kuu na hawataki kuimprove wanakula wageni wasiokua na ubora kama wao wawachukulie namba kwenye kikosi.

_ Satan _
Simba iliyoitoa Zamalek mwaka 2003 ugenini Misri kwenye hatua ya 16 bora na kufika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa Afrika ilikuwa na mchezaji mmoja tu wa kigeni,Ramadhani Wasso.
 

Twamo

JF-Expert Member
May 27, 2017
2,562
2,000
Wawe 10 au hata 20 kigezo cha umri ni muhimu sana! Watu kama meddy na Wawa ule umri wasiruhusiwe kucheza kwenye ligi yetu! Waende uarabuni au China!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mkale

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
1,156
2,000
mwenye uwezo apewe nafasi.. haijalishi ni mgeni ama mzawa ,kwenye mpira wa kisasa ni kupitwa n wakati kuleta sera kama izo za uzawa n ugeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Satan

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
485
500
Simba iliyoitoa Zamalek mwaka 2003 ugenini Misri kwenye hatua ya 16 bora na kufika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa Afrika ilikuwa na mchezaji mmoja tu wa kigeni,Ramadhani Wasso.
Mkuu, mpira unabadilika...
Ukiangalia mpira unaochezwa na wachezaji wa bongo peke yake utashangaa...
Wachezaji wakigeni wanafanya walau mpira uufurahie..
Kama kutakua na mipango kabambe ya kuandaa wachezaji kuanzia chini basi nitamuunga mkono waziri.
 

nkese

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
3,030
2,000
Wasalam wadau wa michezo.

Waziri wa Habari, Michezo Sanaa na Michezoi, amelitaka Baraza la Michezo Tanzania kuangalia namna ya kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni katika ligi kuu ya Tanzania.

Amesema haya wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2020/21

Kama mdau, nini maoni yako juu ya kauli hii?

Karibuni kwa mchango. Waziri Mwakyembe ataona hapa.


Sent using iphone pro max
Huyu ndiye mwenye "mawe" manne au namfananisha?
 

babu na mjukuu

JF-Expert Member
Jun 23, 2016
2,731
2,000
Itakuwa Ajibu na Ndemla wamemlalamikia waziri...mimi naona kusiwe na limit ya wachezaji wa kigeni maana wachezaji wetu wamebweteka wanakaa vijiwe vya bangi
Inashangaza sana. Yote hayo yqnafanyika kwa ajili ya Simba,Yanga na Azam. Kwani hao ndio mara nyingi wanasajili wachezaji wengi. Swali rahisi ni vilabu vingapi Tanzania wanaweza kusajili idadi kubwa ya wachezaji toka nje?
Mi nadhani waziri angehangaika na viwango na sifa za wachezaji tunao waleta toka nje. Suala la idadi liachwe kwa vilabu.

Ukiangalia idadi ya wachezaji wa ligi kuu ni zaidi ya 300. Wachezaji wa nje hawafiki hata 100. Khofu yetu ni ya nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Veto

Member
Apr 23, 2020
25
95
Bado na idadi hii iliyopo(10) timu zenye uwezo wa kusajiri wachezaji wa nje ni Simba,Yanga na Azam na timu nyingine baadhi vilevile wachezaji wa ndani ni wengi kuliko wa nje
Leo hii kuna straika gani kama kagere,kuna kiungo gani kama chama au morrisoni au beki gani kama N.Wadada au kuna Kapombe wangapi Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Veto

Member
Apr 23, 2020
25
95
Simba iliyoitoa Zamalek mwaka 2003 ugenini Misri kwenye hatua ya 16 bora na kufika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa Afrika ilikuwa na mchezaji mmoja tu wa kigeni,Ramadhani Wasso.
Tangu kipindi iko imetokea hivyo mara ngapi?
Kwa kikosi cha kipindi kile cha wazawa kuna wachezaji wazawa kama hao walioitoa Zamaleki..Tukubali,tukatae Wachezaji wetu ni wavivu,wanabweteka,determination ndogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,882
2,000
Mkuu, mpira unabadilika...
Ukiangalia mpira unaochezwa na wachezaji wa bongo peke yake utashangaa...
Wachezaji wakigeni wanafanya walau mpira uufurahie..
Kama kutakua na mipango kabambe ya kuandaa wachezaji kuanzia chini basi nitamuunga mkono waziri.
Ni sawa..mpira unabadilika.Point yangu ni lazima kuwe na regulation haiwezekani watu waamue tu bila kuwawekea sheria au kanuni..Sio kweli kuwa wachezaji wote wa bongo hawajui au sijui hawana akili.Wapo wachezaji wa bongo wenye determination hadi inafurahisha..

Pia sio wachezaji wote wanaokuja kiholela kwenye ligi ya bongo ni wachezaji wazuri kuzidi wachezaji wote wa bongo kwenye hiyo nafasi anayocheza uwanjani..Wengine ni mafamba tu na hatari ni pale timu zao zinapolazimisha wacheze kukwepa lawama za kuwa wamewanunua kwa fedha nyingi halafu wanakaa benchi..Hapa kuna shida kubwa sana na anaedhulumiwa hapa ni huyo mchezaji wa bongo mwenye uwezo kuliko mgeni lakini mgeni anacheza kwakuwa tu ni mgeni!

Sasa ni bora kupunguza idadi ili tupate kweli wachezaji wa nje ambao ni bora kuliko wetu kwenye eneo husika.Hawa akina Molinga,Yikpe,sijui wabrazil nk tutaepukana nao kama kuna kanuni.Klabu zitahakikisha zinaleta kweli wachezaji bora sio kujaza tu nafasi za kigeni eti kwakuwa kanuni inaruhusu!!
 

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
19,245
2,000
Usikose kuangalia kipindi cha Tamasha la Michezo ITV kuanzia saa nane mchana ili umshuhudie Kocha Liston Katabazi akieleza kwa undani madudu ya TFF na ubadhilifu wa pesa unaofanywa na viongozi wachumia tumbo wa shirikisho hilo ambao ndio chanzo cha kudumaa kwa mchezo wa Soka hapa nchini.
 

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,315
2,000
Mwakyembe atambue kuwa akina samatta, Msuva n.k nao ni wacheezaji wa kigeni ambao wamepata fursa

Huyu mwakyembe ni wakumstaafisha katika uchaguzi wa mwaka huu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza naona angeanza kuweka Sera kwenye michezo iliyokufa hapa Tanzania Kama ndondi,riadha,kuogelea,basket,netball n.k,akifanikiwa katika Hilo ndipo tutajua Sera zake zinaweza kuinua kiwango Cha soka nchini.

Hata hivyo Kuna michezo mingi nchini,ashughulike nayo hiyo Kwanza.

Kenya,Uganda wanatuzidi Nini hadi wawe wanashiriki aina nyingi za michezo kimataufa.
 

Dalmine

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
5,538
2,000
Ma
Wasalam wadau wa michezo.

Waziri wa Habari, Michezo Sanaa na Michezoi, amelitaka Baraza la Michezo Tanzania kuangalia namna ya kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni katika ligi kuu ya Tanzania.

Amesema haya wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2020/21

Kama mdau, nini maoni yako juu ya kauli hii?

Karibuni kwa mchango. Waziri Mwakyembe ataona hapa.


Sent using iphone pro max


Maoni yangu,,,wapunguzwe wale wabrazili hakuna wanachofanya wanakula pesa ze2 tu. Wakat tunao wachezaj wazur zaid yao na wenye thaman ndogo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom