Mwakitinya: Wapinzani kwao tume inakuwa nzuri wakishinda, wakishindwa inakuwa mbaya

Is "seifism" acceptable ?
YES, IF THE COMMISSION IS NOT CREDIBLE! THAT'S WHY THEY WANT AN INDEPENDENT COMMISSION SO AS TO AVOID THE REPEAT OF JECHAISM/SEIFISM!. That will be for the good of all well wishers and peace loving lot.
 
Ushahidi wa kwamba time yetu ni huru unaanza kwenye mchakato wa kutangaza wagombea wa vyama mpaka utangazaji matokeo kwa mshindi kulingana na idadi ya kura.

Tunaweza kusema kwamba tume si huru kwa sababu wajumbe wa tume ni wateule wa Rais, je hao wajumbe wanasaidia vipi upangaji wa washindi katika zoezi lenye mchakato mrefu na mpana wa upigaji unaosimamiwa na kuratibiwa na vyama vya siasa kwa ukaribu na umakini wa hali ya juu?

Watu wanaenda kupiga kura kukiwa na mawakala wa vyama, kura zinhesabiwa kukiwa na mawakala, fomu za idadi ya kura zinasainiwa na mawakala baada ya kujiridhisha mchakato mzima ulivyokuwa na mshindi anàtangazwa , bado mnadai mnaibiwa kura? Basi waulizeni mawakala wenu, kura zenu wamepeleka wapi na kwa nini wasaini ?

Tusidanganyane humu , kwa kila mwenye akili timamu na kwa ambaye hajui mchakato wa upigaji kura mpaka utangazaji matokeo atakubaliana nanyi lakini wenye hekima na busara wanakaa kimya wakisikia mnadai kitu kilichopo

Haya uliyoandikika ni nadharia lakini hayana uhalisia wowote. Umeandika maelezo ya jinsi tume inavyopaswa kufanya kazi, na sio jinsi inavyofanya kazi kwa uhalisia. Huo ukiukwaji mkubwa wa sheria tunauona wazi na wananchi wote wanafahamu, na chini ya awamu hii ya Magufuli, huo uhuni uko wazi. Kwa macho yangu nimeona kwenye vituo vya uchaguzi mawakala wa cdm wakipigwa na polisi ili kujaza fomu zisizo halali za matokeo, na viongozi wa tume wakiwa wako kimya kabisa. Kwa macho yetu tuliona live kupitia ITV, mabox ya kura yakitolewa vituoni ili kwenda kujaza kura za ccm, haya yalifanyika mbele ya macho ya polisi na wasimamizi wa tume ya uchaguzi, na bado ndani ya ushenzi wote huo tume ya uchaguzi bado ilitangaza mshindi! Kwakuwa kulikuwa kunafanyika ushenzi na uhayawani wa wazi, ndio maana ikatolewa amri ya vyombo vya habari kutotangaza na kurusha yanayojiri kwenye chaguzi mbali mbali hapa nchini. Hayo ni mambo yanayofanyika chini ya awamu hii ya tano na yana baraka zote za rais wa sasa.

Hiyo ndio namna mpya toka Magufuli aingie madarakani asilimia zaidi ya 80 washindi wa ccm wanaotangazwa na tume ya uchaguzi wanavyopatikana. Kutokana na ushenzi na uhayawani wa wazi uliongia katika chaguzi zetu chini ya awamu huu ya tano, ndio maana wananchi wengi walisusia kujiandikisha kupiga kura uchaguzi wa SM. Na hata huo uchaguzi wa 2020 iwapo hakutakuwa na tume huru ya uchaguzi inayoweza kufanya kazi yake bila kuingiliwa na rais au mwanaccm yoyote, hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu ataweza kushiriki huo ushenzi. Wananchi walishatoka utumwani Misri, hawawezi tena kurudishwa kwenye mfumo wa chama kimoja kwa matumizi mabaya ya madaraka ya urais.
 
Chadema.ni kichaka cha wakora,hawaeleweki wanataka nini katika jamuhuri hii
"Nawashangaa sana wapinzani wanalalamika wanataka Tume huru ya uchaguzi kana kwamba hakuna tume, kungekuwa hakuna tume huru kule bungeni kusingekuwa na wawakilishi wao au kwenye madiwani. Wao Tume inakuwa nzuri wakishinda, wakishindwa inakuwa mbaya"- MNEC Mwakitinya.

Nashindwa kuwaelewa hawa viongozi wengine wanaoshindwa kutafsiri maana ya tume huru sijui huo uongozi waliupataje.

View attachment 1322054

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ndio ukweli kama sio tume huru hawa walishindaje?


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hukuepo vituoni 2015..... Mdee kapambana mpaka kura zimerudiwa kuhesabiwa..... Wenje mpaka ngumi zilirushwa kituoni kura zikarudiwa..... Mnyika mpaka wananchi walitishia kuchoma kituo ndio akatangazwa.... Kule mbagala ni mabomu na vituo vikachomwa hadi uchaguzi ukafutwa.

Hakuna jimbo upinzani ameshinda kiuwepesi bila nguvu ya umma.... Ni Ujiji tu ndio Zitto alitangazwa mapema sana bila figisu!!
 
Huyo hata ukimueleza kiasi gani maana akili zake zinashikiliwa na chakubanga pale lumumba
Mkuu hukuepo vituoni 2015..... Mdee kapambana mpaka kura zimerudiwa kuhesabiwa..... Wenje mpaka ngumi zilirushwa kituoni kura zikarudiwa..... Mnyika mpaka wananchi walitishia kuchoma kituo ndio akatangazwa.... Kule mbagala ni mabomu na vituo vikachomwa hadi uchaguzi ukafutwa.

Hakuna jimbo upinzani ameshinda kiuwepesi bila nguvu ya umma.... Ni Ujiji tu ndio Zitto alitangazwa mapema sana bila figisu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ndio ukweli kama sio tume huru hawa walishindaje?


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Hatimaye nimepata kipimo cha ufahamu wako. Itanisaidia siku za usoni kukuelewa. Lakini nikwambie tu jambo hapa - uchaguzi sio tukio linalojitenga bali tegemezi. Tume huru ni ile iliyo na uwakilishi usioegemea upande mmoja. Tumesikia na kuona form zikitolewa na kupokelewa kwa zengwe, wajumbe wakiwekewa mapingamizi yasiyo na msingi na rufaa zao kukataliwa au kucheleweshwa kwa makusudi. Mawakala wa uchaguzi kukataliwa vituo vya kupiga kura. Kura kuibwa na matukio mengi yanayohusu wajibu wa Polisi katika kampeni za siasa. Na yote hayo yamefanywa kwa kupendelea wateuzi wa Tume ya Uchaguzi.

Tume huru inapata nafasi ya kuwa na mtazamo wa haki na usawa. Kwa sasa mambo hayo mawili hayaonekani kutendwa!!

Umeuliza hao walioshinda wameshindaje. Jibu - figisu na zengwe hazikufanikiwa katika maeneo walioshinda.
 
Back
Top Bottom