Mwakiteleko Aaagwa na Idadi Kubwa ya ...Haijapata Kutokea!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,463
113,530
Mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Rai na Mhariri Mtendaji Msaidizi wa New Habari Corporation Limited, Danny Mwakiteleko, aliyefariki dunia juzi alfajiri katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), Dar es Salaam, umeagwa rasmi leo nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam na Maelfu ya waombolezaji, ikiwemo idadi kubwa ya waandishi wa habari kwa kiwango ambacho haijapata kutokea.

Takwimu za kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kutokea kati ya misiba ya wanahabari niliobahatika kuihudhuria, hivyo idadi hiyo ni kwa mujibu wangu niliyovyowashuhudia mimi binafsi, na sio kwa utafiti, takwimu wala hojaji, bali ni massive press turn out. Turn out hiyo ni uthibitisho kuwa Danny alikuwa mtu wa watu.

Turn out hiyo imehusisha kwanza wahariri toka vyombo vyote vya habari jijini waliovalia sare rasmi, kundi kubwa la waandishi na watangazaji toka vyombo vyote vya habari jijini, idadi kubwa ya maofisa habari toka wizara, idara, na mashirika mbalimbali pamoja na idadi kubwa ya waandishi wakongwe toka enzi za Radio Tanzania na Magazeti yakiwa ni Daily Nuwes na Uhuru Pekee.

Idadi hiyo kubwa ya waandishi, pia imejumuisha baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari, na wakurugenzi wa mawasiliano mbalimbali, wakiongozwa na mkurugenzi wa mawasiliano muhimu kuliko wengine wote.

Mwakiteleko anatarajiwa kuzikwa kesho, kijijini kwao Rugombo, Mwakaleli mkoani Mbeya

Mwakiteleko ameacha mjane, Winifrida na watoto Caro (13) na Vanessa (11).

Mungu Aipumzishe roho ya Danny Mwakiteleko, Mahala Pema Peponi, Apumzike kwa Amani

Amen.

Pasco.

Picha kwa Hisani ya Globu ya Jamii.





Wadau mbalimbali msibani

Wahariri wakiwa tayari kutoa mwili wa marehemu

Safari inaanza
Mbunge wa Bumbuli mh. January Makamba akitoa heshima zake

Askari akiaga kijeshi


Askari akiaga kijeshi

Ankal na wapiganaji wakimuaga Danny
Abdallah Majura, Mkurugenzi Mtendaji wa Sports FM na Hassan Mhelela wa BBC

Mkuu wa Kurugenzi ya Habari Ikulu Bw. Salva Rweyemamu akiwa na wanahabari wenzie katika msiba wa Danny Mwakiteleko huko Tabata Chang'ombe jijini Dar ambpoe baada ya heshima za mwisho mwili wake umesafirishwa leo kuelekea Mwakaleli, Tukuyu, kwa Mazishi


Wanahabari wakibadilishana mawazo


Wabahabari wakiwa msibani.


Umati wa wanahabari, wanasiasa, ndugu jamaa na marafiki msibani


Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Absolom Kibanda akiongea na Badra Masoud wa TANESCO na Usiah Mkoma wa UN


Wahariri waandamizi msibani


Majonzi


Saluti kwa Danny Mwakiteleko toka kwa wafanyakazi na mkewe hospitali ya jeshi Lugalo


Wahariri wakiwa wamejipanga tayari kubeba mwili wa marehemu kuupeleka garini


Marafiki wa karibu na marehemu, Angetilleh Osiah, Msoud Sanani nna Juma Pinto


Wahariri wakisubiri muda


Wadau toka kila nyanja walikuwepo msibani


Mpiganaji Athumani Hamisi na wadau wengine wapo
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi, akiongea na Salva

Wazee wa familia na viongozi wa dini wakiwa msibani


Wadau msibani


Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. John Mongella akiongea na Mkurugenzi mtewndaji wa New Habari Corporation Bw. Bashe (kati) na Bw. John Nchimbi msibani


Majonzi na vilio vyatawala


Eric shigongo na wadau wengine msibani


Beka Tall (shoto) na Beka Hendsam (kati) wakiwa na Kaka John Bwire


Msafara unaanza
Mhariri Mtendaji wa Mtanzania Bw. Deo Balile (suti) akiwa na wapiganaji wenzie

Jeneza latolewa nje


Mke na watoto wa marehemu wakiaga


Mpiganaji Athumani Hamisi akimuaga Danny

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absolom kibanda akitoa heshima zake za mwisho




 
nini hasa unataka ku address mtoa mada!
ndio watu wengi wamejitokeza so........?

mix with yours
 
nini hasa unataka ku address mtoa mada!
ndio watu wengi wamejitokeza so........?

mix with yours

Mbona ameshajibu kwenye post yake!

Takwimu za kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kutokea kati ya misiba ya wanahabari niliobahatika kuihudhuria, hivyo idadi hiyo ni kwa mujibu wangu niliyovyowashuhudia mimi binafsi, na sio kwa utafiti, takwimu wala hojaji, bali ni massive press turn out. Turn out hiyo ni uthibitisho kuwa Danny alikuwa mtu wa watu.
 
Hii inaionyesha ni jinsi gani danny alikuwa mtu wa watu na mchapakazi hodari. Tutamkosa sana kwenye fani
 
Back
Top Bottom