Mwakilishi wa wayahudi katika bunge la Iran: Hatua ya Trump ya kuitambua Jerusalem ni ubaguzi wa kimbari

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,685
2,000
Mwakilishi wa jamii ya wachache ya Mayahudi katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya rais wa Marekani ya kuitangaza Baitul Muqaddas mji mkuu wa utawala wa Kizayuni ni ubaguzi wa kimbari.
Dokta Siamak Moreh Sedgh ameashiria hatua iliyochukuliwa na Donald Trump ya kuitambua rasmi Quds tukufu kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel na kueleza kwamba: kwa mujibu wa kanuni za kidhalimu za kimataifa zilizopo, Baitul Muqaddas ni eneo lililovamiwa na linalokaliwa kwa mabavu.
Mwakilishi huyo wa Mayahudi katika bunge la Iran amebainisha kuwa, kwa kuitangaza Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni, Rais wa Marekani Donald Trump ameonyesha kuwa hakubaliani na mfumo wa kionevu na kidhalimu uliopo hivi sasa duniani; na anachotaka yeye ni kuwa na dunia yenye mfumo wa kidhalimu zaidi ya uliopo.
Moreh Sedgh ameongeza kuwa Trump amezidharau hata sheria zinazokubaliwa na madhalimu katika uhusiano wa kimataifa, na hii inaonyesha kuwa tabia yake ni ya ubaguzi wa rangi na kimbari na isiyo na utu.
Tarehe 6 ya mwezi huu wa Desemba, Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kuitambua rasmi Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel; hatua ambayo imekabiliwa na upinzani mkubwa wa walimwengu, viongozi wa nchi na jumuiya za kimataifa.
Mji wa Baitul Muqaddas, ulipo msikiti mtukufu wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu isiyotenganika na Palestina na ni moja ya maeneo matatu matakatifu ya Kiislamu yenye umuhimu na hadhi maalumu kwa Waislamu wote duniani...
Source;Iqna.ir
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,987
2,000
Kibla cha kwanza! Haikutegemewa aongee tofauti na alivyoongea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom