Mwakilishi Haji Khatib Kai (CUF) ataka Muungano Uvunjike, Mwingine Ataka Kura ya Maoni

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Mmoja ataka uvunjike, mwingine kura ya maoni

Mjadala kuhusu kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, umefika pabaya, kufuatia baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar na Wawakilishi, kutaka Muungano huo uvunjwe kwa madai kwamba, unawapendelea wananchi wa Tanzania Bara na kuwaacha nyuma Wazanzibari katika maendeleo.

Matamshi hayo yalitolewa na wabunge hao kwa nyakati tofauti walipokuwa wakichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, bungeni, mjini hapa jana. Mbunge wa Micheweni (CUF), Haji Khatib Kai, alisema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano, ambayo iliunda mataifa mawili yakiwa na lengo la kuunda taifa litakalosimamia maendeleo ya nchi.

Hata hivyo, alisema kinyume cha matarajio hayo, kila siku Wazanzibari wamekuwa wakinanung’unika zaidi kuhusu kubanwa na kero za Muungano, ambazo kila wakati zimekuwa zikizungumzwa bungeni, lakini hadi sasa serikali haijaeleza kama zimetatuliwa au la. “Wakati mwingi Wazanzibari wananung’unika zaidi kuliko Watanzania Bara.

Wazanzibari imefika mahali hawana imani na Muungano huu kwa sababu wao ndio walio nyuma katika maendeleo, lakini ikiangalia Tanzania inasonga mbele,” alisema Kai.

Aliongeza: “Kwa hivyo, tunachokisema na tunachokiomba ikiwa serikali hii imeona kwamba Zanzibar imekuwa kikwazo ama imekuwa kero ama mzigo, basi ni vema watuache…narudia tena kusema ikiwa Zanzibar imekuwa mzigo na imekuwa kero, basi hebu tuachieni huo mzigo, uteremsheni kichwani ili muwe huru. La, si hivyo vinginevyo, basi afadhali Muungano huu uvunjwe, uundwe tena iwapo itawezekana.”

Kauli hiyo ilimfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuingilia kati na kumtaka mbunge huyo kusubiri mchakato wa kuandika Katiba mpya ili watumie fursa hiyo kutoa maoni yao.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Spika Makinda haikufua dafu, kwani Mbunge wa Mgogoni (CUF), Kombo Khamis Kombo, naye aliposimama kuchangia mjadala huo, aliendeleza hoja ya Kai kuhusu kero za Muungano.

Alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina wizara 26, ambazo kati ya hizo, sita ni za Muungano na kusema hali hiyo inamaanisha kwamba, mambo yote, ambayo si ya Muungano, yanapangiwa bajeti ndani ya serikali hiyo.

“Mheshimiwa Spika, tuangalie kutakuwa na usawa gani katika Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar?” alihoji.

Alisema licha ya kwamba mambo ambayo si ya Muungano yamezungumzwa kwenye Katiba, kimantiki hakuwezi kuwa na usawa katika Muungano kama wizara za Muungano ni sita na wizara zilizokuwa si za Muungano ni 20 na bajeti ni moja.

Kombo alisema kama kweli serikali ya Jamhuri ya Muungano ina nia ya dhati ya kutatua kero zilizomo ndani ya Muungano, anaamini mapendekezo ya JFC (Kamati ya Pamoja ya Fedha) yangelifuatwa kama yalivyo, lakini hayakufuatwa.

Alisema anaamini hakuna ukweli wa dhati wa kutatuliwa kero hizo na kuitaka serikali ikae ikijua kwamba, imewafikisha Wazanzibari kuona kwamba, Serikali ya Muungano wa Tanzania inawadhalilisha.

Kombo alisema kuna wanajeshi, polisi na wafanyakazi wengine Zanzibar, ambao wanatumia huduma visiwani humo, lakini hawalipi kodi kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzinbar (SMZ), badala yake kodi zao zote zinaelekezwa Serikali ya Muungano.

Alisema Serikali ya Muungano imekuwa ni ‘juja wa maajuja’ kwa Wazanzibari kwa kuifanya Zanzibar haina haki wala uwezo wa kuweza kupewa nafasi ya kuitumikia Tanzania nje ya nchi. “Tuangalie mabalozi waliopo.

Zanzibar ina mabalozi wanne tu. Na hawa wote hupangwa katika nchi za Kiarabu, nchi za Kiislamu. Isipokuwa Mheshimiwa Mapuri (Ramadhan Omar) labda kapelekwa China.

Sasa niseme kwamba, Wazanzibari nao wana haki na uwezo katika Muungano huu na wana haki ya kupewa wafanyakazi kufanya katika ofisi za kibalozi,” alisema Kombo.

Alisema kuna kamati, ambazo huundwa mara kwa mara kushughulikia kero za Muungano, ikiwamo Tume ya Jaji Francis Nyalali, ambayo alisema ilikuja na mapendekezo yake, lakini mpaka leo hawajui yalikokwenda.

Kombo alisema pia kuna kamati ya Shellukindo, lakini ripoti yake mpaka leo haijatolewa na pia kuna ya Amina Salum Ali, ambayo hadi leo haijatolewa na kuhoji: “Hivi tuamini kuna kamati gani itaweza kukaa kutatua kero za Muungano?

Kutokana na hali hiyo, alisema haamini kwamba, Serikali ya Muungano ina nia ya dhati ya kutatua kero zilizomo kwenye Muungano, hivyo, akamtaka Waziri Mkuu kusimamia jambo hilo ili lipatiwe ufumbuzi ili Wazanzibari waweze kujenga imani ya dhati.

MWAKILISHI ATAKA KURA YA MAONI
Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana alishauri Serikali ya Mapinduzi kuitisha kura ya maoni itakayoamua hatma ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.

Saleh Nassor Juma (Wawi-CUF) alisema kura hiyo itumike kupata maoni iwapo wananchi wa Zanzibar wanataka au hawautaki Muungano.

Saleh alikuwa anachangia makadirio ya bajeti ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Baraza la wawakilishi jana, alisema walio wengi Zanzibar wanatofautiana kuhusu suala la Muungano uliofikiwa baina ya pande hizo mbili mwaka 1964.

Alisema makubaliano ya Muungano yanainyima Zanzibar fursa ya kuongoza taasisi nyeti kama vile Idara za Polisi, Usalama wa Taifa, Jeshi na Bunge.

“Mheshimiwa Spika, iitishwe kura ya maoni haraka … Zanzibar haijawahi kuongoza nafasi ya juu katika vyombo vya ulinzi na usalama,” alisema.

Saleh alisema kuwa marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yameipa Zanzibar hadhi ya kuwa nchi, hivyo pia ni lazima iruhusiwe kujiunga na Jumuiya Afrika Mashariki bila kupitia mgongo wa Serikali ya Muungano.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakari Khamisi Bakari, alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali kwa sababu uliridhiwa na wabunge kutoka pande zote za Muungano.

Waziri Abubakari alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi, Omar Ali Sheha (CUF) wa Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.

Alisema kwamba mkataba wa Muungano uliridhiwa na wabunge wote kutoka Tanzania bara na Zanzibar jambo ambalo linaonyesha uhalali wake.

Alisema kwamba mkataba wa Muungano ulitakiwa kuridhiwa na Bunge na Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM) taratibu ambazo zimezingatiwa baada ya wabunge kutoka pande mbili za Muungano kuridhia mkataba huo.

Hata hivyo, alisema kwamba jambo lolote linalotumika kwa muda mrefu bila kuhojiwa uhalali wake huwa ni halali kutokana na uwepo wake.

“Muungano ni halali kwa sababu mkataba wa Muungano ulipitishwa na wabunge wakiwemo wa pande zote kwa utaratibu uliowekwa na katiba katika kupitisha mambo ya Muungano,” alisema.

Aidha, alisema kwamba mambo yaliyoorodheshwa ya Muungano hivi sasa yamefikia 22 kutoka 11 na sio zaidi ya 30 kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Hata hivyo, alisema kwamba kwa mujibu wa katiba mambo ya Muungano hayawezi kuongezwa au kupunguzwa hadi ipatikane theluthi mbili ya wabunge kutoka Tanzania Zanzibar na Bara.

Awali, Sheha alitaka kujua taratibu gani za kikatiba zimezingatiwa kabla ya mambo ya Muungano kuongezwa kutoka 11 tangu kufikiwa kwa Muungano huo mwaka 1964.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa (Viti Maalum-CCM), Raya Suleiman Hamad, alisema Muungano wa Tnganyika na Zanzibar umeleta faida kubwa ikiwemo kujenga umoja wa kitaifa kwa wananchi wake “Leo Ndugu zetu wapo Tanzania Bara ukivunjika waende wapi, jambo la msingi ni kurekebisha kasoro za Muungano kwa sababu umeleta faida kubwa kwa wananchi,” alisema mwakilishi huyo.

Akifunga Mjadala, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alisema Muungano umeleta faida kubwa na tayari kero mbalimbali zimepatiwa ufumbuzi kupitia Kamati ya pamoja ya kujadili kero za Muungano.

Kuhusu utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar, Balozi Iddi alisema suala hilo haliwezi kutekelezwa kabla ya kufanyika marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kuwataka Wajumbe wa Baraza hilo kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kulitafutia ufumbuzi.

CHANZO: NIPASHE
 
..waanze kwa kugomea shughuli zote za serikali ya muungano pamoja na bunge.
 
...Wazanzibari imefika mahali hawana imani na Muungano huu kwa sababu wao ndio walio nyuma katika maendeleo, lakini ikiangalia Tanzania inasonga mbele," alisema Kai.
...
Zanzibar iko nyuma na tanzania inasonga mbele! Sasa hiyo Tanzania si ndio pamoja na Zanzibar!? Au hapendi Tanzania kwa ujumla wake isonge mbele?
 
Kama hawataki muungano kwa nini wanapanda boti kuja Bara kwa vikao vya bunge? wabaki Zanzibar na watangaze kwa sauti ya juu kabisa kuwa muungano basi.
 
Wamwambie makamu na raisi wao watoe tamko
nani anashida nao kama kweli wanania hakuna haja ya kupiga kelele kila siku
waende umoja wa mataifa kama sudani ya kusini

au waite kura kama wanavyosema dhahabu ya mwabui, geita na nyamongo, na utalii wa serengeti kilimanjaro unajenga barabara na kutoa huduma zanzibar harafu leo wanajifanya wanamali kisa mafuta waende.

ndipo watagundua kwamba watalii walikuwa wankwenda zanzibar kama sehemu ya safari ya serengeti na kilimanjaro
 
Katiba yao haikuliona hili na kulijadili wakati wanaiga kura ya maoni ya umoja wa kitaifa?wagomee vikao vya dodoma tuone kuwa wamedhamilga,waache porojn faida nionayo mimi ni tunapata vitu kwa bei ndogo kutoka kwa wapemba basi.
 
Ukweli ni kwamba hakuna muungano hapa kuna nchi moja yenye serikali mbili!! uwezi kuwa serious unasema kuna muungano wakati Zanzibar haitambuiliwi, inategemea Tanzania kwenye kila kitu, haina mchango unaoonekana!. Hao wabunge wana ndoto kwamba kuna nchi ambayo inaweza kujitemea kama vile wanakipato!!!. Zanzibar ni jina tu lakini muungano umekufa siku nyingi sana sasa nchi ni moja ya Tanzania. Kama kuna Muungano hiyo nchi ya Tanganyika iko wapi!!!.
 
Zanzibar iko nyuma na tanzania inasonga mbele! Sasa hiyo Tanzania si ndio pamoja na Zanzibar!? Au hapendi Tanzania kwa ujumla wake isonge mbele?
Sio rahis kutofautisha tanzania na tanganyika,mpaka uende shule
 
Thursday, 26 April 2012 09:52

Elias Msuya

WAKATI Muungano kati ya Tanganyika ukiwa umetimiza miaka 48 sasa, kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa pande zote, watu wakihoji uhalali wake.
Inaonyesha Muungano huu ulikuwa wa ghafla mno huku wananchi wakiwa hawajui nini kilichokuwa kikiendelea, tayari viongozi walishachukua uamuzi mkubwa wa kuunganisha nchi mbili.
Kuna mengi yanayosemwa kuhusu chanzo cha Muungano huo, lakini itoshe tu kusema kuwa hata kama kulikuwa na sababu za msingi kiasi gani, bado wananchi walipaswa kushirikishwa.
Kama kuna mambo ambayo nimekuwa nikitofautina na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere basi ni suala hili la Muungano. Siyo kwamba naupinga Muungano, ila sikubaliani na njia zilizotumika kuingia kwenye muungano.
Ni sawa na kumlazimisha kijana kuoa mke asiyemtaka, hata kama kuoa ni muhimu, bado mwoaji au mwolewaji ana haki ya kumchagua amtakaye.
Lakini inaonyesha Mwalimu Nyerere na Abeid Karume waliwalazimisha Watanzania kuingia kwenye muungano bila hata kuwauliza. Halafu walipomaliza wakapigilia misumari, eti mtu asihoji Muungano. Kwamba kuhoji Muungano ni uhaini.
Wakawarithisha vijana wao waliowarithisha madaraka dhana hiyo. Ndiyo maana hata kwenye mchakato huu wa kuandika Katiba, kuna kipingele ambacho hata hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiwaapisha wajumbe wa Tume ya Katiba alikitaja kwamba, wananchi wasijadili kuvunja Muungano bali kuurekebisha.
Kwa nini Rais Kikwete alikazia kipengele hiki? Inawezekana ni kuendeleza dhana ile ile ya kuwalazimisha Watanzania kukubali mambo wasiyoyataka.
Kama kweli Rais Kikwete amefungua mlango wa mjadala kwa Watanzania kujadili mustakabali wa nchi yao, kwa nini tena aweke vikwazo hapa na pale? Je, Watanzania watapata Katiba wanayoitaka?
Kwa mtazamo wangu, naona suala la Muungano ndiyo kero ya kwanza kwa Watanzania, sasa kama kero hiyo ndiyo imeshaanza kuwekewa mizengwe, tusitegemee kupata Katiba tuitakayo.
Jitihada nyingi zimekuwa zikifanywa ili kuondokana na kero za Muungano. Kwa upande wa Bara watu kadhaa walijikuta kwenye matatizo, kwa sababu tu ya kuhoji Muungano.
Mwanzoni mwa miaka ya 1990 baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maarufu kwa jina la G55 walijipanga na kupeleka hoja bungeni wakidai Serikali ya Tanganyika.
Lakini wakati huo Mwalimu Nyerere akiwa hai aliingilia kati na kuwazima. Kama hiyo haitoshi, alimkosoa vikali aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo Samuel Malecela kwamba alishindwa kumshauri Rais Ally Hassan Mwinyi.
Huko Zanzibar nako kumekuwa na harakati nyingi za kuuhoji Muungano. Vikundi mbalimbali vimeanzishwa vikihoji na hata kutaka upya uhuru wa Zanzibar.
Mwaka huu mambo ndiyo yamepamba moto, huku vikundi hivyo vikijifua kutaka kuitoa Zanzibar kwenye Muungano.
Fukuto hili lote limesababishwa na waasisi na waendelezaji wa Muungano. Tangu Muungano ulipoanzishwa, wananchi hawakushirikishwa kikamilifu, lakini hadi leo bado Serikali haitaki kuwashirikisha, je, unategemea nini?
Makundi haya yatakwenda mbali na kuanzisha vurugu zisizo na msingi. Usishangae kuona makundi ya kigaidi kwenye nchi za wenzetu, kama vile, Al-Qaeda, al-Shabab, Boko haram na mengineyo mengi, yamezalishwa na tabia hizi za kutowashirikisha wananchi kwenye mambo yanayohusu maslahi yao. Kwa nini tufike huko?
Nadhani njia bora ya kuepukana na hili ni kuwashirikisha wananchi hatua kwa hatua katika ujenzi wa Taifa lao. Kwa suala hili la Muungano, wananchi washirikishwe upya. Serikali iitishe kura ya maoni kuwauliza wananchi wa Bara na visiwani kama wanautaka Muungano.
Kura zikishapigwa na majibu yakipatikana Serikali sasa ipime kama unakubalika basi tuendelee nao, ila kama haukubaliki, tufikirie vinginevyo. Inawezekana wananchi wakapiga kura ya kuukataa Muungano, lakini Serikali ikatoa sababu za kuendelea na muungano ambao wananchi hawautaki. Hilo litakuwa jema kuliko kufunika funika matatizo katika Muungano.
Serikali inaweza kuleta hoja zake za kuonywsha umuhimu wa kuwa na Muungano nazo zipimwe kama zitakubalika basi tunaweza kuendelea nao. Kwa mfano kama kuna maslahi ya kitaifa ambayo tunayapata katikaMuungano na ambayo hayaepukiki, basi yaelezwe. Lakini siyo kama ilivyo sasa ya kukatazwa hata kuujadili tu Muungano.
Kwa kuwa tayari Rais Kikwete ameshaweka kigingi kwenye mjadala wa Muungano, nashauri kura za maoni zitofautishwe na Kura ya Maoni ya Katiba. Vinginevyo, Tume ya Katiba ipewe pia jukumu la kuwahoji wananchi kama wanauhitaji Muungano au la. Hapo ndipo tutapata picha halisi ya nini kinachotakiwa na wananchi.
Sijui kwanini Serikali inaona ugumu wa kufanya hivyo, lakini nadhani hii ndiyo njia sahihi ya kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa taifa lao. Huu ndiyo wakati mwafaka wa kuujadili Muungano, siyo wakati wa kufunika funika, Waswahili wanasema; ‘Mficha …., hazai!”
Elias Msuya ni mwandishi wa makala wa gazeti la Mwananchi; 0754 897 287

Elias Msuya
wewe umeonesha uelewa mkumbwa wa mambo ya muungano tafauti na wachangiaji wengi humu JF
wazanzibar walipokwenda baraza la wawakilish Kudai kura ya maoni kuhusu muungano14/04/2012 POLISI WALIWEKA BANGO JEKUNDU
ILANI ILANI ILANI WATU WOTE WALIOKUSANYKA HAPA WANAAMRISHWA NA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUTAWANYIKA HARAKA KWA AMANI VYENGINEVYO NGUVU ZITATUMIKA

ndio maana tunasema tunataka uhuru wa zanzibar upya,,,mm naone hatari ya alichokitahadharisha Elias Msuya.WAZANZIBAR tunafikishwa mahala tuwe hatuna option ila bokoharam na al qaida. tusifike huko jamanii mambo hayo yakiaza hakutokua na nguvu itakayo weza kuzima moto...KINGA NI BORA KULIKO TIBA

''JAMUHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA ''kwa harama yoyote ile.
 
Who cares?? let it go!!

Kwani ubaguzi na kubebwa nani anaongoza kati ya Tanganyika na Zanzibar??
ON ZANZIBARIS; They have a different identity (frm Tanganyikans). They are Zanzibaris- Mtikila, 1993.
 
Mmoja ataka uvunjike, mwingine kura ya maoni

Mjadala kuhusu kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, umefika pabaya, kufuatia baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar na Wawakilishi, kutaka Muungano huo uvunjwe kwa madai kwamba, unawapendelea wananchi wa Tanzania Bara na kuwaacha nyuma Wazanzibari katika maendeleo.

Matamshi hayo yalitolewa na wabunge hao kwa nyakati tofauti walipokuwa wakichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, bungeni, mjini hapa jana. Mbunge wa Micheweni (CUF), Haji Khatib Kai, alisema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano, ambayo iliunda mataifa mawili yakiwa na lengo la kuunda taifa litakalosimamia maendeleo ya nchi.

Hata hivyo, alisema kinyume cha matarajio hayo, kila siku Wazanzibari wamekuwa wakinanung'unika zaidi kuhusu kubanwa na kero za Muungano, ambazo kila wakati zimekuwa zikizungumzwa bungeni, lakini hadi sasa serikali haijaeleza kama zimetatuliwa au la. "Wakati mwingi Wazanzibari wananung'unika zaidi kuliko Watanzania Bara.

Wazanzibari imefika mahali hawana imani na Muungano huu kwa sababu wao ndio walio nyuma katika maendeleo, lakini ikiangalia Tanzania inasonga mbele," alisema Kai.

Aliongeza: "Kwa hivyo, tunachokisema na tunachokiomba ikiwa serikali hii imeona kwamba Zanzibar imekuwa kikwazo ama imekuwa kero ama mzigo, basi ni vema watuache…narudia tena kusema ikiwa Zanzibar imekuwa mzigo na imekuwa kero, basi hebu tuachieni huo mzigo, uteremsheni kichwani ili muwe huru. La, si hivyo vinginevyo, basi afadhali Muungano huu uvunjwe, uundwe tena iwapo itawezekana."

Kauli hiyo ilimfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuingilia kati na kumtaka mbunge huyo kusubiri mchakato wa kuandika Katiba mpya ili watumie fursa hiyo kutoa maoni yao.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Spika Makinda haikufua dafu, kwani Mbunge wa Mgogoni (CUF), Kombo Khamis Kombo, naye aliposimama kuchangia mjadala huo, aliendeleza hoja ya Kai kuhusu kero za Muungano.

Alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina wizara 26, ambazo kati ya hizo, sita ni za Muungano na kusema hali hiyo inamaanisha kwamba, mambo yote, ambayo si ya Muungano, yanapangiwa bajeti ndani ya serikali hiyo.

"Mheshimiwa Spika, tuangalie kutakuwa na usawa gani katika Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar?" alihoji.

Alisema licha ya kwamba mambo ambayo si ya Muungano yamezungumzwa kwenye Katiba, kimantiki hakuwezi kuwa na usawa katika Muungano kama wizara za Muungano ni sita na wizara zilizokuwa si za Muungano ni 20 na bajeti ni moja.

Kombo alisema kama kweli serikali ya Jamhuri ya Muungano ina nia ya dhati ya kutatua kero zilizomo ndani ya Muungano, anaamini mapendekezo ya JFC (Kamati ya Pamoja ya Fedha) yangelifuatwa kama yalivyo, lakini hayakufuatwa.

Alisema anaamini hakuna ukweli wa dhati wa kutatuliwa kero hizo na kuitaka serikali ikae ikijua kwamba, imewafikisha Wazanzibari kuona kwamba, Serikali ya Muungano wa Tanzania inawadhalilisha.

Kombo alisema kuna wanajeshi, polisi na wafanyakazi wengine Zanzibar, ambao wanatumia huduma visiwani humo, lakini hawalipi kodi kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzinbar (SMZ), badala yake kodi zao zote zinaelekezwa Serikali ya Muungano.

Alisema Serikali ya Muungano imekuwa ni ‘juja wa maajuja' kwa Wazanzibari kwa kuifanya Zanzibar haina haki wala uwezo wa kuweza kupewa nafasi ya kuitumikia Tanzania nje ya nchi. "Tuangalie mabalozi waliopo.

Zanzibar ina mabalozi wanne tu. Na hawa wote hupangwa katika nchi za Kiarabu, nchi za Kiislamu. Isipokuwa Mheshimiwa Mapuri (Ramadhan Omar) labda kapelekwa China.

Sasa niseme kwamba, Wazanzibari nao wana haki na uwezo katika Muungano huu na wana haki ya kupewa wafanyakazi kufanya katika ofisi za kibalozi," alisema Kombo.

Alisema kuna kamati, ambazo huundwa mara kwa mara kushughulikia kero za Muungano, ikiwamo Tume ya Jaji Francis Nyalali, ambayo alisema ilikuja na mapendekezo yake, lakini mpaka leo hawajui yalikokwenda.

Kombo alisema pia kuna kamati ya Shellukindo, lakini ripoti yake mpaka leo haijatolewa na pia kuna ya Amina Salum Ali, ambayo hadi leo haijatolewa na kuhoji: "Hivi tuamini kuna kamati gani itaweza kukaa kutatua kero za Muungano?

Kutokana na hali hiyo, alisema haamini kwamba, Serikali ya Muungano ina nia ya dhati ya kutatua kero zilizomo kwenye Muungano, hivyo, akamtaka Waziri Mkuu kusimamia jambo hilo ili lipatiwe ufumbuzi ili Wazanzibari waweze kujenga imani ya dhati.

MWAKILISHI ATAKA KURA YA MAONI
Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana alishauri Serikali ya Mapinduzi kuitisha kura ya maoni itakayoamua hatma ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.

Saleh Nassor Juma (Wawi-CUF) alisema kura hiyo itumike kupata maoni iwapo wananchi wa Zanzibar wanataka au hawautaki Muungano.

Saleh alikuwa anachangia makadirio ya bajeti ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Baraza la wawakilishi jana, alisema walio wengi Zanzibar wanatofautiana kuhusu suala la Muungano uliofikiwa baina ya pande hizo mbili mwaka 1964.

Alisema makubaliano ya Muungano yanainyima Zanzibar fursa ya kuongoza taasisi nyeti kama vile Idara za Polisi, Usalama wa Taifa, Jeshi na Bunge.

"Mheshimiwa Spika, iitishwe kura ya maoni haraka … Zanzibar haijawahi kuongoza nafasi ya juu katika vyombo vya ulinzi na usalama," alisema.

Saleh alisema kuwa marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yameipa Zanzibar hadhi ya kuwa nchi, hivyo pia ni lazima iruhusiwe kujiunga na Jumuiya Afrika Mashariki bila kupitia mgongo wa Serikali ya Muungano.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakari Khamisi Bakari, alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali kwa sababu uliridhiwa na wabunge kutoka pande zote za Muungano.

Waziri Abubakari alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi, Omar Ali Sheha (CUF) wa Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.

Alisema kwamba mkataba wa Muungano uliridhiwa na wabunge wote kutoka Tanzania bara na Zanzibar jambo ambalo linaonyesha uhalali wake.

Alisema kwamba mkataba wa Muungano ulitakiwa kuridhiwa na Bunge na Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM) taratibu ambazo zimezingatiwa baada ya wabunge kutoka pande mbili za Muungano kuridhia mkataba huo.

Hata hivyo, alisema kwamba jambo lolote linalotumika kwa muda mrefu bila kuhojiwa uhalali wake huwa ni halali kutokana na uwepo wake.

"Muungano ni halali kwa sababu mkataba wa Muungano ulipitishwa na wabunge wakiwemo wa pande zote kwa utaratibu uliowekwa na katiba katika kupitisha mambo ya Muungano," alisema.

Aidha, alisema kwamba mambo yaliyoorodheshwa ya Muungano hivi sasa yamefikia 22 kutoka 11 na sio zaidi ya 30 kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Hata hivyo, alisema kwamba kwa mujibu wa katiba mambo ya Muungano hayawezi kuongezwa au kupunguzwa hadi ipatikane theluthi mbili ya wabunge kutoka Tanzania Zanzibar na Bara.

Awali, Sheha alitaka kujua taratibu gani za kikatiba zimezingatiwa kabla ya mambo ya Muungano kuongezwa kutoka 11 tangu kufikiwa kwa Muungano huo mwaka 1964.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa (Viti Maalum-CCM), Raya Suleiman Hamad, alisema Muungano wa Tnganyika na Zanzibar umeleta faida kubwa ikiwemo kujenga umoja wa kitaifa kwa wananchi wake "Leo Ndugu zetu wapo Tanzania Bara ukivunjika waende wapi, jambo la msingi ni kurekebisha kasoro za Muungano kwa sababu umeleta faida kubwa kwa wananchi," alisema mwakilishi huyo.

Akifunga Mjadala, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alisema Muungano umeleta faida kubwa na tayari kero mbalimbali zimepatiwa ufumbuzi kupitia Kamati ya pamoja ya kujadili kero za Muungano.

Kuhusu utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar, Balozi Iddi alisema suala hilo haliwezi kutekelezwa kabla ya kufanyika marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kuwataka Wajumbe wa Baraza hilo kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kulitafutia ufumbuzi.

CHANZO: NIPASHE
Wabunge wa ZNZ ni wanafiki.Tindu Lissu ktk kutoa hotuba yake juu ya katiba mpya na alizungumzia juu ya muundo mpya wa katiba mpya mkambeza na mkadai anaubaguzi. Yaani asubuhii ndio mnakumbuka blanketi!!! Sasa Leo mnadai nini.
Haya hivyo binafsi ninawasiwasi na hii katiba mpya. Bila kuujadili Muungano hii katiba haitadumu na ninauhakika baada ya miaka michache baada ya katiba hii mpya lazima tutakuja kugharimia tena kuiandika up ya. Hii katiba ni ya kuziba viraka na si ya kudumu
Kwa nini kusiwe na kura ya maoni ya kutaka kujua wangapi wanataka Muungano na wangapi hawautaki. Na Kama unahitajika je kuwe na serikali tatu au serikali moja. Binafsi sipendi serikali mbili ambazo mpaka sasa hivi na umri wangu huu nashindwa kuifahamu na hata kushindwa kumfafanulia rafiki yangu wa Uganda maana na umuhimu wa kuwa na serikali mbili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom