Mwakilishi CUF: Tumtambue Karume

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Mwakilishi CUF: Tumtambue Karume

na Mwandishi Wetu, Zanzibar


WAKATI sakata la Zanzibar ni nchi au la, likiwa bado halijatulia Mwakilishi wa Chama cha Wananchi (CUF -Chambani), Abass Juma Muhunzi, amekishauri chama chake kikubali kumtambua Rais wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume.

Muhunzi alisema hayo alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani katika bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi jana, baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, anayeshughulikia Fedha na Uchumi Dk. Mwinyihaji Makame, kuwasilisha bajeti hiyo.

Alisema ingawa kauli yake hiyo inaweza kuwa kitanzi chake cha kisiasa, hatasikitika, kwa vile ushirikiano huo ukipatikana utaleta heri na maendeleo kwa Wazanzibari wote.

Kauli hiyo ya Abass Juma Muhunzi, inafungua ukurasa mpya wa siasa za Zanzibar, kwani anakuwa kiongozi wa kwanza wa CUF kuwa na msimamo huo unaopingwa na chama chake.

"Mheshimiwa Spika, wako wenzangu wananiangalia kwa mshangao, kwani haya hatujayapitisha, lakini hawatanifahamu haraka na nawaomba wakubaliane na mawazo yangu ili tujenge uwanja mpya wa kukabili matatizo yetu," alisema Muhunzi.

Mwakilishi huyo ambaye ni Waziri Kivuli wa wizara hiyo, alisema endapo CUF itakubali kumtambua Dk. Amani Karume, itasaidia kutatua kero za Muungano na matatizo ya kisiasa.

"Mimi kwa niaba yangu, napendekeza mbele ya umma wa Wazanzibari kuwa wenzangu katika kambi ya upinzani wanikubalie nimuombe Kiongozi wetu wa Kambi ya Upinzani, aonane na Mheshimiwa Amani Abeid Karume, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kuzungumzia hoja ya kumwomba Rais wa Tanzania ashirikiane na Rais Karume kuunda tume kushughulikia kero za Muungano," alisema mwakilishi huyo.

Alisema kwamba hayo ni maoni yake binafsi na si msimamo wa chama chake, na kusisitiza kuwa suala hilo ni muhimu na endapo litazingatiwa, litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha Wazanzibari na kutatua kero za Muungano.

"Naamini kwa dhati kuwa kwa muda huu, Karume ndiye Rais hasa, kwa vile nchi haiwezi kukaa kipindi chote bila ya rais. Na kumtambua au kutomtambua ni mbwembwe tu za kisiasa, lakini ukisema unapigania kuwa Zanzibar ni nchi, maana yake unakubali kuwa kuna mkubwa wa nchi ambaye ndiye rais," alisema Muhunzi na kuongeza:

"Bila ya wanasiasa kujitoa mhanga tutamaliza karne katika mabaraza na mabunge, sisi tunakula na kuvaa vizuri na tutatumia vijipesa kidogo kuwarubuni wapiga kura watuongezee muda kwa kufikiri tunaleta maendeleo kumbe sivyo."

Alisema kutokana na hali halisi ya maisha ya wananchi, kuna umuhimu wa kushirikiana na serikali iliyopo madarakani ili kuyatafutia ufumbuzi matatizo yaliyopo, badala ya kuendeleza malumbano na kushutumiana, kutukanana na baadaye kubaguana.

"Mheshimiwa Spika, mbele ya umma unaonisikiliza nayasema haya huku nikijiamini kuwa ni mwanachama muanifu wa CUF na sikusudii hata kidogo kwa njia yoyote kusaliti heshima waliyonitunukia," alisema mwakilishi huyo.

Katika hatua nyingine mwakilishi huyo amewataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kumsamehe Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na kauli yake kuwa Zanzibar si nchi.

"Nachukua nafasi kuwaomba tena wenzangu na wananchi, tumsamehe Waziri Mkuu na tuyachukulie maneno yake kama changamoto ya kuifanyia kazi badala ya kuchukizwa," alisema mwakilishi huyo.

Tangu Karume alipotangzwa rasmi kuwa Rais wa Zanzibar, CUF ilitoa msimamo wa kutomtambua, kwa madai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

Hatua hiyo ya kutomtambua, ilisababisha chama hicho kukosa nafasi mbili za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wanaoteuliwa na rais kupitia nafasi 10 alizopewa kwa mujibu wa katiba.

source:
 
Mhh, huyu naye ....japo kwa hapo kaamua kuwa na independent mind ila wenzake watamuelewa kweli?

Unaweza kusikia wanampa onyo kali ,kwani hiyo ilikuwa silaha ya kuupata muafaka sasa yeye akishawishi wenzake wamtambue muafaka utafikiwa tena?
 
Sasa si ndio anavyotaka Karume atambuliwe ,wanamtambua ikiwa umebaki mwaka mmoja sikifikiri kama Karume atakubali kutambuliwa ,labda huku kunamaanisha matatizo yaliotokea ya Zanzibar ni Nchi au si Nchi ,hivyo wameamua kuungana . Ngoja tusubiri taarifa rasmi ya Chama ,ila huyu amesharuka na kusema hayo hayahusiani na chama wala wananchi waliomchagua ,ni yake mwenyewe.
 
HATA KATIKA NYUMBU..... WAJANJA NA MAJASIRI WAPO......!
THIS IS CUF's "CHACHA WANGWE"
 
HATA KATIKA NYUMBU..... WAJANJA NA MAJASIRI WAPO......!
THIS IS CUF's "CHACHA WANGWE"
Hapana huyo anaplay political game ,wenyewe wanamwita Nge au Tandu anatafuna huku anapuliza hapo inaonekana yupo katika tendo la kupuliza kabla hajatafuna,subiri tuone move hiyo aliyochukua ,kuna Chess inachezwa baina ya Karume na CUF.
 
Wananchi wa kawaida hapo Zenj wote wanamtambua Prez Dk. A. Karume..... Hivyo kwa Mwakilishi huyo kutamka hayo ni mwendelezo wa ufahamu wa wananchi wa kawaida visiwani hapo...
 
Taratibu wanaanza kupakana mafuta waungane wawe na Sauti moja. Siwalaumu, nawapa pongezi. Imebidi suala la Zanzibar kuwa ni Nchi au si Nchi lilete sura ya mshikamano kati ya CUF na CCM Zanzibar!

Amesema
“Mheshimiwa Spika, wako wenzangu wananiangalia kwa mshangao, kwani haya hatujayapitisha, lakini hawatanifahamu haraka na nawaomba wakubaliane na mawazo yangu ili tujenge uwanja mpya wa kukabili matatizo yetu,” alisema Muhunzi.

Mwakilishi huyo ambaye ni Waziri Kivuli wa wizara hiyo, alisema endapo CUF itakubali kumtambua Dk. Amani Karume, itasaidia kutatua kero za Muungano na matatizo ya kisiasa.

“Mimi kwa niaba yangu, napendekeza mbele ya umma wa Wazanzibari kuwa wenzangu katika kambi ya upinzani wanikubalie nimuombe Kiongozi wetu wa Kambi ya Upinzani, aonane na Mheshimiwa Amani Abeid Karume, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kuzungumzia hoja ya kumwomba Rais wa Tanzania ashirikiane na Rais Karume kuunda tume kushughulikia kero za Muungano,” alisema mwakilishi huyo.

Alisema kutokana na hali halisi ya maisha ya wananchi, kuna umuhimu wa kushirikiana na serikali iliyopo madarakani ili kuyatafutia ufumbuzi matatizo yaliyopo, badala ya kuendeleza malumbano na kushutumiana, kutukanana na baadaye kubaguana.

Akimaanisha matatizo ya Wazanzibar wote kutoka Pemba mpaka Unguaja. Hapa anamaana kuwa pamoja na matatizo ya kawaida ya uchumi, ajira na mwengine ya kijamii, tatizo kubwa kwa Zanzibar ni Muungano na nafasi yao katika Muungano. Naomba Mungu CUF wasimchukulie hatua bali waungane naye ili Zanzibar wawe na umoja.

Kukiwa na umoja Zanzibar, basi CCM ya Kikwete itabidi ikae mguu sawa na kuwanza kufanya kazi kwa manufaa ya Watanzania.

Amebainisha:
“Bila ya wanasiasa kujitoa mhanga tutamaliza karne katika mabaraza na mabunge, sisi tunakula na kuvaa vizuri na tutatumia vijipesa kidogo kuwarubuni wapiga kura watuongezee muda kwa kufikiri tunaleta maendeleo kumbe sivyo

Rushwa au Takrima ni kitu cha kawaida katika Siasa za Tanzania. Tena anakiri kuwa pesa zinatumika kurubuni, kununua kura ili wabunge na wawakilishi waendelee kuneemeka na kudanganya umma.

Tamko kama hili si la kupuuziwa hata kidogo, huyu Bwana hata kama mnamchukia kwa sababu zozote, mimi namvulia Kofia, amekuwa muungwana, mnyenyekevu na mwenye busara kuungama ukweli!

La mwisho alilofanya la kijasiri ni hili la kuwataka Wazanzibari wamsamehe Pinda na kuona tamko la Pinda kuwa ni changamoto. Hapa hata CCM Zanzibar wamepigwa goli la Kisigino!

Katika hatua nyingine mwakilishi huyo amewataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kumsamehe Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na kauli yake kuwa Zanzibar si nchi.

“Nachukua nafasi kuwaomba tena wenzangu na wananchi, tumsamehe Waziri Mkuu na tuyachukulie maneno yake kama changamoto ya kuifanyia kazi badala ya kuchukizwa,” alisema mwakilishi huyo.
 
Tunangojea kauli ya Chama Cha CUF maana,CUF hawana haraka na mtu watamwacha kwanza apambane na wapiga kura wake halafu ndio linakuja fagio ,uzuri wa CUF wanathamini demokrasia ya mtu ,ila usivuke mipaka ya kutaka wewe kutumika ili kukivuruga hapo ndio utakuwa mwisho wako ndani ya chama cha CUF ,kwa kusema tu ni demokrasia ambayo wanayo wanachama eote ndani ya CUF viongozi na wengine wapiga makofi,wanasema ni haki ya kila mtu ,ila hapa alichokisema Mhunzi kinagusa msimamo wa Chama kwa ujumla Mhunzi ametumia taaluma ya uhunzi na kukwepa kukichanganya Chama chake na kujipeleka kwenye demokrasia ya uhuru alionao kama mwananchi wa kawaida ,hivyo hapo pana vitu viwili ambavyo mhunzi ameviruka ,kwanza ameitenga kauli yake na ya Chama pili ameitenga kauli yake na wananchi waliompa kura naweza kusema amewasilisha mawazo yake ,amejitumia yeye mwenyewe kama mbunge kwa kuituma kauli yake ndani yake ,sijui kama nimefahamika.
Au kwa kuwaweka sawa wengine .labda tutumie upili ,alikuwa mwananchi wa kawaida na mawazo ambayo alitaka yawakilishwe kwenye baraza la wawakilishi ,mawazo hayo ilibidi ili yafike kwenye baraza ni lazima yapitie kwa Muwakilishi wa Jimboni kwake ,na hapo jimboni Muwakilishi ni yeye ,hivyo hoja yake kama mwananchi wa kawaida akaikabidhi kwake mwenyewe kama Muwakilishi ili ifikishwe kwenye Baraza la Wawakilishi.
Kitu kimoja ambacho naweza kusema itaonekana amekosea na kuvunja kipengee cha kuwasilisha ,kwa vile ilikuwa ni hoja au barua kutoka kambi ya Upinzani ilikuwa mkuu wao aione na hapo ndipo alipokwenda kinyume.
 
Mwiba,

Still Muhunzi kafanya kitu ambacho wote CCM Zanzibar na CUF wamekuwa wakigwaya kukifanya, nacho ni kuondoa tofauti na kunganisha nguvu kupiga vita adui yao wa maendeleo ya Zanzibar!
 
Rev. Kishoka,

Umesema umependa huyo kiongozi alivyosema tusamehe maneno ya Pinda kwamba wao sio nchi, ila wayachukulie kama changamoto. Changamoto ya nini, kutafuta nchi kwa bidii ?

(Ninavyojua mimi, mtu akikwambia, kwa mfano, wewe sio mcheza mpira mzuri , badala ya kukasarika wanasema hiyo iwe changamoto ya kufanya mazoezi zaidi. Sio ili ujenge nyumba, au utafute Uhuru. No no no. Ufanye mazoezi ili ujue mpira zaidi.)

Sasa kuambiwa wewe sio Nchi iwe changamoto, kivipi ? Kama ni ya kutafuta maendeleo ya Zanzibar, kama ambavyo imegusiwa, basi sentensi ya Nchi/Sio Nchi ambayo has got nothing to do na mambo ya maendeleo whatoever; na sioni itakupa changamoto gani zaidi ya kutafuta nchi kwa bidii. Au ni mimi ndio sielewi ?

Naomba nipe mwanga hapo.
 
Rev. Kishoka,

Umesema umependa huyo kiongozi alivyosema tusamehe maneno ya Pinda kwamba wao sio nchi, ila wayachukulie kama changamoto. Changamoto ya nini, kutafuta nchi kwa bidii ?

(Ninavyojua mimi, mtu akikwambia, kwa mfano, wewe sio mcheza mpira mzuri , badala ya kukasarika wanasema hiyo iwe changamoto ya kufanya mazoezi zaidi. Sio ili ujenge nyumba, au utafute Uhuru. No no no. Ufanye mazoezi ili ujue mpira zaidi.)

Sasa kuambiwa wewe sio Nchi iwe changamoto, kivipi ? Kama ni ya kutafuta maendeleo ya Zanzibar, kama ambavyo imegusiwa, basi sentensi ya Nchi/Sio Nchi ambayo has got nothing to do na mambo ya maendeleo whatoever; na sioni itakupa changamoto gani zaidi ya kutafuta nchi kwa bidii. Au ni mimi ndio sielewi ?

Naomba nipe mwanga hapo.

Wewe mwanazuoni mwenzangu mbona mkorofi hivi? umenielewa vema, lakini lazima uchokonoe.

Waswahili husema kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchuuzi. Wakaendelea kidole kimoja hakiui chawa, wakamaliza kusema rasilimali ya mnyonge ni umoja!

Ndiyo nashangilia umoja kati ya CUF naCCM Zanzibar kwa kuwa kuungana kwao, kutaleta ama suluhisho au marekebisho ya mengi ambayo tunasumbuka nayo.

Siasa za Tanzania kina Mrema, Mbowe, Marandu na Cheyo hawajakaa wakumbatiane, kama CCM Zanzibar ni minority katika CCM lakini wana nguvu 50% katika CCM nzima, wakiungana nguvu na Wapinzani wao CUF na kudai kwa kushinikiza Serikali ya Muungano ilete usuluhishi na mchakato wa Kweli kuhusu Muungano na Katiba, je huoni kuwa huo ndio mwanzo mpya wa kuanguka Mfalme CCM?

Nashangilia kwa kuwa Taifa litanufaika ikiwa wote CUF na CCM Zanzibar wataungana na kuwa na sauti moja! Mfumo wa muungano itabidi ubadilike na upitiwe upya pamoja na katiba kama ridhaa ya Wananchi na si ridhaa ya CCM!

Kumbuka nusu ya kura za CCM ziko Zanzibar, na kuna siye Watanganyika ambao tuko tayari kuungana na kuhakikisha kuwa kura ni 2/3!

Lakini pamoja na dhamira hiyo, wajibu wa kila uongozi wa kisiasa ni kuitumikia nchi kwa manufaa ya Taifa kwanza, jambo ambalo CCM wamelisahau, ndiyo maana kauli ya Muhunzi naiunga mkono ni kauli ya ukweli isiyo na mwegemeo wa kisiasa, ni kutaka kuwajibika kwa Wananchi na Taifa!

Tumefika hapa tulipo kwa kuwa Rafikiyo Mtalii wa dunia haweza kalisha matako chini afanye kazi, kila siku kutalii akikwepa majukumu! sasa wamshurtishe aamke. Taifalizaliwe upya!
 
Muhunzi huna Mpya. cuf Bwana. Naona wameshaanza kuwa muflis. Hii ni "spinning". Eti tena anatumwa Muhunzi kuifanya. ambaye ni mkandiaji mkubwa wa SMZ. CUF kaeni chonjo bwana. Hoja ya Mseto mmefungwa bao. Hoja ya Nchi ( si yenu- mmevamia) pia mmefungwa bao. Subirini ubaoni hadi 2010.
 
Muhunzi huna Mpya. cuf Bwana. Naona wameshaanza kuwa muflis. Hii ni "spinning". Eti tena anatumwa Muhunzi kuifanya. ambaye ni mkandiaji mkubwa wa SMZ. CUF kaeni chonjo bwana. Hoja ya Mseto mmefungwa bao. Hoja ya Nchi ( si yenu- mmevamia) pia mmefungwa bao. Subirini ubaoni hadi 2010.

Nina wasiwasi kama CCM Zanzibar watatuletea kinachotakiwa na wananchi wa Zanzibar kwani Wabia wao wa Bara hawako tayari kuona Zanzibar inapiga hatuwa ya Maendeleo na hilo ndilo linaloifanya CUF kuwa ni majaribio yaliyobakia kupata heshima ya Zanzibar. Wenyewe husema Ukosapo mafuta basi hata mate hujipaka.
 
Wananchi wa kawaida hapo Zenj wote wanamtambua Prez Dk. A. Karume..... Hivyo kwa Mwakilishi huyo kutamka hayo ni mwendelezo wa ufahamu wa wananchi wa kawaida visiwani hapo...

Wanamtambua kama mkuu wa mkoa tofauti ambayo itakusaidia huyo akiingia kwenye baraza la Mawaziri anaingia kama waziri asie kuwa na wizara maalum maana haijambo angalau angekuwa kama mgeni mualikwa Raisi wa Zanzibar lakini wameona hilo ni baya zaidi bora wamvishe lemba la ukoka eti waziri asiekuwa na wizara maalum na hiki cheo sijawahi kukisikia katika rank za mawaziri wa Muungano.
Ila polisi wasije kukusikia ukimwita Mkuu wa Mukoa utakuwa umewapa kibalua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom