Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 789
Mwakilishi CUF: Tumtambue Karume
na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WAKATI sakata la Zanzibar ni nchi au la, likiwa bado halijatulia Mwakilishi wa Chama cha Wananchi (CUF -Chambani), Abass Juma Muhunzi, amekishauri chama chake kikubali kumtambua Rais wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume.
Muhunzi alisema hayo alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani katika bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi jana, baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, anayeshughulikia Fedha na Uchumi Dk. Mwinyihaji Makame, kuwasilisha bajeti hiyo.
Alisema ingawa kauli yake hiyo inaweza kuwa kitanzi chake cha kisiasa, hatasikitika, kwa vile ushirikiano huo ukipatikana utaleta heri na maendeleo kwa Wazanzibari wote.
Kauli hiyo ya Abass Juma Muhunzi, inafungua ukurasa mpya wa siasa za Zanzibar, kwani anakuwa kiongozi wa kwanza wa CUF kuwa na msimamo huo unaopingwa na chama chake.
"Mheshimiwa Spika, wako wenzangu wananiangalia kwa mshangao, kwani haya hatujayapitisha, lakini hawatanifahamu haraka na nawaomba wakubaliane na mawazo yangu ili tujenge uwanja mpya wa kukabili matatizo yetu," alisema Muhunzi.
Mwakilishi huyo ambaye ni Waziri Kivuli wa wizara hiyo, alisema endapo CUF itakubali kumtambua Dk. Amani Karume, itasaidia kutatua kero za Muungano na matatizo ya kisiasa.
"Mimi kwa niaba yangu, napendekeza mbele ya umma wa Wazanzibari kuwa wenzangu katika kambi ya upinzani wanikubalie nimuombe Kiongozi wetu wa Kambi ya Upinzani, aonane na Mheshimiwa Amani Abeid Karume, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kuzungumzia hoja ya kumwomba Rais wa Tanzania ashirikiane na Rais Karume kuunda tume kushughulikia kero za Muungano," alisema mwakilishi huyo.
Alisema kwamba hayo ni maoni yake binafsi na si msimamo wa chama chake, na kusisitiza kuwa suala hilo ni muhimu na endapo litazingatiwa, litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha Wazanzibari na kutatua kero za Muungano.
"Naamini kwa dhati kuwa kwa muda huu, Karume ndiye Rais hasa, kwa vile nchi haiwezi kukaa kipindi chote bila ya rais. Na kumtambua au kutomtambua ni mbwembwe tu za kisiasa, lakini ukisema unapigania kuwa Zanzibar ni nchi, maana yake unakubali kuwa kuna mkubwa wa nchi ambaye ndiye rais," alisema Muhunzi na kuongeza:
"Bila ya wanasiasa kujitoa mhanga tutamaliza karne katika mabaraza na mabunge, sisi tunakula na kuvaa vizuri na tutatumia vijipesa kidogo kuwarubuni wapiga kura watuongezee muda kwa kufikiri tunaleta maendeleo kumbe sivyo."
Alisema kutokana na hali halisi ya maisha ya wananchi, kuna umuhimu wa kushirikiana na serikali iliyopo madarakani ili kuyatafutia ufumbuzi matatizo yaliyopo, badala ya kuendeleza malumbano na kushutumiana, kutukanana na baadaye kubaguana.
"Mheshimiwa Spika, mbele ya umma unaonisikiliza nayasema haya huku nikijiamini kuwa ni mwanachama muanifu wa CUF na sikusudii hata kidogo kwa njia yoyote kusaliti heshima waliyonitunukia," alisema mwakilishi huyo.
Katika hatua nyingine mwakilishi huyo amewataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kumsamehe Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na kauli yake kuwa Zanzibar si nchi.
"Nachukua nafasi kuwaomba tena wenzangu na wananchi, tumsamehe Waziri Mkuu na tuyachukulie maneno yake kama changamoto ya kuifanyia kazi badala ya kuchukizwa," alisema mwakilishi huyo.
Tangu Karume alipotangzwa rasmi kuwa Rais wa Zanzibar, CUF ilitoa msimamo wa kutomtambua, kwa madai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.
Hatua hiyo ya kutomtambua, ilisababisha chama hicho kukosa nafasi mbili za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wanaoteuliwa na rais kupitia nafasi 10 alizopewa kwa mujibu wa katiba.
source: