Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE ARUSHATaarifa nyingine zimeeleza zaidi kuwa serikali imekusudia kuihamisha barabara inayotoka mjini Arusha kwenda Babati, ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Arusha.
Vyanzo vya uhakika vimeeleza kuwa uhamishaji wa barabara hiyo utalighalimu taifa fedha ambazo idadi yake haijajulikana, lakini kukamilika kwake kutakuwa na manufaa kwa nchi.NIPASHE Jumapili ilipowasiliana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mhandisi Suleiman Said Suleiman, alipokea simu na baada ya kujulishwa hoja aliyotakiwa kuitolea ufafanuzi, alisema alikuwa kwenye mkutano.Nipo kwenye mkutano naomba unipigie baada ya half an hour (nusu saa), alisema, ingawa alipotafutwa mara kadhaa baada ya muda huo kupita, simu yake iliita bila kupokewa.
Binafsi sioni sababu ya kuihamisha barabara ya Arusha Babati kwa ajili ya upanuzi wa uwanja huo iwapo inachopanuliwa ni njia za kukimbilia ambazo haziwezi kuzuia njia za magari kwa kujenga barabara ya chini kwa magari na fly over kwa ajili ya ndege kama mataifa mengi yafanyavyo.