Mwakawago ashauri Mkutano Mkuu CCM uongezewe muda

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,082
BALOZI Daudi Mwakawago, ambaye ni mwasisi na Katibu Mtendaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) asema chama hicho kinabidi kiongeze muda wa kufanya mkutano wake mkuu ili kuweza kuwapa wajumbe muda wa kuwajua wagombea na kuweza kuwaliza maswali.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalum juzi, Balozi Mwakawago alisema inashangaza kuona wajumbe wa mkutano huo kushindwa kuuliza maswali wagombea, jambo ambalo si jema kwa demokrasia.

"Kwa jinsi mkutano huo ulivyo sasa, umeandaliwa kwa namna ambayo wajumbe hawawezi kumjua mgombea hadi azunguke mikoani, pia hata maswali wajumbe wanashindwa kuuliza. Haiwezekani wajumbe wote washindwe kuuliza hata vipengele vya elimu ambayo vilikuwa havionekani katika maelezo ya wagombea," alisema.

Alisema ni vema mkutano muhimu wa chama kama huo, wajumbe wakapewa muda ili kuwauliza wagombea maswali kama ilivyokuwa zamani.

Pia alisema katika a historia yake ya uongozi na uanachama katika chama hicho hakuwahi kuona wagombea wa nafasi ya Halmashauri Kuu (NEC) wakizunguka nchi nzima kwa ajili ya kufanya kampeni.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalum juzi, Balozi Mwakawago alisema kwamba utaratibu wa zamani wa chama hicho katika kuendesha uchaguzi ni tofauti kabisa na sasa kwani katika kipindi cha nyuma wagombea walikuwa wafanya kampeni katika mkutano na si kuzunguka mkoani kama ilivyojionyesha katika Mkutano wa chama hicho uliomalizika hivi karibuni.

"Mimi nauita utaratibu mpya kabisa, mtu anatembea nchi nzima kuomba kura za NEC, hili ni jambo jipya na ndio maana katika hutoba ya Rais Kikwete alisema hata wale ambao hawajazunguka nchi nzima nao wachaguliwe. Chama kinapaswa kuandaa utaratibu ambao utasaidia wagombea wote waweze kujulikana na kuomba kura katika kipindi cha mkutano," alisema.

Alisema jambo jingine ambalo limechangia kwa watu kuanza kuzunguka mikoani ni kutokana na wajumbe wengi kugombea nafasi ya NEC bila kuwa na historia katika chama.

"Wengi wanadhani wakishakuwa na wadhifa wa kiserikali, tayari wanaweza kugombea NEC, tufike mahali tutambue watu ambao wamekulia katika chama na ambao wanakijua chama kama ilivyo kwa Rais Kikwete," alisema.

Alishauri chama kirudishe utaratibu wake wa zamani, ambapo mkutano huo ulikuwa ukifanyika kwa wiki nzima, na wajumbe walikuwa wana nafasi ya kuwajua wagombea wenye uwezo na wale ambao hawana.

Vilevile, alipongeza hatua ya wajumbe wa CCM kuwanyima kura viongozi wa upinzani ambao wajiunga na chama hicho kutoka upinzani. " Hali hii inaonyesha kwamba wajumbe bado hawana imani na viongozi hawa kutoka upinzani, mimi nawapongeza kwa hilo," alisema.
 
Back
Top Bottom