Mwakaleli (kijiji cha Kandete) bei za mashamba zipoje ili nisipigwe?

Nimekulia huko muda mrefu na ni njia yangu. Nimeendesha pikipiki na gari miaka mingi. Unaweza kuona kwenye kipimo cha pikipiki au gari.

Ila najua watu wengi hawajui km moja ni umbali kiasi gani. Kwa vipimo vingine, km 1 ni zaidi ya futi elfu 3 kama mita 1000 zinachanganya. Ukizijua hesabu na vipimo vyake, huwa hazidanganyi.
Sidhani kama yuko sawa
 
Uthibitisho mzuri, nenda mwenyewe! Hapa tunakupa mwongozo tu. Ukitokea Mbeya 8-8 utashukia Katumba (njia panda ya kwenda Mwakaleli). Ni barabara ya vumbi lakini inapitika muda wote. Ni km 30 hadi Kandete mjini. Nauli ni elfu 4 kwa Noah na utakuta za kumwaga hapohapo Katumba
Unafikiri kwanini mahakamani wanahitaji ushahidi...kwasababu kikubwa sio uelewa bali ni uthibitisho na ndo nnachokitafuta mkuu sio vinginevyo
 
Uthibitisho mzuri, nenda mwenyewe! Hapa tunakupa mwongozo tu. Ukitokea Mbeya 8-8 utashukia Katumba (njia panda ya kwenda Mwakaleli). Ni barabara ya vumbi lakini inapitika muda wote. Ni km 30 hadi Kandete mjini. Nauli ni elfu 4 kwa Noah na utakuta za kumwaga hapohapo Katumba
Ningetaka kufanya hivo ningeshaenda kitambo tu, lakini michango ya wadau huwa ni muhimu sana...kwahiyo nahisi udhibitisho mwingine tutaupata kwa wachangiaji wengine wanaofatia
 
Rukwa, Katavi, Dodoma vijijini, Morogoro vijijini, Ruvuma vijijini, na kwengineko utakakoona wewe kunafaa. Nchi yetu bado ina mapori mengi. Lakini kama unafanya utafiti na kufuatilia sensa ya watu, maeneo yenye wakazi wengi vijijini ni uchagani, Unyakyusani na Uhayani.

Hata kama unataka mashamba ya bure utapata! Lakini sidhani kama utataka kuwa porini peke yako, maana hata wafugaji wa kimasai au kisukuma hawawi peke yao!
pole sana mkuu....sehemu ambazo hazijajaa makazi ya watu ni wapi? me ndo nakutaka huko...
 
Mwakaleli nzima hakuna mashambani, ni makazi ya watu. Rejea maelezo yangu ya awali. Pasipo na watu ni misituni tu juu ya milima ambayo ni hifadhi ya Kitulo, hifadhi ya Mlima Rungwe, hifadhi ya mlima Kyejo na hifadhi ya misitu midogo ya kienyeji (amasyeto).

Nimeandika mwanzoni kuwa kuna mashamba ya chai na miti ya kupanda. Kama husomi kwa makini ukweli huu, ni bora uende ukafanye utafiti mwenyewe!
Luteba na Matamba ndo mashambani sio?? kama ndiyo huko ndo mimi nakutaka kabisaa
 
...uthibitisho (certification or verification)... Udhibitisho ina maana tofauti (it refers to control).
Ningetaka kufanya hivo ningeshaenda kitambo tu, lakini michango ya wadau huwa ni muhimu sana...kwahiyo nahisi udhibitisho mwingine tutaupata kwa wachangiaji wengine wanaofatia
 
Hakuna mashamba makubwa kwa kuwa maeneo mengi ni mashamba ya chai na miti. Pia wakazi wengi hugawana mashamba madogo madogo (imbaka au utupaka) kiukoo au kifamilia. Ni kama ilivyo uchagani, huwezi kupata shamba kirahisi. Ekari moja haiwezi kupatikana kwa mtu mmoja labda uunganishe watu wawili au watatu. Na Kandete ni mjini, si mashambani!

Binafsi nina shamba kijiji cha jirani Lugombo linakaribia ekari moja, nauza milioni 3. Kuna maji ya bomba, umeme wa REA hapohapo shambani na barabara. Maeneo hayo hulimwa sana maparachichi na hustawi sana hata kaeneo kadogo. Pia viazi mviringo huzaa sana!

Karibu sana Mwakaleli, bonde la neema, hali ya hewa safi, watu wakarimu na wacha Mungu.
Mkuu eneo lako lipo lugombo, lipo karibu na mto mkuu?
 
Habari wakuu?

Kwa atakayekua amesoma uzi wangu wa unaouliza sehemu nzuri ya kuishi kati ya Tukuyu na Kyela atakua anajua.

Kikubwa ni kwamba sehemu niliyochagua kuishi ni Tukuyu eneo la Mwakaleli kijiji cha Kandete. Ninataka nikifika ninunue shamba dogo kwaajili ya chakula (ndizi, viazi Ulaya, mboga mboga nk) na sio kwa ajili ya kujenga. Hivo naomba msaada wa kujua bei za kununua mashamba au hata kama ni kwa kukodisha zipoje?

Sitaki shamba kubwa sana, hata nusu/robo hekali itanitosha kabisaa.
Mkuu unaenda kijijini kwetu kabisa sema kandete ni town town kwa bush labda maeneo ya pembeni ila kule tuna tabia ya kupeana mashamba kifamilia sana ila be careful japo sie ni wakarimu sana ila wenye tamaa hawakosekani
 
Asante kwa kunirekebisha umenisaidia kuchukua tuzo ya BAKITA, na tuzo mbalimbali ikiwemo kufundisha somo la KISWAHILI nje ya nchi, Asante sana mkuu.
 
Kwa kukusaidia tu, haujawahi kuwepo ubunge wa Tukuyu! Bahati mbaya hujui unawasiliana na nani na mwenye hadhi gani. Ila nimetambua upeo wako kwa sehemu kutokana na majibu yako. Nahitimisha kwa kukutakia kila la heri
Bahati nzuri sihitaji kujua nnaowasiliana nao na ndo maana wengi humu Jamiiforum ni anonymous, shida yangu ni kupata jibu/mrejesho wa swali langu na asante kwa kuonyesha wazi kuwa wewe si mtu sahihi wa kufanya hivo. Hata hilo suala la ubunge wadau washanielekeze PM kitambo tu.
Et hadhiiii hahahahaha man your so desperate......who do you think gives a fck about who you are...
 
Bado nitaheshimu sana utu wako pasipo kukudharau au kuingia mtego wako wa matusi. Naomba Mungu akupe moyo uliopondeka na kuheshimu wengine ndipo nawe utaheshimika zaidi. Kwanza nilikuwa naandika ili kuitangaza Mwakaleli maana wengi wanasoma humu. Si kukujibu wewe tu!

Pia najua sana kwamba bandiko lako si mara ya kwanza. Kwa aliye makini asingeuliza tena. Naamini kuna siku utakomaa kiutu na kiakili na kisha kuacha kukebehi au kumdharau mtu yeyote, hata wa chini yako. Pokea baraka na ufanikiwe katika unachotafuta kwa staha.
Bahati nzuri sihitaji kujua nnaowasiliana nao na ndo maana wengi humu Jamiiforum ni anonymous, shida yangu ni kupata jibu/mrejesho wa swali langu na asante kwa kuonyesha wazi kuwa wewe si mtu sahihi wa kufanya hivo. Hata hilo suala la ubunge wadau washanielekeze PM kitambo tu.
Et hadhiiii hahahahaha man your so desperate......who do you think gives a fck about who you are...
 
Back
Top Bottom