Mwakalebela aiteka kampeni ya JK Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakalebela aiteka kampeni ya JK Iringa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mlachake, Sep 22, 2010.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,786
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Fidelis butahe, Iringa

  ALIYEKUWA mshindi katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fredrick Mwakalebela jana alikuwa kivutio na kufunika mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Jakaya Kikwete baada ya kutakiwa kupanda jukwaani.

  Katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Samora mjini hapa, wananchi walililipuka kwa shangwe na vigeregere huku wakimtaja jina lake mpaka mgombea huyo alipopanda jukwaani.

  Akizungumza katika mkutano huo, Mwakalebela aliwaomba wanachama wa CCM wa Iringa Mjini kuvunja makundi, kwani anaamini kuwa bado chama hicho kina nafasi.

  "Wana Iringa kila kitu tunachokiona hapa kimeletwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wabunge na madiwani wa CCM. Napenda kuchua fursa hii kuhakikisha chama chetu kinashinda Iringa..."

  "Napenda kusema mbele ya Rais Jakaya Kikwete tukiunge mkono chama chetu, kwani tulikuwa watu 12, lakini sasa tuwe kundi moja. Natangaza kuvunja makundi, wapinzani wasitutumie kama mtaji," alisema Mwakalebela huku wananchi wakishangilia na kelele za sauti ya juu.

  Baada ya kumaliza kuzungumza na kushuka jukwaani, Mwakalebela alikumbatiana na Kikwete na kisha kushikwa mkono na mgombea huyo wa urais hadi jukwaani tena na kuonyeshwa kwa wananchi.

  "Mmemuona Mwakalebela?" alihoji Kikwete mbele ya umati wa wananchi waliofurika katika mkutano huo, wananchi walijibu 'tumemuona" huku wakiendelea kushangilia na kumkumbatia tena Mwakalebela akiwa naye jukwaani.

  Kabla ya Mwakalebela kuzungumza Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Deo Sanga 'Jah peaple' aliwaita wagombea wanne waliokuwa katika kinyanganyiro cha kura za maoni ambapo kwa nyakati tofauti walieleza kuvunja kambi zao na kuumuunga mkono mgombea alisimamishwa kwa tiketi ya chama hicho, Monica Mbega.

  Awali, mgombea ubunge katika jimbo la Iringa Mjini, Monica Mbega, aliwaomba wananchi kuwachagua wagombea wa CCM, kwani chama hicho kimeweza kutekeleza sehemu kubwa ya ahadi walizozitoa miaka mitano iliyopita.

  Mgombea huyo alipoitwa jukwaani na Kikwete hakushangiliwa kama ilivyokuwa kwa Mwakalebela na hata alipoanza kuzungumza baadhi ya watu katika uwanja huo walianza kuondoka.

  Mwakalebela ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) alishinda nafasi ya kugombea ubunge Iringa Mjini kwa kupata kura 3,897 dhidi ya Mbunge aliyepita, Monica Mbega aliyepata kura 2,989 katika matokeo ya kura za maoni CCM.

  Mwakalebela alitumia dakika tatu kuzungumza na wananchi waliofurika katika uwanja huo huku sauti yake ikisikika kwa shida kutokana na shangwe na kelele kutoka kwa wananchi hao.

  Akizungumza na wananchi uwanjani hao Kikwete alisema hospitali ya mkoa huo itaboreshwa pamoja na kujenga maabara.

  "Hospitali ya mkoa iendelee kuwa ya mkoa, ya wilaya itajengwa na kuongezwa kwa vituo vya afya ili watu wasijazane katika hospitali hizi" alisema Kikwete.

  Akijinadi kutetea kiti chake katika Jimbo la Kalenga, Rais Kikwete aliwataka wanawake nchini kutokuwa na hofu na kwamba katika serikali ijayo ya miaka mitano itaendelea kuwapa kipaumbele katika nafasi za uongozi mbalimbali
  SOURCE: MWANANCH
   
 2. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,718
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Siasa za kinafiki CCM ndo penyewe....
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 10,617
  Likes Received: 1,919
  Trophy Points: 280
  haya acha waendelee kuwasomba wanafunzi mashuleni kuudhuria mikutano yao huku utafiti ukionesha wanafunzi haohao kufelu kwa 50%.........kikwete anadhambi
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180
  Mwakalebela hana jinsi ya kufanya zaidi ya kujipendekeza kupita kiasi ili kuweka mazingira ya yeye kukumbukwa kwenye ufalme wa Kikwete!(its just like he is undressing and bowing)!huh!.............Kwa hali hiyo he might be considered!
   
 5. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,415
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  CCM ni chama cha wanafiki hata ungekuwa wewe ndio Mwakalebela ungefanya hivyo hivyo ili hiyo kesi iliyopo mahakamani ifutwe!! Sasa ngojea huyo mzee wa kikikuyu wa huko Mufindi nae atafanya hivyo hivyo ili kujipendekeza!! Jamaa hawa hawajui maana ya binadamu kuwa na hadhi yake; Shellukindo alionyesha intergrity yake kule Bumbulu kwa kutokubaliana na huu ushenzi!! Hata hivyo nadhani hawa wanyalukolo wamemchuuza tu huyu mkwere come october hawamchagui huyo Monica mbega kwani hana jipya na wamemchoka!!
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Atakuwa ameaahidiwa Ukuu wa Wilaya na yeye
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hizi siasa za Tanzania nisiseme Tanzania ngoja niseme Africa maana we are almost practicing the same thing, Na ilikuwa lazima JKamuite Mwakalebela kwa kuwa inaonyesha kabisa huyu jamaa alifanyiwa mizengwe lakini ukiangalia kwa ndani zaidi wanajitahidi kumpoza jamaa inawezekana huko mbeleni akapata cheo fulani
   
 8. e

  ejogo JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu Mwakalebela pole sana, maana inaonekana unakubalika kwa wananchi kuliko huyo waliyempitisha. Nadhani watakupoza kwa madaraka fulani
   
 9. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,786
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Nilifurahi sana coz Wananchi wa iringa walimdhibitishia JK uzuzu wa akina Makamba and Co. kwa kumtema mwakalebela.
   
 10. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,786
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Unaambiwa hata Orijinal Komedi hawakushangiliwa kama ilivyokua kwa Mwakalebela.
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Mwakalebela alipigwa bit asipomsupport Mama Mbega basi na Kesi yake na PCCB haita isha,sasa afanyeje jamani?
  Kijana ikabidi atii amri vinginevyo kesi ingeendelea.
  Ila kazi anayo Mama Mbega manake hana mvuto na hakuna cha maana alichofanya
   
 12. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,786
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Mkuu Katika pita pita zangu zote. sijawahi kusikia sehemu/kijiwe chochote aanapopewa support mama Mbega.
  Jana mama Mbega aliingia katika hoteli moja hapa Iringa wananchi walimzomea sana. Then gari ya Mgombea wa Chadema akipaki Nje ya hiyo hoteli na Kuporomosha Kampeni.
   
 13. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,229
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ni kweli kabisa mkuu...! bila kesi jamaa angekuwa amevaa kombati za ukombozi..i mean za CHADEMA
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 8,833
  Likes Received: 1,982
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna wilaya ngapi Tanzania?? Maana kina kukicha nasikia mtu kaahidiwa u-DC!!!
   
 15. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,068
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  call a spade a spade. Kwani vikao vya kumtema mwakalebela viliongozwa na nani? Na anayewanadi akina mrammba na lowassa ni nani?
   
 16. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,786
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Mwakalebela aliposhuka Jukwaani. wananchi walianza kusambaa. Kikwete wakati anaongea watu wanasukumana getini kutoka nje. what a shame!!!
   
 17. Kidege

  Kidege Member

  #17
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 18, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mpiganaji hakutakiwa kuogopa kesi. Leo hii angekuwa Chadema, kesi angeshinda na Ubunge angepata. Amewaangusha sana wana-Iringa.
   
 18. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mwakalebela katika si-hasa
   
 19. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watatengeneza wilaya za kufikirika kama majimbo ya Vatikani
   
 20. V

  Vaticano Member

  #20
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyeshangiliwa ni mwanachama wa CCM. Kashangiliwa kwenye mkutano wa kampeni ya mgombea wa CCM. Nyie kelele kama wendawazimu za nini?
   
Loading...