Mwaka unaisha! Ni mambo gani yamekufanya uchelewe kuoa au kuolewa kutokana na umri wako?

Mao ze dong

JF-Expert Member
Aug 28, 2012
941
1,006
Mimi binafsi ni kijana wa miaka 27 na mwakani ningependa kuoa ili pia kuwa na watoto mapema tatizo ni huyo wakuoa ni changamoto.

Baadhi ya vijana wakileo tunapitia mambo mengi yanayotufanya tuchelewe kuoa mfano kwangu.

1. Unakutana na mwanamke msomi ana kazi na kipato na mzur pia, mna date kama mwaka badae unapotaka kufanya taratibu za kuoa nayeye kashabadilika dharau kibao, majibu ya ovyo ata usaliti pia. Unaamua kupiga chini.

2. Unapata ambaye Hana kazi wala elimu Ila tatizo ni mdangaji sana ukilinganisha na uhalisia wa kipato chako, anapenda starehe sana unaamua kupiga chini au wewe anaamua kukupiga chini.

3. Anakuja anayekupenda kwa dhati ila unakuta hujampenda kiasi cha kumfanya mke wa maisha yako. Mwingine unatokea na wewe kumpenda ila tatizo hana akili ya maisha, ukimfungulia biashara yyte inakufa hapendi kazi au hawez kiufupi, unaamua kupiga chini.

Inafika mahali nakua na uamuzi wakutafta mwanamke nimzalishe nilee watoto tu kila mtu akae kivyake . hii wenzetu wazungu wanafanya tena kwa makubaliano .

Wengibne unakuta ni kuchelewa kusoma, kuwa katika extended family na unategemewa wewe, uchumi, malengo n.k

Je wewe ni changamoto gani inakufanya kuchelewa kuoa au kuolewa na kua na familia yako mapema.

N:b
Watu wa miaka 27 hadi 40 ambao hawajaoa wala kuolewa wakitoa changamoto zao itapendeza.

Waliooa mtupe pia ushauri kwajili ya kusaidia wengi. Nini kilikufanya uchukue maamuzi ya kuoa au kuolewa na uliyenae?

Asanteni wakuu nawasilisha
 
Mimi nilitaka kuoa tangu mwezi September Ila kutokana na changa moto za kupunguza wafanyakazi ilifanya nisogeze mbele zaidi Ila nashukuru nilipata kibarua kingine na mwakani mwezi wa 6, 2019 natarajia kufunga ndoa. Na hata ikitokea nikatemwa tena kazini siwezi kuahirisha kuoa tena tafanya hata biashara na maisha yataendelea huku nikitafuta kazi taratibu, nacho shukuru mtu wangu anajua biashara za mtaji mdogo na anaweza kusimamia biashara zangu.
 
Unayemtaka kumuoa hakupi heshima wala kukujali na usiempenda kutoka moyoni ndiye anayekusumbua hii nayo ni changamoto, usipokuwa makini, utamchukua huyo anakusumbua mradi tu uoe halafu baada ya muda umchoke na kumuanzishia vitimbi baada ya kuoana yule mpendaye ameanza kujileta...bora usioe kuliko kuoa usiyempenda ili mradi uitwe baba fulani maana ndoa sio kuitwa baba tu maana upendo wa dhati ndio kitu muhimu katika kuoa yule utayeishi naye milele.
 
Mimi hata sijui nakoseaga wapi.
Sipatagi mtu serious kabisa unakuta inafika mahali unaona kabisa hapa tunapotezeana tu muda mana hakuna uelekeo.
Mtu unakuwa unafanya mahusiano serious kumbe mwenzio anakuchora tu hana mpango.
Nawaonea wivu wenye ndoa zao Ila tu wale wenye ndoa zenye amani na maelewano.
Huwa najifariji pia kuwa bora kuchelewa ukapata mtu sahihi kuliko kuwahi ukaambulia koroma.
Ila haya maisha hayana formula kabisa.
Anyway Mungu yupo.
 
Mimi hata sijui nakoseaga wapi.
Sipatagi mtu serious kabisa unakuta inafika mahali unaona kabisa hapa tunapotezeana tu muda mana hakuna uelekeo.
Mtu unakuwa unafanya mahusiano serious kumbe mwenzio anakuchora tu hana mpango.
Nawaonea wivu wenye ndoa zao Ila tu wale wenye ndoa zenye amani na maelewano.
Huwa najifariji pia kuwa bora kuchelewa ukapata mtu sahihi kuliko kuwahi ukaambulia koroma.
Ila haya maisha hayana formula kabisa.
Anyway Mungu yupo.





Pole mrembo ipo siku yako.
 
Kwa position nliyopo kwenye maisha ingekuwa kijana mwingine angeshaoa ila kinachoninyima mm kuoa, ni kuwa karibia kila mdada ninaemtongoza ananiomba pesa..hata kabla sijala papuchi..sasa nawa-disqualify kwa kuona wapo kimaslahi zaidi..
 
Kwa position nliyopo kwenye maisha ingekuwa kijana mwingine angeshaoa ila kinachoninyima mm kuoa, ni kuwa karibia kila mdada ninaemtongoza ananiomba pesa..hata kabla sijala papuchi..sasa nawa-disqualify kwa kuona wapo kimaslahi zaidi..





Mmh
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom