Mwaka ndo unaisha hivyo; vipi kuhusu mtaala wa elimu mbona hatuelewi?

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,070
2,000
Salaam

Tumejadiliana kwenye magroup ya WhatsApp tukalifikisha kwa waratibu na maafisa wa elimu kisha tukalifikisha hadi kwa wadhibiti ubora wa elimu (wakaguzi wa shule) lakini kote huko ngoma draw

Sasa nalifikisha na humu kuona namna gani serikali imejipanga kuondoa utata huu

Swala lenyewe ni juu ya mtaala wa elimu na maboresho yake ambapo unatupa wakati mgumu sisi walimu. Ninafafanua utata huo kwa namna fulani hapa chini

Tuliambiwa mfumo mpya wa elimu ni kwamba wanafunzi wangeishia darasa la sita kuanzia mwaka huu 2020 (kwahiyo tukajiandaa kupokea mitihani ya namna mbili ya taifa) lakini mpaka juzi mtihani umeletwa mmoja tu wa darasa la saba

Hiyo imetokana na mwendelezo wa matokeo ya kauli ya waziri mwenye dhamana kutamka kwamba hakuna mfumo/mtaala mpya kila kitu ni kilekile cha zamani labda mwalimu aamue kujichanganya mwenyewe tu

Huku tukiamini kwamba kila kitu ni kama ilivyokuwa zamani lakini shuleni kumeletwa vitabu vipya (vya huo mtaala mpya) na ndivyo vinavyotumika tangu 2019

Vitabu hivyo mwisho ni darasa la sita ambapo kama hawa waliopo darasa la sita wakiachwa kuingia la saba itabidi kurudi kwenye vilevile vitabu vya zamani

Vitabu vipya (vya mtaala mpya) vimemaliza maudhui yote ya elimu msingi mpaka kufikia darasa la sita kitu ambacho wakiendelea la saba itakuwa ni marudio na mvurugano wa mambo (mf.usomaji wa Jiografia, Stadi za Kazi, Historia, Maarifa ya Jamii na Uraia)

Tena, Hivyo vitabu vipya vyenyewe kuna ambavyo vimeingia mwaka huu mwezi wa saba. Yaani tangu vianze kutolewa kuna baadhi yake vilichelewa sana kiasi kwamba wanafunzi hasa hawa wa madarasa ya tano na sita walikuwa wakisoma kwa muundo 'wa zamani' mpaka vitabu vilipokuja ndo wakahama (hatahivyo, baadhi ya miongozo ya masomo na vitabu vya mwalimu kwa baadhi ya masomo imebaki stori)

Sasa mwaka unakaribia kupinduka na tumeshashuhudia drs la sabaa wamehitimu na la sita wamebaki lakini vitabu hawana vya mwakani

Cha ajabu jambo hili linatokea wadau wa elimu kimyaa sijui tatizo ni nini. Wagombea wetu (wote) sijasikia hata mmoja akilizungumzia hili au limeonekana siyo tatizo?

Wasalaam

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,070
2,000
Hapana... uchaguzi hauingilii maswala ya elimu labda kwa siku ile ya uchaguzi tu kitu ambacho sikiongelei hapa. Mimi naulizia jambo la muda mrefu kabla yake lilikwepo na hata baada ya uchaguzi litaendelea kuwepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom