Mwaka mpya wa kichina! WACHINA wanasherehekea mafanikio ya biashara ndani ya ardhi ya wenyeji!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka mpya wa kichina! WACHINA wanasherehekea mafanikio ya biashara ndani ya ardhi ya wenyeji!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Jan 15, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wenzetu Wachina leo walikuwa na sherehe ya kuukaribisha mwaka wao mpya pale katika viwanja vya mnazi mmoja. Hakika kulikuwa na umati mkubwa sana wa Wachina utafikiri ni watu wa asili wa nchi hii. Hawa ni washika dau wa kuinua uchumi wa nchi yao bila kujali wapo hapa kwa ajili ya kufanya kazi gani. Hawa wanafanya hadi kazi za kipatao cha chini ambazo kwetu sisi Watanzania ni sawa na aibu. Si ajabu ukamkuta mchina anasaidiana na msukuma mkokoteni kusogeza mzigo wake, mchina utamkuta anauza maua ya alfu moja moja, mchina anauza nguo za ndani na viatu vya mtumba. Mchina anauza vyungu na vikombe vya udongo, Mchina anabeba zege na kupandisha ghorofani, Mchina fundi pikipiki. Kazi zote na biashara ndogondogo sasa wanafanya Wachina. Haya yanafanyika huku sisi wenyeji tukiwashangaa. Leo wanasherehekea mwaka wao mpya ndani ya ardhi yetu kwa mafanikio makubwa. Sisi wenyeji tunashindwa vipi kuiga mfano wa watu hawa? Ni wavivu, au nini kinachotusumbua? Nasi tusafiri sasa kwenda China ili tukafanye kama wanavyofanya wenzetu kwa maslahi ya uchumi wa nchi yetu, ili siku moja nasi tusherehekee matunda ya mafanikio katika mwaka mpya kwa kulipua fataki hewani katika jiji la Shanghai au Beijing. Ili nao siku hiyo waulizane hayo ni mabomu? Au la!
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Watz hatujui kutumia fursa tulizonazo.Tumsubiri EL aje atusaidie
   
 3. Kiziza

  Kiziza JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbe kweli nilisikia fataki nikahisi,ina maana mwaka wao hauanzii saa sita.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kila kitu kivyao siyo
   
 5. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndio wanawamaliza na piki piki zao zitaongeza vilema hadi mkose nguvu kazi si mmewaruhusu bwana
   
 6. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  I nearly had a heart attack... Do they have to be so noisy? Who cares if some Chinaman wants to celebrate bloody new year? What has a Chinese new year got to do with us?
   
 7. s

  sanjo JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Acha washerehekee mwaka mpya wao. Wachina wanakimbia kwa haraka katika maendeleo kwa sababu ya vitu vifuatavyo:
  (1) wanafanya kazi kwa juhudi sana na kuheshimu kazi hata kama ni kufagia barabara, kusimamia choo cha jumuia n.k.
  (2) Serikali yao haina uvumilivu kwa wala rushwa, wavunja sheria na wahalifu mbalimbali.
  (3) Serikali yao ina maono (vision) juu maendeleo ya watu na nchi katika nyanja mbalimbali na mikakati ya kufanikisha hayo malengo ipo na inafuatiliwa (monitored and reviewed) kila wakati.
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wanapenda maendeleo wa China...
   
 9. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Kitu kimoja sikukipenda katika tukio hilo. Wakati wakipiga mafataki yao walikuwa wakipiga ule wimbo wa
  Jambo! Jambo bwana, Habari gani? Nzuri sana! Na ilipofika sehemu ya nchi wanaweka! Kenya yetu, hakuna matata! Hivi kweli hii si ni kuidhalilisha nchi yetu Tanzania? Na bado TBC nao wakaendelea na kurusha wimbo huo bila hata kushtuka! Kweli tumenunuliwa mpaka nchi yetu wenyewe!!
   
 10. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Wimbo si umepigwa na Wakenya kwa ajili ya kuisifu Kenya? Ulitaka wapige wimbo upi wa TZ? Jamani kulalamika bila solution zozote sasa kunatia kinyaa. For once leteni thread ambazo ni positive. Hata ukienda kwenye forum za uchumi, teknolojia, elimu, n.k. unakuta ni lawama tu. Thread zinzochangamkiwa sana ni siasa, ngono, utani, n.k. How can you call yourself a great thinker when you are always reacting to what others are saying/thinking instead of originating yours? Boring.
   
 11. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #11
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Alichosema Kaduguda hapo ni kuhusu Wachina kuisifia kenya ilihali wanafanya shughuli zao katika ardhi ya Tanzania. Kuhusu nyimbo mbona zipo, mfano wimbo 'Jambo' ulipogigwa na Vada Hats. 'jambo, habari gani! nzuri, salama Tanzania! Tanzania! Mbona ulikuwa unafaa sana.
   
 12. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hao wanaongea kiswahili . ni vzr kuwaelewesha tu ili matukio mengine wajirekebishe,
   
 13. zagalo

  zagalo Senior Member

  #13
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  mwaka wenyewe utakua feki
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  New China year wanasheherekea dunia nzima, sio Tanzania tu, Uingereza, Marekani, Ujerumani, Ufaransa. Ugiriki..na leo kwao hakuna kazi mpaka wiki mbili zipite
   
Loading...