scholarsway
Member
- Jul 18, 2013
- 25
- 2
Matukio ni mengi yaliyoitikisa Tanzania, lakini hili la mawaziri wanne kungoka limefunga mwaka vibaya,
WALIONG'OKA
- Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.
- Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
- Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
- Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo.
WANAOKALIA KUTI KAVU:
Aidha, kufuatia sekeseke hilo, vyanzo mbalimbali vya habari za ndani vimesema kuwa, mawaziri wanaotajwa kukalia kuti kavu katika nafasi zao ni pamoja na
- Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe
- Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Jumanne Kawambwa
- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Abdulkadil Ghasia
- Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi, Dk. William Mgimwa
WANAOTAJWA KUINGIA:
Habari zinadai kuwa katika fumuafumua inayotarajiwa kufanyika ndani ya baraza hilo, baadhi ya wabunge na manaibu waziri wanatajwa kuingia kwenye baraza hilo.
- Dk. Asha-Rose Mitengeti Migiro (Mb kuteuliwa) kuwa waziri
- Mh. Januari Makamba (naibu waziri wa sayansi, teknolojia na elimu ya juu) kuwa waziri kamili,
- Mh. Mwiguru Nchemba (Mb) kuwa waziri,
- Mh. Peter Serukamba (Mb) kuwa waziri,
- Mh. Faustine Ndungulile (Mb) kuwa waziri
- Mh. Jenister Joachim Mhagama (Mb) kuwa waziri.
Je kutakua na mabadiliko katika maendeleo ya nchi hii 2014 au yale yale.....