Mwaka mpya mawaziri wapya hawa hapa, kutangazwa hivi karibuni

Nyie wote mnajisumbua huyu mkweree atawapiga chenga na utabili wenu kama alivyowapiga chenga alipomteua Mangu kuwa IGP!!! Huwa hapendi mambo yake yakivuja na ndio maana wale ambao ni maadui wa Andengenye ilibidi wavujishe jina lake ili akose kuwa IGP!!! Chezea fitina za bongo .
 
Matukio ni mengi yaliyoitikisa Tanzania, lakini hili la mawaziri wanne kung’oka limefunga mwaka vibaya,

WALIONG'OKA

  1. Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.
  2. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
  3. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
  4. Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo.

WANAOKALIA KUTI KAVU:
Aidha, kufuatia sekeseke hilo, vyanzo mbalimbali vya habari za ndani vimesema kuwa, mawaziri wanaotajwa kukalia kuti kavu katika nafasi zao ni pamoja na

  1. Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe
  2. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Jumanne Kawambwa
  3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Abdulkadil Ghasia
  4. Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi, Dk. William Mgimwa

WANAOTAJWA KUINGIA
:
Habari zinadai kuwa katika fumuafumua inayotarajiwa kufanyika ndani ya baraza hilo, baadhi ya wabunge na manaibu waziri wanatajwa kuingia kwenye baraza hilo.
  1. Dk. Asha-Rose Mitengeti Migiro (Mb kuteuliwa) kuwa waziri
  2. Mh. Januari Makamba (naibu waziri wa sayansi, teknolojia na elimu ya juu) kuwa waziri kamili,
  3. Mh. Mwiguru Nchemba (Mb) kuwa waziri,
  4. Mh. Peter Serukamba (Mb) kuwa waziri,
  5. Mh. Faustine Ndungulile (Mb) kuwa waziri
  6. Mh. Jenister Joachim Mhagama (Mb) kuwa waziri.
View attachment 129634

Je kutakua na mabadiliko katika maendeleo ya nchi hii 2014 au yale yale.....

FISADI January Makamba yeye anautaka urais uwaziri wa nini
 
Mwiguli Nchemba kuwa rais???kweli serikali haipo makini hata kidogo

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
usishangai nchemba kuwa wazir,kwan serikalin tunapeana uongoz kulipana fadhila na nchemba kaifanyia nyinyiem makubwa.
 
Wote mizigo, labda tuombe Mungu 2015 tuutoe madarakani mfumo uliopo wa chama cha mizigo! Hapo tunabadiri chupa tu ila pombe ni ileile!
 
Matukio ni mengi yaliyoitikisa Tanzania, lakini hili la mawaziri wanne kung’oka limefunga mwaka vibaya,

WALIONG'OKA

  1. Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.
  2. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
  3. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
  4. Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo.

WANAOKALIA KUTI KAVU:
Aidha, kufuatia sekeseke hilo, vyanzo mbalimbali vya habari za ndani vimesema kuwa, mawaziri wanaotajwa kukalia kuti kavu katika nafasi zao ni pamoja na

  1. Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe
  2. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Jumanne Kawambwa
  3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Abdulkadil Ghasia
  4. Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi, Dk. William Mgimwa

WANAOTAJWA KUINGIA
:
Habari zinadai kuwa katika fumuafumua inayotarajiwa kufanyika ndani ya baraza hilo, baadhi ya wabunge na manaibu waziri wanatajwa kuingia kwenye baraza hilo.
  1. Dk. Asha-Rose Mitengeti Migiro (Mb kuteuliwa) kuwa waziri
  2. Mh. Januari Makamba (naibu waziri wa sayansi, teknolojia na elimu ya juu) kuwa waziri kamili,
  3. Mh. Mwiguru Nchemba (Mb) kuwa waziri,
  4. Mh. Peter Serukamba (Mb) kuwa waziri,
  5. Mh. Faustine Ndungulile (Mb) kuwa waziri
  6. Mh. Jenister Joachim Mhagama (Mb) kuwa waziri.
View attachment 129634

Je kutakua na mabadiliko katika maendeleo ya nchi hii 2014 au yale yale.....

bila kubadili system Tanzania yetu itabaki ile ile hata waziri mkuu atoke mbinguni!
 
Umenikumbusha wimbo fulani tukiwa primary wakati wa mpira wa miguu, timu pinzani wakifanya mabadiliko tunaimba "ametoka babu anaingia bibi". .
 
hapo solution ni edward ngoyai lowasa apewe tamisemi kidogo sisim watajikongoja vinginevyo tuanze kusema bwana alitoa na bwana alitwaa.
 
January apandishwe kwa kipi alichofanya au kwasababu ya umaarufu ambao unaweza kupatikana kwa njia nyingi mbaya na nzuri, ina maana Diomond maarufu na anapendwa akigombea ubunge akipata atakua na haki ya kuwa waziri kwa umaarufu wake, tunataka watu wenye uwezo wa kuiwakilisha nchi ndani na nje ya nchi.
 
usishangai nchemba kuwa wazir,kwan serikalin tunapeana uongoz kulipana fadhila na nchemba kaifanyia nyinyiem makubwa.

Duuuu!!!!yaani huyu jamaaa ana roho ya kishetani, hana utu hata kidogo.
 
Back
Top Bottom