Grahams
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 11,094
- 34,173
Salaam,
Mwaka 2020 umeisha na sasa tumeanza Mwaka Mpya 2021. Wengi mtakuwa mlijiwekea malengo mbalimbali yawe makubwa, ya kati au madogo kwa mwaka uliopita, lakini kwa sababu mbalimbali kuna mliofanikiwa kuyatimiza na wengine mkashindwa kuyatimiza. Sizungumzii kuhusu malengo ya kuoa au kuolewa kwani binafsi nahisi ni kama malengo ya kijamii zaidi kwani ili kuyafanikisha unahitaji Support ya Ndugu na Jamaa.
Kufanikiwa kutimiza malengo yako au kushindwa kuyatimiza malengo yako, hakukufanyi ushindwe kujiwekea malengo Mapya mwaka huu wa 2021. Muda wa kujiwekea malengo ni sasa, kwa kuwa ndiyo kwanza Januari 2021.
Binafsi Mwaka huu 2021 nimejiwekea malengo yafuatayo;-
Ili kutimiza malengo yeyote uliyojiwekea ni muhimu kuwaza kuhusu rasilimali fedha itakayohitajika, Binafsi nategemea vyanzo vifuatavyo kutumika kupata fedha kwa ajili ya kutimiza malengo yangu. Vyanzo hivyo ni;-
Swali ni Je, Umejiwekea Malengo gani Mwaka huu 2021?

- Kukamilisha Ujenzi wa apartment mbili kwa ajili ya kupangisha
- Kuanza Ujenzi wa Lodge ya vyumba 12
- Kuanzisha shamba la ekari 50 za Korosho
- Kufungua mgodi mdogo wa Dhahabu na kuanza uchimbaji
- Kununua gari la kutembelea
- Kuhakikisha malipo ya ada ya Mwaka kwa Watoto inalipwa.
Ili kutimiza malengo yeyote uliyojiwekea ni muhimu kuwaza kuhusu rasilimali fedha itakayohitajika, Binafsi nategemea vyanzo vifuatavyo kutumika kupata fedha kwa ajili ya kutimiza malengo yangu. Vyanzo hivyo ni;-
- Kupitia Mikopo kutoka Taasisi za Fedha
- Kupitia mapato ya biashara
- Kupitia mapato ya Kodi kutoka kwenye apartments zangu
- Kupitia Mavuno ya Shambani
- Kupitia mauzo ya gari lililopo