Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,399
- 39,548
Mhariri
Daily News; Wednesday,July 23, 2008 @20:01
JANA katika gazeti hili tuliripoti kwamba wanafunzi takribani 10,000 waliojiunga na vyuo vya elimu ya juu mwaka jana walifanya udanganyifu na kujipatia mikopo ya elimu zaidi ya mara moja.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, wengi wa wanafunzi walipata mikopo hiyo kwa njia ya udanganyifu kutokana na kudahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja.
Katika mazingira ya mwaka huu ambako kuna zaidi ya wanafunzi 18,000 waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja, kuna hatari kwamba huenda kukawa na idadi kubwa ya wanafunzi wasio waaminifu ambao wanaweza kutumia fursa hiyo kuiba fedha kwa kisingizio kwamba hiyo ni mikopo.
Tuonavyo sisi, inabidi matukio haya ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kuchukua mikopo zaidi ya mara moja yachukuliwe kama makosa ya jinai ambayo yanastahili kufanyiwa kazi na vyombo ya sheria. Tusipofanya hivyo kuna hatari ya kulea kizazi ambacho hakina woga wala aibu kudokoa na kujipatia fedha za umma kwa njia za uongo na ulaghai.
Lililo baya ni kwamba uhalifu huu unafanyika wakati serikali ikiwa lawamani kila kukicha kwamba haitoi fedha za kutosha kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi watokao familia zisizo na uwezo kifedha kupata mikopo ya kuwaendeleza kielimu.
Sisi sote ni mashuhuda wa jinsi ambavyo wanafunzi katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu wanavyofanya maandamano, migomo na vurugu kwa madai ambayo kwa njia moja au nyingine yanahusiana na utoaji mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Kwamba mwaka huu kuna wanafunzi zaidi ya 18,000 waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja ni ishara kwamba upo uwezekano wa kuwapo kwa matukio mengine mengi ya udanganyifu katika uchukuaji wa mikopo. Hili tunaamini ni changamoto kwa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi kulifanyia kazi na kama tulivosema si kwa maneno matupu bali kuliweka wazi kwa waombaji kwamba atakayebainika akifanya udanganyifu atachukuliwa hatua za kisheria na ikiwezekana anyimwe fursa ya kupata mikopo hiyo.
Tunaamini kwamba bila kuchukua hatua kali kama hizo hatutatenda haki kwa walipa kodi na maelfu ya wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo ya juu kwa kukosa mikopo ambayo kumbe inatumbuliwa na wenzao wasio waaminifu.
My Take:
a. Wamechelewa mwaka mmoja nyuma. Tulipoandika na kutoa ushahidi wa majina kuwa kuna kupewa mikopo mara mbili si walituambia tunawazushia? Wakati tunafuatilia wale vijana wa Ukraine 29 ambao waliambiwa serikali haina fedh hadi wakarudishwa nyumbani leo hii ndio wameamka kuangalia?
b. Ni uongo na uonevu kuwabebesha lawama wanafunzi wakati tulionesha tatizo lilipo. Tatizo haliko kwa wanafunzi, liko kwenye Bodi ya Mikopo. Tulipiga kelele na kuonesha hilo kwa data zilizowazi wakatukebehi, kweli wanafikiri kwa vile Daily News limeandika ndiyo mambo yatakuwa tofauti?
c. Tulipotoa taarifa za wizi wa fedha hizi kwa ushirikiano na watu wa bodi ya mikopo, tukataja na majina ya mifano na TAKUKURU wakasema wanafuatilia hizo kesi zimeishia wapi?
Tukubali tu, tunalo hili, tena tumelala nalo.