Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli Madarakani umetosha kumzika Lowassa kisiasa

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Sasa nimeamini hawa watu wako tofauti sana. Tena hawalingani hata kwa chembe. Watanzania hatukufanya Makosa kumchagua Rais Magufuli na kumkataa Lowasa. Katika huu mwaka mmoja wa utawala wa Rais Magufuli, hakika nimeona dhamira njema aliyonayo kwa Watanzania. Nimeona pia mantiki ya kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

Katika Mwaka mmoja wa Rais Magufuli, mikakati imeshawekwa kwa ajili ya kujenga upya Reli ya Kati na Bomba la Mafuta kutoka Uganda. Miradi hii ikikamilika hakika Tanzania tutakuwa tunapata fedha nyingi za kigeni na hivyo kuweza kugharamia mahitaji mengi ya ndani.

Rais Magufuli pia kawaalika majirani zetu wa Rwanda, Zambia, Uganda, DRC na kaalikwa Kenya kwa lengo la kuhakikisha Wanafanya biashara na Tanzania na hivyo kutengeneza fedha lukuki.

Rais wetu pia kafanya mambo makubwa katika kubana matumizi yasiyo ya lazima. Nadiriki kusema kuwa Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli umetosha kumzika Lowasa kisiasa na sijui hata akigombea tena 2020 atakuja na sera zipi.
 
Lowassa kaonekana Ndanda!anasaka wanachama wa cuf wajiunge chadema.Ndio maana walishabikia sana mgogoro wa cuf na povu likamtoka mwenyekiti kuwa watamsaidia sefu,kumbe nia yao kuuwa cuf bara,ili chadema ipate nguvu
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Ndiyo Magu anajitahidi baadhi ya sehemu si kila sehemu. Ila wewe wala hufananii na anachosimamia Magufuli. Mdogo wako unatakiwa ukatwe.......acha chuki kwa Lowassa yeye anapanga mikakati yake Magu nayeye aendeleze harakati zake.
 
Lizaboni nahisi huwa anaona asipomtaja Lowassa ni kama atapoteza maisha vile. Yaani ni kama vile uhai wa Lizaboni uko kwa kumtaja Lowassa. Ajabu!
 
Lizaboni nahisi huwa anaona asipomtaja Lowassa ni kama atapoteza maisha vile. Yaani ni kama vile uhai wa Lizaboni uko kwa kumtaja Lowassa. Ajabu!
Duh! Ila si mbaya kwa vile kuna uhai wa kiafya na kisiasa.
 
Mnajifaragua tu lakini ukweli mnaujua wenyewe. Hebu waruhusuni wafanye kazi zao za siasa muone hali halisi ikoje....
 
Kwa sasa tunafanya kazi kwanza

Kazi ipi hasa?Ya kutukana RAIS na wafanyakazi wa serikali??Au kuporomosha uchumi na kukosa dira na muelekeo??
Au mnafanya kazi ya kujigamba hadharani..

Hashim Rungwe kamaliza kabisa nenda kamsome then utajua kama mnafanya kazi au mnajitahidi kuigiza zaidi.
 
Tunataka nchi ya viwanda tuione ifikapo mwaka 2020. La sivyo hamtaeleweka....
 
Walioko Bukoba wanajua nini Serikali imefanya juu yao ila si ninyi wa mitandaoni

Ni kweli wanajua kwani ndiyo wahanga wakubwa wa uminywaji wa haki za msingi za mtanzania.Mmekula mpaka rambi rambi za wahanga.
 
Back
Top Bottom