Mwaka mmoja wa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka mmoja wa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WATANABE, Nov 22, 2011.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Ndugu wanaJF,

  Hivi sasa ni mwaka mmoja toka CHADEMA kiwe chama kikuu cha upinzani hapa nchini. Mengi yametekelezwa yanayofurahisha watanzania wapenda mabadiliko. Kama ilivyo ada ni vyema tukajikumbusha baadhi ya mambo yaliyotekelezwa na chama chetu na wabunge wetu na tukajipima utendaji wetu katika nyanja mbali mbali.

  Naanza na machache ni imani yangu wapenda mabadiliko tutachangia kwa nia njema tukiacha ushabiki wa vyama vyetu hasa ikizingatiwa kuwa hata ukiwa mshabiki wa CCM ni muhimu sana ukatambua umuhimu wa chama kikuu cha upinzania katika mustakabari wa taifa; kwa kuwa si wapenzi wote wa chama tawala wanaonufaika na ufisadi na ufuajai wa mali unaoendelea hapa nchini. Hivyo ni dhahiri kuwa uimara wa chama kikuu cha upinzani unachangia kuondoshwa kwa umaskini kwa kasi zaidi.

  Naanza:-

  1) Uelewa wa Kanuni za Bunge kwa upande wa wabunge wetu:- Wabunge wetu, japo sio wote walionyesha wazi wazi nia na shauku ya kuzisoma, kuzielewa, kumudu na kuzitumia kanuni za bunge licha ya mapungufu yake katika kuwateta watanzania. Uongozi wa CDM lazima upongezwe kwa kuweza kuwatayarisha wabunge wageni mjengoni kuweza kumudu kuzitumia kanuni za bunge vyema. Kama ilivyo ada katika msafara wa mamba, kenge hakosekani, wapo baadhi ya wabunge ambao hatukuwaona kabisa katika kipindi hiki.

  2) Kulinda maslahi ya taifa:- Chadema na wabunge wake wameendelea kung'ara katika nyanja hii ya ulinzi wa maslahi ya taifa. Waheshimiwa Mbowe, Zitto, Tundu Lissu, Halima Mdee, Mnyika, Wenje, Msigwa, Lema n.k waling'ara sana katika nyanja hii. Ulinzi wa raslimali za taifa ndio ulikipandisha chama chati chetu hivyo viongozi na wabunge wetu hawatakiwi kupunguza kasi ya katika nyanja hii.

  Kama ilivyo ada katika msafara wa mamba kenge hawakosekani. Wapo baadhi ya wabunge wetu hatukuwasikia kabisa katika mjadala wowote wa ulinzi wa maslahi za umma ilihali mali ya umma katika nchi hii zinafujwa kwa kiwango cha kutisha, ufisadi unazidi kutalamaki n.k. Ni dhahiri kuwa nyanja hii ikiendelea kutumiwa vyema na wabunge wetu wote 45 kwa kufanya tafiti zinazohusiana na kuwasilisha matokeo ya tafiti za ufisadi na ufujaji wa mali ya umma kupitia michango na mijadala bungeni kama alivyokuwa akifanya Mhe Wilbroad Slaa wakati akiwa mbunge wa Karatu nina hakika CHADEMA ina nafasi kubwa ya kushawishi idadi kubwa ya watanzania wasiojitokeza kupiga kura wajitokeze, kujiandikisha, kupiga kura na hatimaye CDM ijizolea kura nyingi zitakazoushinda wizi wa kura wa CCM katika chaguzi zijazo.

  Lakini ikiwa idadi kubwa ya wabunge wa CDM wakiendeleza utaratibu walioingia nao bungeni mwaka 2010/11 wa kunyamazia ufujaji wa mali ya umma na ufisadi unaoendelezwa kwa nguvu sana na viongozi wa watendaji wa CCM, na viongozi wa CDM wakajikita katika mada na hoaja dhaifu kama uchaguzi wa Meya wa Arusha tuu; basi wananchi walio wengi hawataona faida ya kujitokeza kujiandikisha, kupiga kura na hatimaye kuendelea kuwapigia kura wagombea wa CDM.

  3) Kuunganisha nguvu za vyama vya upinzani:- "Wahenga walisema kidole kimoja hakiui chawa" juzi katika mjadala wa mchakato wa katiba tumeona dhahiri umoja na mshikamano vinavyoweza kutoa mchango mkubwa zaidi mara baada ya wabunge wawili wa NCCR nao kuamua kususia kikao hicho cha bunge. Laiti kama ingekuwa wabunge wote wa vyama vya upinzani wangekuwa wamesusia kikao hicho ni dhahiri kuwa hali ingekuwa tofauti. Najua hapa zipo tofauti za msingi katika vyama mbali mbali vya upinzani; lakini viongzi wa CDM lazima watazame maslahi mapana zaidi ya taifa na watambue kuwa watanzania walio wengi watakuwa tayari kupiga kura hata kupinga hiyo katiba kama inakuwepo united opposition.

  Viongozi wa CDM lazima wajihoji kama leo wanashindwa kuunganisha nguvu ya vyama vya upinzani, hata kama zipo tofauti zao za msingi kati ya vyama, watawezaje kukabiliana na changamoto na mikiki ya uongozi wa taifa lenye makundi, makabila, dini na migawanyiko ya kila aina.

  Viongozi wa CDM watambue kuwa watanzania wengi wenye busara na hekima wanawatazamia kutumia miaka mitano ya uongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuunganisha nguvu ya vyama vya upinzania badala ya kila siku kurushiana vijembe katia ya vyama vya upinzani. kwani ikumbukwe huo muafaka unaopachikwa jina la CCM B leo, ulianza hivi hivi kwa busara na hekiama za kutumia meza za majadiliano kama vile kutafuta mazunguzmo na Raisi wa nchi baada ya kuchoshwa na watu kuumizwa na kuuawa na vyombo vya dola.

  4) Mchakato wa Katiba mpya:- Katika uchaguzi mkuu wa 2010, hii ilikuwa ni ajenda ya CDM. Kitendo cha Raisi Jakaya Kikwete kupachika ajenda hii katika utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2010-2015 ni kielelezo cha kufanikiwa kwa njia CDM ilizotumia kuufikia umma wa watanzania hususan "Operesheni Sangara" n.k.

  Ukongwe na uzoefu wa CCM vilipelekea ikabaini mapema kuwa kuwa CDM imefanikiwa kuwaaminisha watazania hususan watanzania wa hali za chini (mtaji wa CCM) kuwa kupatikana kwa katiba mpya itakuwa ndio suluhisho la matatizo yaliyopo hapa nchini hivi sasa. Hivyo CCM ikapoka ajenda hiyo kutoka CDM kwa lengo la kurejesha matuamaini ya idadi kubwa ya watanzania wa hali za chini.

  Mahali CDM ilipofanya vyema katika mchakato huu-

  a) CDM na wabunge walifanya vyema kuwaongoza wabunge wengine kuchambua mapungufu ya muswada wa mchakato wa Katiba uliowasilishwa bungeni Aprili 2010 na hatimaye kuilazimsha serikali kuurejesha ukafanyiwe kazi upya.

  b) CDM na wabunge wake wamefanya vyema sana kuwakilisha maoni ya watanzania walio wengi kuhusu mapungufu yaliyopo katika muswada uliwasilisha katika bunge lililomalizika hivi karibuni hadi kufikia hatua ya kususuia vikao vyote vya kupitishwa kwa muswada huo. Angalau CDM watakuwa na cha kuwaamabia wananchi mara tu athari za upitishaji wa katiba kimabavu zitakapoanza kuonekana.


  Mahali ambapo CDM haikufanya vyema-

  a) CDM ilitakiwa kusoma alama za nyakati mapema kuhusu nia ya viongozi wa CCM hususan JK na mawaziri wake kuhusu kuwapatiwa wananchi haki ya kutoa maoni yao katika muswada wa sheria yoyote unapowasilishwa bungeni hususan muswada wa sheria ya kuunda mchakato wa marekebisho ya katiba.

  Kutokana na wananchi kutokujua maana ya kusomwa mara ya kwanza au ya pili, na CDM iliyokuwa ikitegemea nguvu za umma kushindwa kuwapatia elimu hiyo mapema; wananchi walishindwa kuunga mkono upande wowote kati ya CDM na wabunge wake au CCM na wabunge wake mara tu malumbano yalipoibuka bungeni kuhusu muswada usomwe kam mara ya kwanza halafu waanchi wakatoe maoni au usomwe kwa mara ya pili na ujadilwe na wabunge na hatiamye kuwa sheria.

  Katika harakati kama hizi zenye kuhitaji nguvu ya umma ni lazima CDM ikiri nguvu ya umma hupatikana pale tu umma uatakapokuwa umeelewa nini kinachobishaniwa au kugombewa. Na ni hapo tu unapoweza kudai kuwa nguvu ya umma ipo upande wako. Katika hili CCM walitumia uzoefu wao wa siasa kutupiga bao, baada ya kugundua kuwa tulikuwa tukitumia muda, nguvu na raslimali nyingi katika sakata la umeya wa Arusha na kusahau mambo mengine yenye umuhimu pia.

  b) Japokuwa Mhe Tundu Lissu ni mchambuzi mtafiti na mchambuzi mzuri sana. Lakini kama binadamu ana udhaifu katika Communication Skills hususan katika nyanja matamshi na body language. Japokuwa hotuba yake ilikuwa ni ya kihistoria na yake iliyosheheni "facts" kuhusu mapungufu ya sheria husika na muungano, mapungufu yaliyotajwa hapo yaliweza kutoa mwanya kwa wabunge mambumbu wa CCM kujaribu kuikosoakijuu na bila facts zozote. Nitatoa mifano michache

  Mpaka sasa ni watanzania wachache sana wakiwemo waandishi wa habari walioweze kumuelewa Mhe Tundu Lissu kuhusu nafsi ya wananchi katika mchakato wa utungwaji wa sheria hususan haki ya wadau na wananchi kutoa maoni yao mara tu baada ya muswada kusomwa kwa mara ya kwanza.

  Mpaka sasa ni watanzania wachache sana wakiwemo waaandishi wa habari waliweza kumuelewa Mhe Tundu Lissu anapokokotoa idadi ya wabunge watakaounda bunge la kutunga katiba ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo iliyopitishwa robo tatu watatoka CCM. Si watanzania wengi watakaolifurahia jambo hilo baada ya kueleweshwa kwa makini ikizingatiwa rekodi ya wabunge wa CCM bungeni kutojali na kuthamini maslahi ya umma.

  Ni vyema viongozi wa CCM wenye Communication Skills za hali ya juu kama DR Slaa, Zitto n.k wakayarejea yaliyomo katika hotuba hiyo hiyo mara kwa mara kwa lengo ya kuzamisha vichwani mwa watanganyika na wazanzibari yale yaliyokusudiwa na hotuba ile na kuondoa upotoshaji wa kuwa CDM haiwapende wazanzibari na haiipendi Zbar.

  Ushauri wangu ni kuwa kwa kuwa mpaka sasa CDM hawajatoa kauli yoyote kuhusu kukiukwa kwa Katiba au sheria yoyote kuhusu upitishwaji wa sheria hiyo ambavyo vinaweza kushughulikia na mahakama, hivyo hawajata kusudio la kupinga
  mahakamani upitishwaji uliofanywa na bunge wa sheria ya mchakato wa marekebisho ya katiba iliyopitishwa hivi karibuni . Tusipoteze muda kupinga kitu ambacho hakiwezi kupingwa kisheria.

  Badala yake CDM irekebisha makosa yake kwa kutelekeza
  "Operesheni Sangara" ambayo ingeweza kutumika kuwaelimisha watanzania nini maana ya muswada kusomwa kwa mara ya kwanza au ya pili bungeni. Hivyo "Operesheni Sangara" i
  rejeshwe haraka iwezekanavyo kwa lengo la kuwapatiwa watanzania elimu ya uraria kuhusu hoja mbali mbali za kikatiba kama vile umuhimu wa kupunguzwa kwa madaraka ya Rais ndani ya Katiba mpya na sheria mbali mbali, kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, kuundwa kwa Seikali ya Tanganyika n.k.

  Nina hakika mikutano ya aina hii itaruhusiwa na Serikali na Polisi kwa kuwa haitatumiki kupinga sheria halali iliyotungwa na bunge na badala yake itakuwa ikijihusisha na mambo ya katiba ya nchi.

  c) Kwa Chama kama CDM chenye harakati kubwa na zenye maana kubwa kwa taifa hili ni udhaifu mkubwa sana kwa CDM kutegemea hisani wa wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari kufanikisha harakati zao. Laiti kama CDM ingekuwa na vyombo vyake vya habari ni dhahiri kuwa idadi kubwa ya watanzania ingeweza kupata elimu ya nini maana ya "muswada kusomwa kwa mara ya kwanza au ya pili" kwa kasi na hivyo kuwa katika nafasi ya kuweza kupitisha maamuzi wauunge mkono upande upi.

  Ni vyema uongozi wa CDM kama kweli una malengo ya kuliondoa taifa hili hapa lilipo ukalipa uzito pendekezo hili hususan ikizingatiwa wapenda mabadiliko wapo tayari kununua hisa ili kuzalisha mtaji wa vyombo hivi. Kuendelea kupuuza wazo hili ni kukaribisha kupigwa mabao ya kisigino mengine kama tulivyopiga katika mhakato huu kwa kushindwa kuhamasisha nguvu ya umma kwa kuwa umma wenyewe hauelewi nini kiini cha mvutano.
   
 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Chadema ni sindano ndogo ishonayo mbaka makoti..imagine wabunge 48 tu watu wanajamba jamba wakiwa akina tundu 70 si wata fariki??
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Waanzishe mass media zao na pia wawe na msemaji imara wa chama
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Tunahitaji uchambuzi makini namna hii JF badala ya ushabiki wa kitoto wa vyama usio na tija!
   
 5. m

  mtolewa Senior Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hili la kuanzisha tv na radio sijui hata wameelewa umuhimu na utayari wa watz kuchangia kwa hali na mali.labda kuna strategic plan,ngoja tuone naamini cdm huwa haikurupuki.
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  kuibuliwa kwa fisadi mbali mbali serikalini. directors wa Mashirika ya umma wakimuona zitto huchanganyikiwa
   
 7. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kaka co siri uchambuzi wako umetulia sana,hongera na naamini kwa vile cdm ni chama imara na makini huo uchambuzi wataufanyia kazi.Zaidi hilo la kuwa na tv au redio ya cdm ni mhimu kwani umma utaweza kupata habari zinazokihusu in proper manner tofauti na sasa ambapo taarifa za chama zinatolewa kwa kifupi mno na mda mwingine zinapotoshwa na hizi medias za watu wa magamba, the so called TBC1
   
 8. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hoja yako nzuri.
   
 9. l

  lemberwa Member

  #9
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bomba sana
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yaani mkuu uchambuzi wako ni makini na umetulia sana sina cha kuchangia kazi Kwenu CDM kuufanyia kazi huu waraka.
   
 11. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  I salute your love to YOUR COUNTRY and YOUR PARTY - CHADEMA!
   
 12. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Well said..Asante kwa kurudisha heshima ya jf..post kama hizi ndo zimefanya jf kuheshimika..kuna kundi limetumwa kutibua hapa jf wanaandika post za kijinga ili watu watukane tu..
   
Loading...