Mwaka mmoja umetueleza mengi

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,638
Huu mwaka mmoja tokea awe madarakani umetuonyesha mengi na sasa tunaweza walau hata kuanza kuhitimisha kuwa kumbe wala hayuko tofauti kivile na wengine na huenda akawa ni bomu kabisa kuliko wote waliomtangulia.

Aliingia kwa mikwara ya kufa mtu. Akafutilia mbali sherehe za uhuru [2015] katika lengo la kuheshimu vipaumbele.

Sherehe za muungano [2016] nazo zikafutwa na pesa ambazo zingetumika kwenye hizo sherehe akaagiza ziende kwenye upanuzi wa barabara ya uwanja wa ndege wa Mwanza.

Pia akabana safari za kipuuzi puuzi za kwenda nchi za nje za watumishi wa umma.

Yote hayo pamoja na jitihada za kupambana na ufisadi yalikuwa ni nuru njema kwa wengi. Baadhi yetu tukadhani labda kweli tupo kwenye zama mpya...lakini wengine tukajipa muda maana muda huonyesha mengi.

Juzi sherehe za uhuru zikafanyika. Maajabu! Manake mwaka jana hakukuwa na sababu ya kusherehekea kwa sherehe kubwa kwa ajili ya gharama kuwa juu lakini mwaka sijui hakukuwa na hizo gharama...

Na sijui hizo za muungano nazo zitafanyika hapo mwakani baada ya kutofanyika mwaka huu?

Sasa leo yamekuja haya ya kufanyia mikutano ya CCM ikulu.

Tafadhali sana MTUKUFU rais....like....seriously? Kwa nini msifanyie hayo mamikutano yenu huko Lumumba?

Wahshi kabisa....you will go down as the worst president in the history of our existence...past...present...and future!

Mikwara yote ile kumbe hamna lolote...bora hata gesi ya CocaCola.

NB: Pia iliwahi kuripotiwa kuwa angetuonyesha pay stubs za mshahara wake. Kumbe ilikuwa ni uongo tu. Mpaka leo hamna kitu na hakuna anayejali [ukiacha mimi labda].
 
Huu mwaka mmoja tokea awe madarakani umetuonyesha na mengi na sasa tunaweza walau hata kuanza kuhitimisha kuwa kumbe wala hayuko tofauti kivile na wengine na huenda akawa ni bomu kabisa kuliko wote waliomtangulia.

Aliingia kwa mikwara ya kufa mtu. Akafutilia mbali sherehe za uhuru [2015] katika lengo la kuheshimu vipaumbele.

Sherehe za muungano [2016] nazo zikafutwa na pesa ambazo zingegharamia akaagiza ziende kwenye upanuzi wa barabara ya uwanja wa ndege wa Mwanza.

Pia akabana safari za kipuuzi puuzi za kwenda nchi za nje za watumishi wa umma.

Yote hayo pamoja na jitihada za kupambana na ufisadi yalikuwa ni nuru njema kwa wengi. Baadhi yetu tukadhani labda kweli tupo kwenye zama mpya...lakini wengine tukajipa muda maana muda huonyesha mengi.

Sasa leo yamekuja haya ya kufanyia mikutano ya CCM ikulu.

Tafadhali sana MTUKUFU rais....like....seriously? Kwa nini msifanyie hayo mamikutano yenu huko Lumumba?

Wahshi kabisa....you will go down as the worst president in the history of our existence...past...present...and future!

Mikwara yote ile kumbe hamna lolote...bora hata gesi ya CocaCola.

Mkuu we ni ngumu mtu kukuelewa upo upande gani,,,,[HASHTAG]#sigaraKali[/HASHTAG]
 
Tanzania kuna vituko!

Kwamba kufanyia mikutano Ikulu anakuwa ''the worst president in the history of our existence...past...present...and future!''

Wale Marais ambao walifungua makampuni na kupanga dili za kifisadi wakiwa Ikulu sijui kwa kiingereza tutawapa maneno yapi ya kiingereza. Mimi hao Marais ninawapa meneno ya kiingereza yanayosema, ''the best president in the history of our existence...past...present...and future''
 
Tanzania kuna vituko!

Kwamba kufanyia mikutano Ikulu anakuwa ''the worst president in the history of our existence...past...present...and future!''

Wale Marais ambao walifungua makampuni na kupanga dili za kifisadi wakiwa Ikulu sijui kwa kiingereza tutawapa maneno yapi ya kiingereza.

Mambo yenu ya ki CCM kafanyieni Lumumba huko, ebo!
 
Uchumi unaelekea shimoni, masikini wanazidi kuongezeka ilihali matajiri wanapukutika na kwenda na maji kila uchao aheri ya jana
 
Mambo yenu ya ki CCM kafanyieni Lumumba huko, ebo!
Yes,

Hawa mambo yao ya ki CHADEMA walikuwa wanatakiwa wakafanyie Ufipa.

CDM5.jpg
 
Sasa nyie mlidhani ana huruma na nchi?ile ilikua gia ya kuingilia tu na mbwembwe kibao
 
na kwa teuzi za ccm za leo,

ccm nayo imekufa,na haitafufuka.

kinana kaomba kustaafu,na atastaafu,akiondoka ccm mahututi inakuwa imekufa kabisa
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom