Mwaka mmoja tu mtaani nimeshakuwa frustrated kiasi hiki, dah!

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
1,233
1,250
Habari za Jumapili wakuu wa JF?

Bila shaka hali nzenu ni nzuri tu.

Baada ya salamu:
Kijana mwenzenu (age,25) nimehitimu rasmi masm yangu ya higher learning mwaka jana mwezi wa saba, mpaka sasa nimeshapewa cheti cha taaluma katika fani ya Logistics and Transport.
Wakuu, toka mwaka jana hiyo mwezi wa saba, nimekuwa nikizunguka jijini hapa kwa matumaini makubwa ya kupata kazi ya kufanya kulingana na fani yangu ama kupata sehemu ya kujitolea ili kuongeza EXPERIENCE katika CV yangu.

Wakuu, toka kipindi hicho nimeanza kuzungusha CV katika makampuni mbalimbali kwa lengo la kutafuta kazi, mpaka leo nimekuwa mtu wa kuhangaika tu kwenye maofisi ya makampuni mbalimbali huku nikiambulia kuambiwa hakuna kazi, mara acha CV tutakupigia simu na huku pia mikikumbana na matapeli mbalimbali kutoka ZoomTanzania(ndio maana zoomTz sina hamu nao tena)..

Wakuu:
Nina fact chache kuthibitisha harakati zangu za kutafuta na kukosa ajira, sijajua nyota yangu imelalia wapi
kwanza, nilipigiwa simu na azam mwaka jana mwezi wa kumi wakidai wanahitaji mtu wa Logistics level ya degree, nikaitika kwa moyo mmoja kuwa nik tayari, wakaniuliza, una cheti cha degree? nikawaambia bad hatujapewa ila nina academic transcripts, wakasema hapana, haiwezekani.. ''tunahitaji mwenye cheti cha academic''.. basi hiyo ikala..
....
pili; nimepata network tu ya kulazimisha mbugani humu, hapa napo naambiwa nitoe laki tano ili nipewe kazi ya 800k kwa mwezi, dah kwa kweli nilichoka, basi nikawaambia nifanye kazi mwezi mmoja kisha niwaachie laki 6, jamaa wamegoma, wanadai niwape hiyo 500k kutoka mfukoni kwangu.. basi nikawaambia pesa sina..
Wakuu mpaka sasa ninapoandika niko frustrated sana na mihangaiko ya kutafuta ajira

Naombeni sana mwenye nafasi tu katika kampuni ama anajua namna ntakavyoweza kupata nafasi ya kujishikiza anisaidie.
CV yangu ipo hapa chini, attached
my number 0764622243
 
Attachments

  • File size
    14.5 KB
    Views
    85

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
1,233
1,250
wakuu,
mimi nilishajitoa kufanya kazi kokote ndio maana nakutana sana na matapeli hapa jijini Dar es salaam japo suala la kutoa pesa nimekuwa mgumu sana. Kuna jamaa wanatoa watu Tanzania na kuwapeleka Arabuni kufanya kazi, nao hao nilishakutana nao wakadai tukafanye kazi za ulinzi kwa mshahara dola 350 kwa mwezi, charges zao wakadai niwape shilingi laki 6 ili wafanikishe kila kitu ibaki mimi tu kuondoka. Kiukweli tulikuwepo vijana wengi sana, wengi wao walikuwa wameshatoa pesa 50% na wengine....hapa nikarudi nyuma... nikabembeleza sana wanilipie gharama, wakakataa
 
optico

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
265
500
Pole ,Muombe Mungu pia jaribu kuongea na watu mbalimbali walio kwenye systems kw muda mrefu wana mawazo mazuri zaidi
 
Bill of Quantity

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
1,233
1,250
Pole sana.

Nimepitia CV yako. Kama hii ndiyo umekua ukiitembeza basi sishangai wewe kukosa kazi. Sababu kubwa ni kwamba CV yako haielezi "nini unaweza kufanya". Haielezi jambo hata moja ulilowahi kufanya na likafanikiwa. Sijui kama umenielewa.

Siku hizi waajiri wanataka kuona wewe una nini (what do you have, what can you deliver)?

Pia, kuweka "businessman/woman" kama reference person ni utani kwa mwajiri. Inashauriwa angalau mmoja awe "academic referee" na mwingine "professional referee".

Yote yakishindikana, jiajiri.
asante sana mkuu.
umenifungua macho kwa upande mwingine
 
Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
646
500
Pia kwenye kipengere cha taaluma...umeanzia chini kuja juu badala juu kuja chini....yaani mwaka ulosoma chuo ndo uwe juu kbsa na primary chimi kbsa
 
ivunya

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
1,928
2,000
Kijan pole sana kumbuka kuna watu wapo mtaan more than 2,3,4 ...... bado kukata Tamaa wapo kwenye game.kitu kingine next time usirudie tena kuweka CV kuna baadhi ya maeneo wakiona CV zimefanana munaondolewa kwenye kuomba kazi. kwenye hiyo CV hongezea mahali ulipo Fanya field na majukumu uliyotekeleza.
 
Dhwahiri

Member
Jun 20, 2016
16
45
Mimi nimepitia CV yako Ni kweli Kama wanadau wanavyoelezea haina mashiko.Fanya mabadiliko ktk kipengele cha Elimu anzaa ya juu kuja elimu ya chini.Pia ktk referee haipo vizuri Na nini unaweza kufanya kwa mfano ktk sehemu uliokuwa unafanya field elezea kazi ulizokuwa unafanya.Zaidi unaweza ukagoogle pia itakusaidia.Asante usichoke kupiga mwisho utafanikiwa.
 
Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,469
2,000
Pole sana ndugu, ila usikate tamaa ni mapema mno kwani kuna wenzako toka 2011 hadi leo bila bila.

Na ujitahidi uufanyie kazi ushauri unaopewa na wadau kwenye CV yako pia pitia sticky thread moja hapo juu inayosema "Nyaraka muhimu kwa maombi ya kazi;Barua CV/resume na rejea" utapata mwanga wa kuandaa CV vizuri kama unavyoshauliwa.
 
Mustaphagentleman

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
3,963
2,000
Habari za Jumapili wakuu wa JF?

Bila shaka hali nzenu ni nzuri tu.

Baada ya salamu:
Kijana mwenzenu (age,25) nimehitimu rasmi masm yangu ya higher learning mwaka jana mwezi wa saba, mpaka sasa nimeshapewa cheti cha taaluma katika fani ya Logistics and Transport.
Wakuu, toka mwaka jana hiyo mwezi wa saba, nimekuwa nikizunguka jijini hapa kwa matumaini makubwa ya kupata kazi ya kufanya kulingana na fani yangu ama kupata sehemu ya kujitolea ili kuongeza EXPERIENCE katika CV yangu.

Wakuu, toka kipindi hicho nimeanza kuzungusha CV katika makampuni mbalimbali kwa lengo la kutafuta kazi, mpaka leo nimekuwa mtu wa kuhangaika tu kwenye maofisi ya makampuni mbalimbali huku nikiambulia kuambiwa hakuna kazi, mara acha CV tutakupigia simu na huku pia mikikumbana na matapeli mbalimbali kutoka ZoomTanzania(ndio maana zoomTz sina hamu nao tena)..

Wakuu:
Nina fact chache kuthibitisha harakati zangu za kutafuta na kukosa ajira, sijajua nyota yangu imelalia wapi
kwanza, nilipigiwa simu na azam mwaka jana mwezi wa kumi wakidai wanahitaji mtu wa Logistics level ya degree, nikaitika kwa moyo mmoja kuwa nik tayari, wakaniuliza, una cheti cha degree? nikawaambia bad hatujapewa ila nina academic transcripts, wakasema hapana, haiwezekani.. ''tunahitaji mwenye cheti cha academic''.. basi hiyo ikala..
....
pili; nimepata network tu ya kulazimisha mbugani humu, hapa napo naambiwa nitoe laki tano ili nipewe kazi ya 800k kwa mwezi, dah kwa kweli nilichoka, basi nikawaambia nifanye kazi mwezi mmoja kisha niwaachie laki 6, jamaa wamegoma, wanadai niwape hiyo 500k kutoka mfukoni kwangu.. basi nikawaambia pesa sina..
Wakuu mpaka sasa ninapoandika niko frustrated sana na mihangaiko ya kutafuta ajira

Naombeni sana mwenye nafasi tu katika kampuni ama anajua namna ntakavyoweza kupata nafasi ya kujishikiza anisaidie.
CV yangu ipo hapa chini, attached
my number 0764622243
Kaka me nilsota sana nikaamua kuanza as a Driver nikawa nalipwa 200,000 per month huku nikiendelea CV siku moja nikaenda kwa Interview nikafanya nikapita nikaacha udereva
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom