tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Hafla ya kuwaaga wanajeshi 14 wa Tanzania waliokuwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliouawa nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imefanyika jiji Dar es Salaam mwaka mmoja uliopita tarehe waliouwawa tarhe 8 December 2017
Wanajeshi hao waliuawa baada ya kupigana na waasi kwa muda wa saa 13 kufuatia waasi hao kuishambulia kambi yao.
Sherehe hizo zimefanyika kwenye Makao Makuu ya Jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania "Ngome" Upanga jijini Dar es Salaam
Mkuu wa ulinzi wa amani wa Umoja wa mataifa Jean Piare Lacroix, alihudhuria sherehe hizo. Familia za wanajeshi hao nazo zilikuwepo na zimeungana na wapendwa wao kuelekea mikoani.
Mungu azilaze roho za marehemu wapiganaji wetu mashujaa wetu mahali pema peponi.Amen