SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,244
- 4,258
N Leo nimemaliza mwaka mmoja tangu nijiunge na JF. Nawashukuru wanaJF wote kwa maandishi yao kwenye majukwaa mbalimbali yaliyonielimisha, kuniburudisha na kunipunguzia stress za maisha.Jukwaa la JF Doctor kwa mfano, limenifundisha mengi sana, mwalimu wangu mkubwa akiwa Dr. Mzizimkavu. Hongera sana MziziMkavu kwa kazi yako ya kuelimisha.
Jukwaa jingine ninalopendelea kutembeleai ni Jukwaa la Siasa. Jukwaa hili ni kama ulingo wa ndondi katika siasa za ushindani hapa Tanzania. Washabiki wa vyama viwili vikuu hapa nchini hutoana jasho kwenye jukwaa hili. Mapema kabisa kwenye mwezi wa pili na wa tatu mwaka huu, nikagundua kwamba Jukwaa hili huponza wengi kupigwa Ban. Nikajifunza namna ya kuvumilia cheche zinazowashwa dhidi ya chama ninachoshabikia cha chadema, cheche nyingi zikiwashwa na wadau wawili waitwao@Ritz na chama wa Gongo la Mboto. Nikijisikia kujibu chochote nafanya hivyo kwa uangalifu mkubwa kwa kutotumia jazba yenye lugha ya kuudhi/kukashifu. Namshukuru Mungu nimefaulu kwa hilo katika mjukwaa yote na mpaka leo Mods hawajanikunjia uso
.Kuna msemo: raha ya kitu huwezi kuifahamu mpaka pale hicho kitu kitakapokosekana. Hiyo kwangu ilidhihirika katikati ya mwezi wa tano mwaka huu pale uongozi wa JF ulipofanya marekebisho kwenye mtandao huu. Kwa muda wote ule wa wiki mbili za marekebisho nilipata shida sana na ndipo nilipogundua kwamba JF ni sehemu ya mwili wangu kama yalivyo macho au masikio yangu.JF is highly addictive! JF ni kila kitu bwana
!Nikimaliza Jukwaa la siasa naingia Habari na Hoja Mchanganyiko. Huko nako watu hutoa habari na mambo mengi ya kuelimisha. Kuna thread moja ilinieleza maisha ya watu katika visiwa vidogo zaidi hapa duniani. Niliipenda sana. Nikimaliza huko naenda mmu na cc.
Nikiingia mmu naangalia kama kuna thread ya wadau waitwao Mtambuzi Bishanga au Preta.Nikiikuta naisoma na kutafuta michango ya The Boss au Kongosho. Michango ya hawa, kwangu ni burudani tosha. Cc nako kulinipendeza kipindi Lizzy alipokuwepo. Baada ya Lizzy kupotea, cc imeendelea kung'aa kwa ujio wa mama moto @Lara1.
Stress zangu za maisha nazitibu kwenye jukwaa la jokes! Huko watu wanatoa utani na vimbwanga vya kuharibu mbavu zilizokaa vibaya. Mdau mmoja(simkumbuki jina) sitomsahau kwa thread yake iliyoniacha mdomo wazi kwa mshangao. Alikuwa anawaeleza watu walokuwa wanalalamika eti jina la Magufuli ni libaya! Mdau huyu akaenda nchi nyingine akatuletea majina ya mawaziri wa nchi hizo . Nukuu ya hiyo thread naiweka hapa chini:"
watanzania mnadai Magufuli ndie waziri mwenye jina baya angalia haya sasa;
Jacqueline Natombeka (Utamaduni Sauzi)
Kazakuku Firafisi (Mipango,Japan) ,
David Kinembe (miundo mbinu Kenya)
James Kakuma (Biashara Zambia)
Akaja Akatombeka (Nishati Ghana)
Nalia Namboo (Sheria Botswana)
Antonie Chipumbu (fedha Msumbiji)
Chirambo Kafirwa (Mazingira Malawi)
Rozia Kamkundu (Kilimo ZimbabwJapan)
Naomba nikiri hapa kwamba hayo majina ya mawaziri wa nchi mbalimbali sikupata nafasi ya ku -cross check kama ni ya kweli au ya kubuni.
Pia sikosekani jukwaa la Jamii Photos. Wajuzi wa kupakua picha hutoa picha zenye mafundisho na burudani. Wanaonifurahisha kwenye jukwaa hili ni: Mzizimkavu, Mbuzi Mzee, Boflo, SILENT WHISPER na Ndallo. Ndallo ni maalum kwa picha za kucheza(motion).
Nilichogundua baada ya kujiunga ni kwamba ukimsifia mtu kwenye jukwaa lolote utaandamwa sana.Hilo lilinitokea pale nilipovutiwa na aina ya uchangiaji wa mdau mmoja aitwaye THK DJAYZ.Huyu,akiona thread ni ngumu au haieleweki anachangia kwa kuandika: "Searching……… No Network…" Staili hii ilinivutia kwa sababu haina maudhi au kashfa kama vile kuandika: ‘kichwa chako kina ubongo au matope? Nilipomsifia THK kwa staili ya uchangiaji wake nilihukumiwa hivi: multiple id @work! Na maneno mengi ya kudhihaki kuvutwa kwangu na staili ya uchangiaji ya THK. Nikajifunza kuwa kusifia mtu hapa JF ni ngumu. Jaribu uone.
Kingine kinachoambatana na ugumu wa kusifia ni huu mtazamo wa baadhi ya wadau kupenda sana kuponda thread za wengine kiasi kwamba wanaomba kitufe cha ‘dislike' kiwepo! Salaleh! Kama thread imekuudhi na huipendi iache hivyohivyo au changia kiungwana kwa kusema kwamba hiyo thread hukuipenda na utoe sababu. Wengi hushindwa kuvaa uungwana na huishia kukashifu na Mods wanatoa ban.
Ule msemo wa busara wa: ‘Hakuna swali la kijinga ila kuna majibu ya kijinga' bahati mbaya sana una ukweli hapa JF.Tazama hili swali lililoulizwa hapa Jf kwenye mmu na majibu yaliyotolewa!
SWALI: Wajameni,naombeni mnijuze hasara na faida za kuangalia picha za ngono Huyu anataka kujua ukweli wa mambo yanayohusu picha za ngono.Anataka aelimishwe. Lakini ebu tazama majibu ya hilo swali
JIBU1. Uko darasa la ngapi vile??
JIBU2. Nenda fecebook hapa sio mahala pake jinga sana wewe naukome kutuchafua humu ni thegreat pekee kwendraa
I think Great thinkers should be great teachers! Let's educate these young men who can't tell branches from roots!
Najisikia kupungukiwa sana pale wadau niliowazoea kwa michango yao kutoonekana hapa jamvini kwa muda mrefu.Wadau hao ni: keren Happuch, e2themiza, @Senetor miss Judith na @Excellent. I really miss them.Nawapongeza Mods wote kwa kazi nzuri ya kusimamia jamvi letu na ninawaomba watuletee vitu vipya mwaka ujao wa 2013!
MAISHA BILA JAMII FORUMS HAIWEZEKANI! ASANTENI SANA NA HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA!