Mwaka mmoja baada ya uchaguzi wa 2020, CCM Bado inakwamishwa au imekwama?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
CCM walituambia upinzani wa kupinga kila kitu umekwamisha maendeleo Kati ya 2015 Hadi 2020. Wakaamua kusiwe na uchaguzi kuwe na uchafuzi. Leo hii tunaelekea mwaka mmoja toka wakae wenyewe kwenye kila secta naikiwemo Bungeni. Kwa maoni yako ni kweli wapinzani walikuwa wanawakwamisha au walishakwama kabla hata yakuwaza wanakwamishwa? Je, maendeleo wanayoyahubiri yanazuiwa na wapinzani au yanazuiwa na uwezo wao wa fikra?

Ni sahihi kuona unafilisika ukaanza kuua wanaokua kibiashara ili usionekane unafilisika au Bora ujiweke karibu na wanaokua ili ujifunze na kutumia mbinu zao kudhibiti usifilisike?
 
"Kama hujui unako kwenda huwezi kupotea" ndio kinachoendelea nchini kwetu, yaani kila siku utasikia mikakati ile ile tuliyoambiwa miaka 10, iliyopita ndio leo tena kiongozi anaibuka nayo!!!kipindi cha awamu ya 5!!watu tulidhania labda hii nchi hakuna tena tatizo la matundu ya vyoo, madawati, na madarasa, lakini hebu angalia leo karibu kila siku ndio habari!!!kutokana na viongozi walivyokuwa wanazungumzia mambo makubwa makubwa, kumbe vidogo tu hivi bado!!!
 
Ile Ni propaganda kwa kitaalamu wanaita state craft,mikutano ya siasa Ni Kama health education kwa wananchi yanaboresha uelewa wa wananchi kuhusu masuala mbalimbali,Kama ujuavyi adui wa ccm Ni elimu ndo maana huwezi kuta wasomi wanaojielewa wanashabikia ccm
 
Wananchi tunasingiziwa mengi? Hao wananchi waliokubali tozo wapo wapi? Au ni wananchi hewa? Au ni Mataga? Au ni mazaga? Au ni watanzania wa kufikirika?
 
Back
Top Bottom