Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,951
Kwa kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Habari ambazo nimezipokea dakika hiihii kutoka Buzwagi zinasema kuwa wananchi wa huko wamefunga mgodi wa madini wa Buzwagi wakitaka walipwe fidia. Mtu aliyenipa taarifa hizi anasema kuwa mapolisi wameshakuwa dispatached kwenda huko tayari kwa kuwatawanya wananchi na mabomu ya machozi yalishaanza kupigwa. Kwa kuwa tuna wanachama wetu wa JF pale kwenye mgodi wa Buzwagi, naamini watatuletea habari kwa kina zaidi.
Kitu kimoja kipo wazi kwa tukio kama hili: wananchi wapo tayari kwa mabadiliko. Pengine kunachokosekana ni uongozi wa kuongoza haya mabadiliko. And this is where the challenge lies for the opposition.