Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,952
- 4,326
Tarehe 31 October 2021, waziri wa Nishati, January Makamba akiwa Arusha alitangaza serikali kuanza kununua mafuta ya petroli na dizeli moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wa nchi rafiki, kupitia Shirika la Taifa la Mafuta (TPDC),ili kuondokana na changamoto za gharama kubwa za wanunuzi wa kati na kudhibiti mfumuko wa bei.
Alisema ile azma ya miaka mingi ya serikali ya kununua shehena ya mafuta moja kwa moja toka kwa wazalishaji, sasa imetimia. Mwezi August 2021 wakati bei ya pipa moja kwenye soko la dunia ilikuwa dola 73, makampuni ya kimataifa ambayo huwa yanatuletea haya mafuta, yalituletea kwa bei ya dola 30 kwa kila metric ton moja. Mwezi Desemba 2021 wakati bei ya pipa ikiwa imepanda hadi kufikia dola 86, TPDC waliweza kutuletea mafuta hayo kwa dola 20 kwa kila metric ton moja.
Hivyo kwa sasa wakati bei ya pipa moja ni dola 100, TPDC tuna uhakika wanaweza kuyaleta mafuta hayo kwa bei ya dola 25 kwa kila tani moja ya ujazo badala ya dola 50 tunayoletewa na haya makampuni binafsi. TPDC wakipewa hiyo ruzuku ya Sh 100 billion ya mwezi June, bei ya mafuta haya inaweza kutelemka hadi kufikia Sh 1,500 kwa lita moja na hivyo kupunguza sana huu mfumuko wa bei tulionao sasa. Tazama ukokotaji wa bei hiyo ya Sh 1,500 kwenye thread yangu iliyopita.
Cha ushangaza, nini kimetokea hapa katikati hadi mpango huu umefilia mbali? Yani licha ya serikali kufanya ziara kwenye nchi rafiki zinazozalisha mafuta huko falme za kiarabu, Waziri wa nishati ameshaacha kuongelea mpango huo. Wabunge wetu tunawaomba mumbane aufufue mpango huo haraka iwezekanavyo, hasa katika kipindi hiki kigumu cha vita kati ya USA/NATO na Russia inayopiganwa kwenye uwanja wa Ukraine.

SERIKALI KUANZA KUNUNUA SHEHENA YA MAFUTA MOJA KWA MOJA KUTOKA KWA WAZALISHAJI MAFUTA.
Na Pamela Mollel,Arusha Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) itaanza kununua shehena ya mafuta moja kwa moja k...
issamichuzi.blogspot.com