Mwaka jana Makinda, mwaka huu Dk. Tulia. Kwanini sio Ndugai?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Kichwa kinauma kufikiri juu la hilo.

Mwaka jana Upinzani bungeni walimlalamikia sana spika Anne Makinda juu ya utendaji wake kuwa wa kibabe na wa kukandamiza demokrasia.

Mwaka huu hayohayo yanalalamikiwa kiasi cha kutaka kumuondoa madarakani naibu spika.

Mwaka jana Ndungai alikuwa Naibu spika hakulaumiwa sana kama Makinda. Mwaka huu Ndungai ni spika lakini cha ajabu halalamikiwi sana kama Naibu Dk. Tulia.

Najiuliza shida ni jinsia? au kuna nini? au Ndungai mzuri sana? na je akija spika na naibu kutoka upinzani mmoja wa kike na mwingine wa kiume. je wa kike atachukiza wengi?

KULIKONI?
 
Ndugai japo kuna wakati anawabeba sisiem ila si kama huyu mama... yaani anaonekana wazi kama vile kuna mtu amemwagiza na sii akili yake.
hii nafasi ulikuwa ya zungu.
 
Huyu mama ndio anaizika ccm bila kujua huku kwetu maisha magumu sana kodi zinazidi kila siku mama endelea hivyo hivyo muda utaongea
 
Huyu mama ndio anaizika ccm bila kujua huku kwetu maisha magumu sana kodi zinazidi kila siku mama endelea hivyo hivyo muda utaongea
chadema ilishafeli, labda sumaye akiwa mwenyekiti wa chama mnaweza kutusua!!
 
Hawajui wanatumia mkono wa chuma! Wasubiri hasira za wananchi wa hali ya chini kabisa! Tulia anaona yeye mambo safi anakula mipesa haoni wala hajui shida za wananchi! Hajawahi ona wananchi wanalala uji wa chumvi na hawana tegemeo lolote! Kosa kubwa kuwarudisha ccm ni ile ile usitegemee chochote!
 
Alipewa ubunge kwa ajili ya kazi 'maalumu' na sasa anafanya kazi 'maalumu' kwa ajili ya malengo 'maalumu'. Ila atakuwa na mwisho mbaya sana ktk jamii huko mbeleni!
 
kichwa kinauma kufikiri juu la hilo. mwaka jana Upinzani bungeni walimlalamikia sana spika Anne Makinda juu ya utendaji wake kuwa wa kibabe na wa kukandamiza demokrasia. mwaka huu hayohayo yanalalamikiwa kiasi cha kutaka kumuondoa madarakani naibu spika. mwaka jana Ndungai alikuwa Naibu spika hakulaumiwa sana kama Makinda. mwaka huu Ndungai ni spika lakini cha ajabu halalamikiwi sana kama Naibu Dk. Tulia. najiuliza shida ni jinsia? au kuna nini? au Ndungai mzuri sana? na je akija spika na naibu kutoka upinzani mmoja wa kike na mwingine wa kiume. je wa kike atachukiza wengi? KULIKONI?

Anne Makinda na Tulia wote waliletwa kwa kazi maalum ya kutetea Serikali. Anne Makinda ilikuwa baada ya utendaji wa Samuel Sitta, ambaye Serikali na Chama cha CCM walimuona kama aliwavua nguo na kuwapa upinzani nafasi kubwa ya kujijenga. Binafsi naona wakati ule alifanya kazi nzuri tu na alikuwa anawasaidia bila wao kujua. Lakini niseme tu kwamba Samuel Sitta wa Bunge la Katiba alikuwa balaa, hafai. Tuendelee na mada. Anne Makinda alipambana sana na Upinzani, lakini baadae alifanikiwa kujenga "Chemistry" na wapinzani, na kwa hiyo uliona hasa hapo mwisho walikuwa wanakwenda vizuri kwa wastani. Ndugai ni mtu mwenye msimamo wake, japo anashinikizwa kulinda maslahi ya Serikali na Chama cha CCM. kumbuka wakati wa Escrow, Ndugai aliondolewa kabisa. unajua unapomtuma mtu atetee au alinde maslahi ya upande fulani, kila mtu ana namna yake ya kutekeleza. kuna ambaye atajibakishia angalau heshima yake, na kufanya tu katika maeneo kadhaa. kuna mwingine ndio kabisaa ataziba masikio, atafumba macho, na kutimua mbio.

Hiyo ndio sampuli ya Dr. Tulia. Yeye kaingia kichwa kichwa, amechukua msimamo mkali sana kulinda kila kitu cha serikali. hakuna Chemistry yoyote mpaka sasa hivi, na ndio maana tunashuhudia wapinzani nao wakilazimika kuchukua msimamo mkali. Katika sayansi ya kuweka watu wa kutetea upande fulani, huwa haitakiwi mtu ajitokeze waziwazi kwa namna anayofanya Dr. Tulia. hapo atashindwa kuisaidia Serikali kwa mujibu wa Katiba. anatakiwa kutumia "software" badala ya "hardware". ule ni ukumbi wa Bunge, ambalo lina heshima yake duniani. na wale ni wawakilishi wa wananchi, waliochaguliwa. wanatakiwa kuheshimiwa, tena zaidi kuliko viongozi wa vyama vya siasa ambao japo wanafanya kazi zao kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, lakini hawajachaguliwa moja kwa moja na wananchi. lakini kwa mihemko ya kutaka kuwadhibiti wapinzani, pengine kwa hasira za kutokana na uchaguzi uliopita, na uchaguzi wa Meya wa Dar, heshima ya Bunge imewekwa kando, na tunashuhudia vituko vya karne
 
Ndungai DJ anaogopa kuchezea fimbo mpaka azimie. Anachezea wanawake Tu kwa wanaume anakimbia. Nimuoga kweli kweli. Kamtia Zito kwa Chacha Wangwe hata siwezi kusema
 
Huyu mama hajui siasa.Katika kichwa chake anafikiri wapinzani ni adui.
 
menopouse, ndio tatizo hizi nafasi wangepewa mabinti wa miaka 25 mpaka 35 wangezitendea kazi vizuri sana, ila hali hii ikianza kukunyemelea huwa ina matatizo sana kwa mujibu wa wataalam wa afya.
 
Wakuu habar za majukum kwa kweli hawa kina mama mi siwaelewag kabsa kama MTU na Dada ake ivi, maana aliyoyafanya makinda ndio anayafanya sasa Tulia, sawa wakuu ebu nipeni utofauti wao katika utendaji wa majukum yao hususani bungeni!!!!!!!
[HASHTAG]#Mtz[/HASHTAG]
 
Ni aibu kumfananisha mama anna semamabi makinda na huyu betina anekaa hapo kwa jeuri ya sizonje level ya betina ni makondakta maana jje ya sizonje si lolote sio chochote. Usirudie tena kijana
 
Ni aibu kumfananisha mama anna semamabi makinda na huyu betina anekaa hapo kwa jeuri ya sizonje level ya betina ni makondakta maana jje ya sizonje si lolote sio chochote. Usirudie tena kijana
Anakaa kwa jeuli ya sizonje kweli lakin Mkuu unataka umaanishe mama makinda alikua vema si ndio,
 
Ndugai. Kipenzi cha Wabunge na wafuasi wa Upinzani. Ni nini kimekukumba?
 
Back
Top Bottom