Elections 2010 Mwaka huu Nachagua Chadema ..... rais, Mbunge hadi diwani

KipimaPembe

JF-Expert Member
Aug 5, 2007
1,285
696
  1. Uendeshaji wa Serikali - Chadema imefanikiwa kunishawishi kuwa ukubwa wa serikali iliyopo ni tatizo kubwa la kuendesha nchi hii. Serikali ni kubwa mno na CCM wala CUF hawalizungumziii suala hili kabisa. In fact CCM wameridhika kuwa hali iliyopo ni sawa na hawaoni chochote cha kubadili. Kulipana posho zaidi ya moja kwa shughuli ile ile, Maofisa wa ngazi za juu serikalini (mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi) kutokaa maofisini wakilangua posho za safari na marupu rupu mengine, Kukosekana kwa vigezo vya utendaji vinavyopimika (performance indicators), n.k. Ni chadema tu inayoonekana kuelekeza nguvu zake hapo ambapo naamini ni mojawapo ya core problems zetu.
  2. Kodi na mapato ya serikali - Ni Chadema pekee inazungumzia vyanzo mbadala vya mapato ya serikali kwa kiwango kinachoeleweka na kinachoonesha kuwa wanaelewa tatizo. Utozaji wa kodi ambao haudhibitiwi unasababisha serikali kuendelea kuongeza viwango vya kudi katika vyanzo vile vile kila mwaka bila kungalia vyanzo mbadala. Kwa mfano, kodi ya nyumba (property tax) ni mojawapo ya vyanzo muhimu vya kodi kwa serikali nyingi duniani. Tanzania nyumba zinazotozwa kodi ni chini ya asilimia 10. Biashara ya upangishaji nyumba kwa miji mikubwa kama DSM, Arusha, Mwanza, Mbeya, n.k. ni biashara kubwa mno. Nyumba hazihamishiki!! Wanaopangisha nyumba kama asilimia 95 hawalipi kodi yoyote. Serikali inapata mapato kidogo mno kutokana na wigo wa kodi kuwa mdogo na vile vile ukwepaji wa kodi mkubwa kwenye vyanzo vikubwa kama mafuta, madini, utalii n.k. Ukwepaji huu wa kodi huchangiwa sana na viwango vikubwa vya kodi usioendana na hali halisi. CCM wanakubaliana na hali. Angalau Chadema wanaonesha kutoridhika na hali ilivyo.
  3. Uendeshaji wa bandari zetu. Tanzania ina faida ya kijiografia kwa kukaa pwani na kupakana na nchi nyingi ambazo hazina bandari. Serikali ya CCM imeshindwa kabisa kuendeleza bandari zetu zilizoko pwani ya Bahari ya hindi na kusema ukweli hali ya bandari ya Dar es Salaam inatisha; wizi wa mizigo na ucheleweshaji usio na maelezo. Hadi mizigo ya Congo kusini Mashariki inapitia Mombasa. Kikwete wa CCM alienda bandarini na kutoa kauli za kusikitisha eti wezi wa mizigo bandarini anawajua ila anawapa nafasi wajirekebishe; hadi leo wizi haujaisha na hajasema chochote tena. Ingawa Chadema hawajazungumzia jambo hili kwa undani sana naamini wanaweza kuleta mabadiliko. CCM wakiingia madarakani hakuna kitakachobadirika kwani jambo hili hawalizungumzii kabisa na rais anayewajua wezi bila kuchukua hatua kwa mujibu wa madaraka aliyopewa na katiba hafai.
  4. Rushwa na Ufisadi - CCM wameshazungumza mara nyingi kuwa rushwa hawaiwezi (kumbuka kauli za Msekwa). Katika kampeni za CCM Mwaka 2005 rushwa na ufisadi ilikuwa ni mojawapo ya ajenda zao kuu. Mbali na kuwa rushwa na ufisadi vimeongezeka, kampeni ya Mwaka huu CCM hawazungumzii kabisa mambo haya ya ufisadi na rushwa. Ni kama vile CCM wamekubali kuwa rushwa na ufisadi ni sehemu ya sera zao ama wameamua kuuvalia miwani ya mbao (ili wasiuone kuwa upo). Ni chadema tu inayoonekana kuzungumzia jambo hili kwa msisitizo unaotakiwa na unaoonesha kuwa uovu huu unawakera na watajitahidi.
  5. Matumizi makubwa ya serikali - Serikali ya CCM haina mkakati wowote inaouzungumzia wa kubana matumizi makubwa ya serikali na kuelekeza sehemu kubwa ya mapato kwenye huduma na miradi ya maendeleo. Ni Chadema pekee inayozungumzia kuwa matumizi ya zaidi ya asilimia 75 kuendeshea serikali ni Jambo lisilokubalika na inatakiwa liwekewe breki.
  6. Uendeshaji wa uchumi wa Kibepari - Tanzania sasa hivi ni nchi ya Kibepari na inatakiwa tuseme hivyo kwa maneno, ili tuunde mfumo wa kibepari wa kuendesha uchumi. Kampeni za CCM zimejaa ahadi za tutajenga daraja, tutanunua Meli, tutajenga uwanja wa ndege, n.k. Ahadi kama hizi hazioneshi malengo ya kudumu ya kuendesha mfumo wa uchumi kwa ufanisi. Ahadi hizi zimejaa malengo ya muda mfupi ya kuwaaminisha wananchi kuwa watafanyiwa hivi vitu bila kuangalia mfumo mzima wa uchumi jinsi utakavyowezesha mambo hayo kufanyika! Ni Chadema pekee inayoonesha kuwa kuna haja ya kubadili katiba na mfumo wa uendeshaji uchumi ili kuweza kutekeleza yale wanayoyaahidi.
  7. Mipango ya muda mrefu - Nimechoshwa na jinsi nchi inavyoendeshwa kwa ujumla bila malengo. Viongozi wawili wa CCM waliotangulia; Mwinyi na Mkapa walidhihirisha kuwa CCM kama chama hakina malengo, ila wenye malengo ni viongozi. Mwinyi miaka yake mitano ya kwanza alifanya kazi nzuri (fagio la chuma, n.k.), miaka yake mitano ya mwisho aliitumia kujenga marafiki watakaomlinda atakapoondoka, rushwa na ufisadi ukazaliwa kipindi hiki. Mkapa alifanya mambo mazuri sana miaka yake mitano ya mwanzo (ukusanyaji wa mapato ya serikali, nidhamu serikalini, n.k.) lakini miaka yake mitano ya mwisho aligeuka Nunda asiyesikia la mtu; ufisadi ukaota mizizi ndani ya kipindi hiki. Katika serikali zote hizi mbili CCM haikufanya chochote kuzuia maovu, bali kuyatetea. Nataka mabadiliko kututoa kwenye hii 'vicious cycle' ya ufisadi. Kikwete miaka yake mitano ya mwanzo imekuwa ni kashfa na ufisadi kwenda mbele, miaka mitano ya mwisho taifa litaingia hatarini. Nchi kuendeshwa kwa kufuata matakwa ya kiongozi mmoja ni jambo la hatari ambalo lazima tulishughulikie kwa kuimarisha taasisi zetu, kwani kiongozi mmoja anaweza kununuliwa. Ni chadema pekee inayozungumzia kubadili katiba na kuzipa nguvu taasisi na kudhibiti madaraka ya kiongozi mmoja wa nchi.
  8. Nataka kuona mabadiliko ya kweli - CCM haiwezi kuleta mabadiliko yoyote na imedhihirisha hivyo. Mabadiliko ya kweli yatakuja pale tu kitakapoingia madarakani chama Kingine. Chadema ni Chama Pekee ambacho toka kimeanzishwa kama chama cha Upinzani kinakua na sasa hivi kimefikia uwezo halisi wa kuweza kupewa dola. Mwelekeo ni kuwa Chadema itakua zaidi mwaka huu na sioni sababu ya kutokichagua chama hiki.
 
hahaaaa na mimi napigia chadema hata kama hawangesema hayo hapo juu ...my vote to CHADEMA kuanzia rais,Diwani,Mbunge na hata kungekuwa na balozi wa nyumba kumi
 
Kura yangu ilishakuwa kwa CHADEMA hata kabla ya Slaa kuteuliwa kuwa mgombea Urais. Baada ya kufahamika kuwa Slaa diye mgombea hata familia yangu nzima imeniunga mkono na wote hivi sasa tunasema kuwa 2010 HATUDANGANYIKI
 
Yeah, ofcourse lakini ni lazima tuseme tunachagua nini. Hatuichagui Chadema tu, kwa kuwa tunaichagua. Kuna vitu tunaviamini na tunaona Chadema watavifanya, kwani wanasema, na uwezo tunaona wanao.
 
Watanzania wengi watapigia chadema ila uchakachuaji wa kura; na vyombo vya habari vya serikali feki kabisa vinapotosha umma wa watanzania ili uchakachuaji uwezekane; Nasifu sana mwananchi na wahariri wake; wakaze bout
 
Tuzungumzie sera na mwelekeo. Sasa hivi CCM wanatembea na petty promises. Hizi petty promises wamekuwa wakizitumia miaka nenda rudi. Lakini sasa hivi wana mpinzani makini anaweza kuzitumia petty promises hizo hizo kuwamaliza hivyo wajikaange kwa mafuta yao wenyewe.

Mimi si mwanachama wa Chadema, ila wamezungumzia issues ambazo zinaonesha umakini. Hizi ahadi wanazotoa CCM na jinsi wanavyozitoa ni jambo la kutia aibu. Ahadi zote za 2005 (kama si zote nyingi yake) wanajua hazijatekelezwa, kwa sababu mapato ya kodi yanatumiwa kuendesha serikali kubwa kupindukia.

Watu simply wanagawiana vyeo tu bila kuangalia tija inayoletwa na kuwepo kwa vyeo hivyo. Matokeo yake serikali inaonekana wakati wa uchaguzi. Ahadi nyingi hazitatekelezwa hata wakichaguliwa.
 
Wito wangu ni kwa akina mama wanavojua kulalamika kuhusu manyanyaso wanayoyapata kutoka chama twawala ikifika uchaguzi ndo wakwanza kukata viuno majukwaani cku uchungu umewakamata hamna usafiri mnakumbuka viuno vyenu cku ya kampeni? mwenye macho haambiwi tazama mtaletewa bajaj tyr fulana na kanga mmeshapewa tia akili binti, mama na bibi mnaoishabikia ccm elewa hakuna anayekujali tunataka mabadiliko chagua slaa chagua chadema.
 
Back
Top Bottom