Uchaguzi 2020 Mwaka huu kama umegombea CCM, ukikatwa jina lako huna mbadala, majina yote kutolewa siku ya mwisho na NEC

Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
3,097
2,000
Yaan kwa haya maneno unajiongopea mwenyew
Kama mgombea huyo alitumia njia ya rushwa kupata ushindi huo, unafikiri wakati wa uchaguzi mkuu chama kitakuwa katika hali nzuri ya kumuuza kwa wananchi jimboni?

Maana chama hakitakuwa tayari kutoka hadharani na kumnadi mgombea ambaye si muadilifu, mtoa rushwa na mla rushwa. Sifa kuu ya kiongozi anayetokana na CCM ni lazima achukie rushwa na aoneshe kuwa anaichukia kwa vitendo, kwa maana rushwa ni adui wa haki.

Kiongozi anayetoa na kupokea rushwa hawezi kuongoza kwa haki!
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,586
2,000
Basi kama ni hivyo upinzani wanaweza kushinda majimbo mengi sana mwaka huu kuliko kamati kuu ya CCM wanavyoweza kuamini.
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
8,275
2,000
Wazee wa kusubiri makombo wanatamani kulia!!! Tuliwaambia hawa jamaa wanawezaje kuchukua nchi wakati hata wagombea hawana????

Queen Esther
Hivi unadhani alichoandika mtoa mada kinawezekana? Chama lazima kimtaarifu mgombea wake mapema ili aweze kwenda nec kuchukua fomu kwahiyo wagombea watajua mapema kama wamekatwa ama la, ila tume kutoa majina siku ya mwisho lengo lao kuwakata baadhi ya wagombea kwa kisingizio wamekosea kujaza fomu
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
8,275
2,000
Hoja ya msingi hii, tume na ccm wapi na wapi wakati kuna siku za watu kuchukua form.
Mtoa mada kachanganya hapa kilichopo NEC watatoa majina siku ya mwisho ili kuengua wagombea kwa kisingizio wamejaza fomu vibaya, na wakiwatoa siku ya mwisho ndio picha limeisha
 

Gidbang

JF-Expert Member
Jun 1, 2014
3,332
2,000
Mwaka huu kama umegombea kwenye kura za maoni, ukashinda halafu kamati kuu au wenye chama wakakata jina lako huna mbadala kama iliyokuwepo siku za nyuma, kwamba utakimbilia upinzani ugombee.

Kama mnavyosikia, alisema Polepole na jana pia amesema Waziri Mkuu kuwa kura za maoni hazikua na maana yoyote, maamuzi yote yako kamati kuu, wao ndio watarudisha jina la Mgombea hata kama ukiwa wa mwisho na kura 0 bado unaweza kurudishwa kua mgombea. Na akamhakikishia shehe majini kua atakua mgombea kule Handeni.

Kinachofanyika mwaka huu, kamati kuu ya CCM itapeleka majina ya Wagombea wa majimbo yote Tume ya Uchaguzi kimia kimia. Ikishafika siku ya mwisho ya kurudisha form ya kuomba kuteuliwa na Tume kwa vyama vya siasa basi Tume itatangaza majina ya wagombea wote hivyo kama ulikatwa unakua huna nafasi ya kuhamia chama kingine kwa sababu muda unakua umeshapita.

CCM wanahofia kua wakitoa majina mapema wale ambao hawatakubaliana na maamuzi ya kamati kuu ya chama au maamuzi ya wenye chama basi wanaweza kukimbilia upinzani na hatimae wakapata nafasi ya kugombea na kushinda uchaguzi.

Hivyo kama uligombea kwenye kura za maoni ukawa mshindi kwa kura nyingi, wenye chama wasipokutaka huna mahala pa kukimbilia. Hivyo wagombea wote jiandaeni na matokeo yoyote yatakayokuja.
WATAJUANA WENYEWE HAYATUHUSU SANA WAPINZANI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom