Uchaguzi 2020 Mwaka huu CHADEMA imeonesha udhaifu mkubwa sana hii ni kutokana na pengine walikuwa hawajajiandaa na kampeni

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,174
27,219
Ukweli una tabia ya kujitenga na uongo, mwaka huu CHADEMA imeonyesha udhaifu mkubwa sana hii ni kutokana na pengine walikuwa hawajajiandaa na kampeni za mwaka huu.

Nimeona mapokezi ya MwanaFA kule Muheza na jinsi alivyoandaa kampeni zake pale uwanja wa Muheza.

Mapokezi yalikuwa mazuri sana na zaidi jukwaa na jinsi kampeni zilivyopangika kwa hakika amemzidi mbali sana mgombea wetu.

MwanaFA kwenye siasa bado ni mchanga sana ila kwa jinsi alivyoendesha kampeni zake leo ni wazi kuna la kujifunza kwenye chama chetu chadema.

Sijajua ni nani hadi sasa ana-organize mikutano ya chama, kwa maana imekuwa "too local" unaweza sema mtu anagombea udiwani.

Jana mMwanza tuliona Mwanza picha za juu(zilizopigwa kwa drones), ila Dar tulinyimwa na hata leo huko sShinyanga hatujapewa picha ya juu hata moja.

Tujirekebishe hapo, la sivyo lawama za kuibiwa kura zitakuwa nyingi huku uhalisia haukuwa hivyo

Video hii hapa chini
.
 
Tizama vumbi lilivyotitimka njiani shauri ya kutokuwepo na barabara bora za lami. Halafu unakuta watu hapa na waimbaji wanapusifia maendeleo yaliyoletwa na Magufuli wanataja mambo kama barabara, uwanja wa ndege, ndege mpya na elimu bure.

Wanasahau kuwa yote waliyoyataja ni kwa manufaa ya wao viongozi na vitambi vyao. Barara zote nzuri zipo sehemu zao wanazozitumia kila siku, mlala hoi hana uwezo wa kumiliki gari na kutumia barabara kila siku, uswahilini hakuna barabara bora ni vumbi tu!

Uwanja wa ndege na ndege mpya ni kwa ajili yao pia, ni mlala hoi gani anaeweza kumiliki kutumia usafiri wa ndege wakati kutumia boda boda tu kwenda na kurudi kazini inamshinda? Kuna faida gani ya kuwa na elimu bure wakati hakuna walimu madarasani, na hata waliopo hawalipwi kwa wakati na kwa sababu hiyo nao hawafanyi jitihada yeyote ya kusomesha?

Tumewahi kujiuuliza ni lini tatizo na maji safi na mazingira bora kwa kila mwananchi yatafanikiwa? Ikiwa ishafika miaka 50 ya uhuru na bado mahitaji madogo kama haya bado si wananchi wote wanaonufaika nayo, tusubiri kwa miaka zaidi?

Kuna yeyote aliejiuliza ni lini mafuriko ya kila mwaka mitaani kila msimu wa masika yatapatiwa ufumbuzi? Jawabu ni kuwa hakuna hata anaejadili hili kwa sababu wakubwa na vitambi vyao hawaathiriki, drainage system ya sehemu wanazoishi zinatunzwa vyema.

Watanzania wote wanapaswa kujiuuliza ni kwa nini nchi kama Rwanda ambayo ilijikuta katika civil war baina ya 1990 - 1994 wameweza kusimama kidete na kuijenga nchi yao upya na sana iko mbele sana kimaendeleo kuliko Tanzania? Sisemi kama hawana mafisadi, ila mafisadi hawajawasahau wananchi wao. Mabadiliko makubwa yako wazi kwa kila mtu kuona toka uchumi wa nchi, elimu, nafasi za kazi, huduma za afya, upungufu wa vifo vya wajawazito na watoto wachanga, makaazi, usafiri, life expectation, na bila ya kusahau mapigano dhidi ya umasikini.

Wagombea ubunge wetu wote Tanzania hakuna hata mmoja ambae anaweza kusimama na kujadili hali ya Tanzania na watanzania kwa ujumla na akaweka wazi ni vpi Tanzania inaweza kujipatia maendeleo ya kweli. Wanachofanya woote ni kuhubiri kasumba tu na kudanganya umma.
 
Kwa hiyo umenuna?

Tundu lisu amesema yey ataleta haki na fulaha kwa kuwa viwanja vya ndege mabarabara vilishaletwa na mkoloni na maraisi wengine.
 
Lkn mwaka huu Lumumba mnaokoseshwa usingizi Sana na Chadema. Kwann? Hayo mambo makubwa mliioyafanya wananchi hawayaoni?
 
Ukweli una tabia ya kujitenga na uongo, mwaka huu chadema imeonyesha udhaifu mkubwa sana hii ni kutokana na pengine walikuwa hawajajiandaa na kampeni za mwaka huu.

Nimeona mapokezi ya MwanaFA kule muheza na jinsi alivyoandaa kampeni zake pale uwanja wa muheza.

Mapokezi yalikuwa mazuri sana na zaidi jukwaa na jinsi kampeni zilivyopangika kwa hakika amemzidi mbali sana mgombea wetu.

MwanaFA kwenye siasa bado ni mchanga sana ila kwa jinsi alivyoendesha kampeni zake leo ni wazi kuna la kujifunza kwenye chama chetu chadema.

Sijajua ni nani hadi sasa ana-organize mikutano ya chama, kwa maana imekuwa "too local" unaweza sema mtu anagombea udiwani.

Jana mwanza tuliona mwanza picha za juu(zilizopigwa kwa drones), ila dar tulinyimwa na hata leo huko shinyanga hatujapewa picha ya juu hata moja.
Tujirekebishe hapo, la sivyo lawama za kuibiwa kura zitakuwa nyingi huku uhalisia haukuwa hivyo

Video hii hapa chini
.
View attachment 1556693
Mwanafa ni mtu mdogo sana mbele ya lisu sio size yake kabisa
 
Back
Top Bottom