MTEMI WA KIJANI
Member
- Mar 5, 2016
- 39
- 62
Mpaka sasa kimya tu ni kama serikali imefuta ajira kimyakimya. Katika majukwaa wanatangaza wataongeza na kutengeneza ajira lakini katika vitendo ni zero.Namna majibu ambavyo yamekuwa yanatolewa na serikali kuhusu ajira utagundua mwenyewe katika serikali hii ajira na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma sio kipaumbele kabsa ,
kipaumbele ni kushughulikia watumishi hewa ndio maana kila kitu ambacho serikali imeshindwa kufanya kisingizio kikubwa ni watumishi hewa tu.Vijana wanaomaliza vyuo hawana matumaini ya kupata ajira serikalini maana serikali ya awamu hii hiichukulii suala la ajira kama ni tatizo kubwa,Ikifika kipindi cha uchaguzi utasikia ahadi kibao kwa vijana kuhusu kupewa ajira..
Vijana wamekuwa wanatumika kama mitaji ya wanasiasa kujipatia kura kipindi cha uchaguzi tu, Wanasiasa wakishapita hata hawakumbuki kuwapatia ajira vijana hao.. Huku unasema Vijana wachape kazi huku hutaki kuwapatia mitaji na wengine kuwapa ajira.. Hii ndio serikali ya awamu ya tano,, ajira kwa vijana sio kipaumbele.. Kipaumbele ni kujenga fly over, mabarabara, viwanja vya ndege, kununua ndege, kutimua wafanyakazi na kushughulikia watumishi hewa tu.